Kama unataka kujua thamani ya maisha na kuongeza imani nenda kijijini kwenu ulipokulia

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,099
12,476
Habari za mda huu wakuu,

Leo tukumbushane kidogo kuhusu maisha jinsi yanavyoenda kasi na jinsi yanavyo badilika Maisha ni safari ndefu ndio msemo maarufu na wenye kutilia mkazo wa maisha jinsi yalivyo, kwamba unatakiwa upambane mpaka siku ya mwisho bila kukata tamaa.

Nadhani wote au kwa asilimia kubwa ya watu waliopo mjini either wametokea vijijini(mikoani) au wamekulia huko ndio wakaenda mjini kwasababu mbali mbali kama kutafuta maisha au kwa ajili ya kusoma na kutafuta nafasi za ajira na hatimae wakahamia huko moja kwa moja.

Ila mjini watu wanaishi kama wanyama hawana huruma hawana utu hawana ubinadamu na hata imani hawana na wanaamini pesa ndio kila kitu na akili zao asilimia kubwa zimetawaliwa na pesa wako tayari kufanya lolote kwa ajili ya pesa. Kama unataka kujua thamani ya maisha na kupandisha imani either ya dini au ya kibinaadamu basi tembelea kijijini kwenu ulipozaliwa au kosoma ndio utajua dunia si lolote si chochote tuna pita maisha ya mjini yanatudanganya sana.

Kwasababu zifuatazo:–
1. Vijijini kuna ndugu zetu na marafiki zetu tumesoma nao tumekuwa nao ila sasa hivi wengine wametangulia mbele ya haki na wengine ni vilema wa kudumu angali awali walikuwa wazima wengine hawasikii wengine hawaoni wengine hawana miguu wala mikono mungu atusaidie kwa kweli.

2. Wazee tuliokuwa tuna watania tuna waogopa kipindi tunakuwa hawako tena duniani wameshatangulia mbele ya haki.

3. Nyumba tulizokuwa tunaziona nzuri kipindi tunakuwa zimegeuka magofu wamiliki wengine wametangulia mbele ya haki na familia zimesambaratika.

4. Walimu waliokuwa wanatufundisha wameshazeeka na wengine wametangulia mbele ya haki licha ya ukali na uzuri waliokuwa nao yamebaki majina tu.

5. Wanawake na wanaume tuliokuwa tunawaona warembo na mabishoo wamezeeka na maisha yamegeuka upande wao hawana pakuanzia kibao kimegeuka.

6. Wazee waliokuwa wanasifika wana hela na kazi nzuri sana sasa hivi wameshastaafu wapo vijijini na wengine wamefilisika hawana pakuanzia licha ya ukwasi waliokuwa nao kipindi cha nyuma.

7. Dada zetu mama zetu wamezalishwa na watu waliowazalisha wamekimbia na kuwaachia jukumu la kulea watoto peke yao huku wakipambana peke yao.

8. Ndoa zilizokuwa za mfano na kila mtu alitamani kuwa kama wao wameachana tena kwa kupelekana mahakamani na wengine wapo jela wanatumikia kifungo cha adhabu yao baada ya kutengana.

9. Watoto waliokuwa wanasoma shule za gharama kipindi tunasoma nao sasa hivi wamekuwa mateja na wengine wamekuwa wezi na walevi maisha yamewabadilikia hawana tumaini wala hawaijui kesho yao .

10. Sehemu tulizokuwa tunacheza tukiwa bado wadogo sasa hivi ni makazi ya watu na sehemu nyingine ni makazi ya maji na nyingine zimejengwa sehemu za ibada sehemu nyingine wameuziwa wageni.

Wakuu tuwe na utamaduni wa kwenda vijijini kwetu tulipozaliwa ili tujikumbushe kwamba duniani ni wapita njia tu na kwamba mali watoto wanawake na starehe na ujana ni vitu vya kupita tu hvyo tusijisahau miasha ya mjini wanafanya mtu kuwa katili na kusahau kama kuna kifo.

Mara ya mwisho umeenda kwenu kutumbea lini?

Alamsik.
 
Hii nzuri sana..
Ila mjini watu wanaishi kama wanyama hawana huruma hawana utu hawana ubinadamu na hata imani hawana na wanaamini pesa ndio kila kitu na akili zao asilimia kubwa zimetawaliwa na pesa wako tayari kufanya lolote kwa ajili ya pesa. Kama unataka kujua thamani ya maisha na kupandisha imani either ya dini au ya kibinaadamu basi tembelea kijijini kwenu ulipozaliwa au kosoma ndio utajua dunia si lolote si chochote tuna pita maisha ya mjini yanatudanganya sana.
 
Ni kweli kabisa mkuu, kuna ndugu yetu mmoja wakati tunakuwa ndio alikuwa kama role model wetu, alikuwa mnyamwez hatari dah sijui nn kilitokea kwa yule jamaa. Alibadirika akawa mtu wa kushinda kwenye vilabu vya pombe baadae akachanganyikiwa kabisa.
 
Wengine tumezaliwa Nje ya nchi ulaya Denmark na tumekulia DSM ma a na Yake kijijini kwetu ni DSM hapa
Hapana mkuu vijijini kwetu ni kule wanapotoka wazazi wetu kiasili sio kwa kuishi mkuuu ndio maana misiba mingi ya dar wanasafirisha ila mitandaoni wanajifanya born hiya hiya.
 
Utofauti wa mjini na kijijini unataka uweje mkuu.? Lazima mjini watu wajiachie vykutosha
No hapana mkuu namaanisha tusijisahau sana hata kama kwenu ni hapo hapo mjini nimetolea mfano kwasababu asilimia kubwa tunatoka vijijini.
 
Baada ya maisha kunichapa mjini nikasema ngoja nirudi hom nikamalizie mwaka nyumbani na nipunzishe akili na mwili wangu. Mkuu ulichosema ni kweli nimerud hm nimegundua nilivyokua nayafikiri maisha sivyo yalivyo.
 
Mimi kusema kweli nimezaliwa mjini na nimekulia mjini, huko kijijini kwetu wanaonifahamu na ninaowafahamu hawazidi kumi!
Ila nitarudi tu kijijini kujifunza
 
Wengine tumezaliwa Nje ya nchi ulaya Denmark na tumekulia DSM ma a na Yake kijijini kwetu ni DSM hapa
Ulishirikisha ubongo wako kabla ya kucomment?

Haji Manara kazaliwa Amsterdam, kakulia kariakoo Dar, hii inaondowa uzaramo wake kwamba wana home town kwenye Ardhi ya mababu zake?
 
Kweli kabisa mm kuna watu nilikuwa nawaogopa kwa uchawi walikuwa tishio lkn leo wote wamekufa wamekuwa matuta na wale waliojiapiza kuwa hatutatoboa wao ndo kimewageukia wamechakaa
 
Back
Top Bottom