kaka vyombo kwangu hainipi taabu,
kutandika kitanda lol....Mungu anisamehe bure
Tumetofautiana mkuu. Mi kuosha vyombo labda niburuzwe na tingatinga la manispaa ya Kinondoni.
Ni heri nikapime ukimwi kuliko kuosha vyombo. Mtihani mkubwa wa kitaifa huo.
kaka yangu nikuambie ukweli, hilo ni dogo sana jamani! sasa wakati hujaoa ulikuwa unatandikiwa kindana na nani? pole sana kiukweli ila mi nakuomba msaidie pale anapohitaji kwani hilo ni dogo mno, not to mention ni la ndani sana hakuna ktu atakayejua km wewe ndio umetandika hicho kitanda...km umeweza hadi kufua ambapo watu wanakuona sembuse kutandika kitanda? pole sana ndg yangu, mimi nakutoa hofu kuwa hilo sio suala la kike we msaidie tu waifu.
kweli tumetofautiana kaka,
kutandika kitanda napata kigugumizi lol...,
Ntafanya kila kitu lakini kuosha vyombo anisamehe walah
Labda itokee tu.
sijawahi, mara nyingi wanaume huwa hatuongei maswahibu yetu ya ndani,
tunaugulia ndani kwa ndani,
hata hivyo nimelileta hapa ili nione wadau wengine wanalionaje lol...
Nako ni ka mtihani. Wife akisafiri, shuka na neti alivyoviacha ndo atakavyovikuta. Ndo maana safari zake simshauri zizidi siku tatu.
İla potelea mbali ntatandika kitanda kama hayupo, ila kama hayupo kuliko nijipikie afu nioshe vyombo, acha tu niwe mteja wa mama ntilie. Potelea mbali. liwalo na liwe.
hili halina shida wajameni
issue kutandika kitanda.......moyo unanisuta kabisa
daaaaaaahhh pole mkuu bacha ila usiogope kutandika kitanda wala haina shida wala tatizo lolote sema tu ni wewe umejiwekea kasumba hiyo ambayo haata ukitaka sasa hivi uachane nayo unaweza iacha na kuisahau kabisa,kitanda wala hakijakaa kike mkuu,maanke kingekuwa kimekaa kike nafikiri wanume wangekuwa hawalali kwenye vitanda,kwa hiyo kama vipi we anza tu kujizoesha kutandika kidogo kidogo hatimaye utaona kila kitu kiko sawa.
mmmmhhh haya banah,je akikugomea kukupa naniliu mpaka umsaidie kuosha vyombo utafanyaje?bado utagoma?
ahaaaa! unakosa uhondo bacha! kutandika kitanda kuna raha yake hasa kama ulikitumia ipasavyo, zile hisia za shughuli nzima ilivyokwenda zitakuja kichwani na kukuletea raha, unaweza kujikuta unatamani ukitumie tena muda ule ule. Kutandika kitanda hasa kwa mwanamume ni moja ya vitu vinavyohamasisha kuendeleza shughuli... fanya uchunguzi then utanipa jibu