Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Kuna siku mdada mmoja ndugu wa mme ananiambia "wifi naomba kesho uje kwangu unisaidie kukaa na watoto nitakua na shughuli fulani"
Kimoyo moyo nkajisemea qmaneenah, yani nimuache mme ndani, na mtoto pia nakuja kusaidia wifi kumwangalizia watoto shwain kabisa!!!!

Umekuwa yaya ghafla!!
 
Wifi unakaa kung'ang'ania kuishi na kaka yako si utafute mji wako au unataka uolewe na kaka yako? Umeshakuwa mtu mzima anza maisha yako ili na wewe upate wako. Kubanana na kaka yako kila saa mnaoishana kwenye korido sio deal....

Utaambiwa hujui walikotoka, umekuja umewakuta ha ha
 
Tukimaliza tunahamia kwenu mashemeji mnaonyoosha tu miguu kwa kaka zenu mkitazama tv hata majani nje hamlimii
mkifika kwa mashemeji mnistue.., habari ya njemba ingine kuangalia makalio ya mke wangu anavyopita pita siyawezi kbsaaaa..., mi nashindwa kumsifia mke wangu vzr bana.....,
Zaidi pale nnapoukumbuka wimbo wa Manfongo

hiyo ya mawifi nyie endeleeni tu mnawezanaga wenyewe.
 
Sawa kabisa, haki sawa kwa kila binadam. Tena waache ujinga wao hakuna aliyeolewa na familia, tukilala tulale wote kazi tufanye wote alaah
Habari ndio hiyo, kama ni njaa uzuri itatuuma wote. Kwahiyo wasijitoe ufahamu tu.
 
Mi naona kila mtu awe anafanya mambo yake mambo ya kusaidiana ndio yanaleta kesi
 
Two ways traffic,kaka anajua anao ndugu zake na wifi anajua pia kuwa wapo. Kila mtu ana nafasi yake .mke awe mke na dada awe dada,usikabe zote.
 
mkifika kwa mashemeji mnistue.., habari ya njemba ingine kuangalia makalio ya mke wangu anavyopita pita siyawezi kbsaaaa..., mi nashindwa kumsifia mke wangu vzr bana.....,
Zaidi pale nnapoukumbuka wimbo wa Manfongo

hiyo ya mawifi nyie endeleeni tu mnawezanaga wenyewe.

Umenifanya nicheke kwa nguvu!!

Aaah hii mtuachie kwakweli, tunawezana.
 
Hata kama hujaolewa una uwezo wa kuwa busy na mambo yako ya kukuletea maendeleo na ukafanikiwa. Kinachowakosanisha watu ni ile kukariri kuwa kwa vile kaka ana mali ni halali yako wifi unakaa kiboya bila kujishughulisha ukitarajia kutimiziwa kila kitu na kaka yako ili hali na yeye ana majukumu yake. Lawama inakuja kwa mke kuwa ndie anayemnyima mume wake kuwasaidia. Kila mtu akitambua majukumu yake na akayafanya kwa bidii hata huyo wifi yako ndie atakusaidia kumwambia kaka yako akusupprot unaposhindwa. Na vile vile mawifi achene maneno maneno kwani ukikaa kimya kuna shida? Mnajijengea uadui na mke wa kaka yenu wenyewe. Mnamsema weee baadae anapata hayo maneno je ataendelea kukuchekea. Kuwa busy ukishafikisha miaka 18 wewe ni mtu mzima acha uzembe fanya kazi kwa bidii utaona matunda yake. Kwa kaka yako nenda kwa mwaliko wao au basi surprise then usikae mpaka unaleta kero kwani huko kwako huna kazi za kufanya? Ni hayo tu.
 
mkifika kwa mashemeji mnistue.., habari ya njemba ingine kuangalia makalio ya mke wangu anavyopita pita siyawezi kbsaaaa..., mi nashindwa kumsifia mke wangu vzr bana.....,
Zaidi pale nnapoukumbuka wimbo wa Manfongo

hiyo ya mawifi nyie endeleeni tu mnawezanaga wenyewe.
Khaa wivu huo si wa nchi hii
 
Back
Top Bottom