Tusipangiane maisha kila mtu aishi kwa standard zake

fatherhood

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
530
551
Habar wana JF

Nakerekwa na baadhi ya tabia za watu kuhisi wao ni perfect kuliko wenzao
Inashangaza sana Watanzania, mtu yupo kwenye mtandao wa kijamii tena kwenye Jukwaa la Mahausiano na zaidi kwenye sub-forum inayoitwa ''Love Connect''; lakini kuna watu wanashangaa kuwa mtu anatafuta marafiki wa kuchat nao.

Kipi kinashangaza hapa na kuja na maswali kama ''kwani mtaani kwenu hakuna watu''? Kama wewe unajua mtaani kuna watu kwanini upo Jamii Forums? Kaa na watu wa mtaani kwenu mjadili na kuzungumza huko.

Tuache akili za kufungwa; mtu anahoji eti miaka 30 unatafuta marafiki? Ni wapi wameandika kuwa mtu wa miaka 30 hatakiwi kuwa na marafiki?

Tuache kujifanya kuwa tuna ''standards'' fulani hivi kiasi cha kushangaa namna wengine wanavyoishi. Wewe na standards zako baki nazo mtaani kwako.

Tukubali kuishi maisha tukiwa na utofauti, kama unaona hili analofanya huyu dada sio ''standards'' zako kaa kimya na acha aishi maisha yake.

Tukianza kuwekeana mipaka kwenye maisha, tutapoteza radha ya maisha.

Wapo watu hawaijui kabisa Jamiiforums na wanaishi vizuri kabisa, huna haja ya kumshangaa.

Wapo wanaokwenda Dubai kwa mapumziko mwisho wa mwaka na yupo ambaye hana uwezo hata wa kwenda msitu wa Pugu lakini hawashangaani; kila mtu kwa maisha yake.

Wapo wanasomesha watoto shule IST na hawashangai wakiona mtoto anasoma pale Uhuru Mchanganyiko au Ubungo Kibangu; kila mtu aishi maisha yake.

Kama wewe una marafiki ukiwa na miaka 20 acha anayetafuta marafiki akiwa na miaka 30 aishi maisha yake.

Kuishi ni rahisi iwapo kila mmoja atatambua mipaka na uhuru wa mwingine.

Wewe umepanga nyumba unalipa laki 3 kwa mwezi na mwingine anaishi kwa elfu 30 kwa mwezi na yupo mwingine analipa Milioni 2 kwa mwezi na hakuna haja ya kushangaana.

Kuna mtu kilipo kitanda, ndipo ilipo friji, Tv, kabati na jiko la gesi; na analala na kupata usingizi, ni maisha yake.

Tambua maisha ni yako, usijipe umuhimu kwenye maisha ya mwingine, ishi kwa standards zako lakini usilazimishe watu waishi kama wewe kwa sababu wewe sio ''standard unit'' ya watu.

Siku njema.
 
Povu la foma
Habar wana JF

Nakerekwa na baadhi ya tabia za watu kuhisi wao ni perfect kuliko wenzao
Inashangaza sana Watanganyika, mtu yupo kwenye mtandao wa kijamii tena kwenye Jukwaa la Mahausiano na zaidi kwenye sub-forum inayoitwa ''Love Connect''; lakini kuna watu wanashangaa kuwa mtu anatafuta marafiki wa kuchat nao.

Kipi kinashangaza hapa na kuja na maswali kama ''kwani mtaani kwenu hakuna watu''? Kama wewe unajua mtaani kuna watu kwanini upo Jamii Forums? Kaa na watu wa mtaani kwenu mjadili na kuzungumza huko.

Tuache akili za kufungwa; mtu anahoji eti miaka 30 unatafuta marafiki? Ni wapi wameandika kuwa mtu wa miaka 30 hatakiwi kuwa na marafiki?

Tuache kujifanya kuwa tuna ''standards'' fulani hivi kiasi cha kushangaa namna wengine wanavyoishi. Wewe na standards zako baki nazo mtaani kwako.

Tukubali kuishi maisha tukiwa na utofauti, kama unaona hili analofanya huyu dada sio ''standards'' zako kaa kimya na acha aishi maisha yake.

Tukianza kuwekeana mipaka kwenye maisha, tutapoteza radha ya maisha.

Wapo watu hawaijui kabisa Jamiiforums na wanaishi vizuri kabisa, huna haja ya kumshangaa.

Wapo wanaokwenda Dubai kwa mapumziko mwisho wa mwaka na yupo ambaye hana uwezo hata wa kwenda msitu wa Pugu lakini hawashangaani; kila mtu kwa maisha yake.

Wapo wanasomesha watoto shule IST na hawashangai wakiona mtoto anasoma pale Uhuru Mchanganyiko au Ubungo Kibangu; kila mtu aishi maisha yake.

Kama wewe una marafiki ukiwa na miaka 20 acha anayetafuta marafiki akiwa na miaka 30 aishi maisha yake.

Kuishi ni rahisi iwapo kila mmoja atatambua mipaka na uhuru wa mwingine.

Wewe umepanga nyumba unalipa laki 3 kwa mwezi na mwingine anaishi kwa elfu 30 kwa mwezi na yupo mwingine analipa Milioni 2 kwa mwezi na hakuna haja ya kushangaana.

Kuna mtu kilipo kitanda, ndipo ilipo friji, Tv, kabati na jiko la gesi; na analala na kupata usingizi, ni maisha yake.

Tambua maisha ni yako, usijipe umuhimu kwenye maisha ya mwingine, ishi kwa standards zako lakini usilazimishe watu waishi kama wewe kwa sababu wewe sio ''standard unit'' ya watu.

Siku njema.
 
Upo sahihi Mkuu, ila sisi sio Watanganyika ni Watanzania.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Umesema kweli Mkuu. Jamii za watu maskini wanapenda sana kuishi maisha ya kufanana. Ukionesha maisha tofauti kidogo na wao tu Wana mind sana Yani.
 
Kama unaowaona face to face wameshindwa kukuamini ili uwe rafiki yako

Je sisi ambao hatukuoni utatuaminishije ili tuweze kuwa rafiki zako?

Kiukweli siamini kabisa kuhusu kupata rafiki sijui mpenz mtandaoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom