Kwenye hili mke wangu naomba unisamehe

Kwenye hili mke wangu naomba unisamehe

Mke wangu alipokuwa mjamzito alinitoa jasho siku moja kidogo roho initoke.

Tumeenda pharmacy mara moja akaona sijui mafuta gani(nadhani ya nazi I dont know) akakomaa yanunuliwe. Poa nikanunua.

Heeeeee akataka nimpake miguuni pale pale pharmacy. Ee bana ee watu kibao madada, wamama, wife kitumbo kiko mbele ndiii(alikuwa trimester ya 3, ya mwisho).

Daah nikamtupia jicho, naye akakaza, nikajua hapa hakuna mjadala. Akakaa kwenye kitu mzima mzima, dah!! Wamama na visistaduu vinatoa macho!

Ee bana nikaenda chini mdogo mdogo nikampaka aisee. Nimenuna mbaya!! Baada ya kumaliza nikaona mwenzangu ana lile tabasamu kama nilipomuona siku ya kwanza maishani.

Wale wamama na visista du wakafuraaaahi wenyewe. Moyoni nimekasirika kinyama. Nikapitia ndovu mbili(maana hapo sababu nishampaka mafuta naweza kupiga bia).

Hahaha mapenzi yanafurahisha sana. Mimi namsaidiaga kutandika anashika kule mimi huku ila weekend mara nyingi au kama dogo akisumbua mama akatoka nae natandika tu si haba. After all chumba kikiwa hakijatandikwa kinakera.

Haaaa...
 
Heri yao walobarikiwa hata kupika wanasaidiwa,wengine hata uwe unaumwa lazima tu upike,nyie wanawake wapende sana wanaume wanaowasaidia,wengine hata kunyoosha tu nguo moja hatusaidiwi unaambiwa mahari nilitoa ya nini.
 
mmh...hivi huwa huoni raha sana baadhi ya kazi ukazifanya wewe na ukazisimamia kwa asilimia zote....,

huoni kama hili la kutandika kitanda linakuhusu kwa asilimia 100?

na yeye afanye ipi apate raha? mie napata raha nikimuona yeye msafi, kuanzia ndani mpaka nje, hiyo ni kazi yangu kumuandalia vilivyo safi vya kumpendeza, mbona kitu kidogo hicho jamani, mana kuanzia tukiwa washikaji nikienda kwake nilikuwa nakuta kafanya usafi wa kitanda chake vizuri tu, sasa hivi akurupuke tu kisa kaoa?
 
mazoea yanatabu.....ukiwabachela ulikuwa hutandiki leo utaanzaje?

Mimi nadhani hii ndiyo sababu hasa hiyo ya kuwa mdogo kwa mke wangu who f** cares..!??? She is my wife not maid for heaven's sake...

Ila bana mazoea duh...!!!!
 
Keshasema atasaidia vyote ila kutandika ndo ngoma inogile jama..

Kwn kabla hajaoa mbona alikua anatandika fresh2! Sasa iweje leo aone ugum kumsaidia mkewe kutandika wkt kaz zingne anamsaidia,yn hlo dogo2 ndo limshnde jmn....!!!!!
 
Heri yao walobarikiwa hata kupika wanasaidiwa,wengine hata uwe unaumwa lazima tu upike,nyie wanawake wapende sana wanaume wanaowasaidia,wengine hata kunyoosha tu nguo moja hatusaidiwi unaambiwa mahari nilitoa ya nini.

Kwa jibu hilo apo cdhan km kn upendo,nahc hyo ndoa ni mwendo wa kijeshijesh zaid,ligwaride kwa sana,looh!
 
kijana unafua...unaosha vyombo....hizo ni ndoto kwa wengine..lucky her!
 
kitanda ?

we bacha uko serious kweli haha

wewe ndio wale wanaotengeneza tundu la kuingia na kutoka ktk net wakiwa peke yao looooh!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nadhani hii ndiyo sababu hasa hiyo ya kuwa mdogo kwa mke wangu who f** cares..!??? She is my wife not maid for heaven's sake...

Ila bana mazoea duh...!!!!
unauhalali kabisa kabisa wa ku quote mistari ya Biblia kama signature yako Chief
 
Kitanda kilichokamilika na kutandikwa vizuri shurti kina mauwa. team penny
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom