Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Inasikitisha sana...

Tabia ya mtu unaiona pale pale mwanzo... Kama ukiamua kufunga nae pingu za maisha... Own your own risk...

Cc: mahondaw
 
Mie siingilii ndoa ya kaka zangu, na mtu asiniingilie kwenye yangu.
Yaan wangejua ni kwa kiasi gani tunavyofight kulinda ndoa zetu angalau tupate amani furaha na upendo japo kwa asilimia sabini tuu wasingejishaua kutaka kutuelekeza yakufanya, jamani mawifi zangu naomba niwaeleze ukweli hakuna kitu kinauma kama mume kwahiyo naomba msiingilie ndoa yangu kwakuitia dosari tuachani tuishi tupendavyo na sio tuishi nyie mtakavyo.
Ushauri wa bure
Jitahidini muolewe na nyie muonje tamu na chungu, ndoa sio lelemama tusichukuliane poa.
 
Kakako akio jua Wifi wewe ni mtu wa kupita tu maana nawe ujiandae kua na mji wako badala ya kukaa na kubinyana mapaja na kakako kwenye kochi kwa mbanano, mawifi mtulie muache meno ya Mbele kung'ata ng'ata ndoa za kaka zenu maana ufanyalo nawe utafanyiwa muda wako ukifika!! Ninachoshukuru wifi yangu ni kigego
Mbona wewe dada zako na Kaka zako hawawi wa kupita??

Wanawake mmeumbiwa roho mbaya tu na ubinafsi.
Ndugu zangu wakiomba, ooh tutachelewa maendeleo Ila ndugu zako wakiomba haina Shida.
Lililoongelewa hapo juu Ndio ukweli wenyewe bahati mbaya hata wale wanaolalamika kuhusu Kaka yao nao wanafanya hivyo huko walikoolewa.

Huwa Wana bahati mbaya zaidi wale wanaozaa watoto wa kiume tu.
Ni hasara tupu
 
Tatizo lako unaishi kwa shemeji yako ndio maana huelewi somo!! Hakuna anayekataa kuombwa au kuomba msaada ila isiwe ndio sababu ya kumpanda kichwani mke wa kaka yako
Ndoa ni maelewano hivyo omba msaada kwa kaka yako alafu muachie akajadiriane na mkewe wewe subiri jibu,ukiwa hivyo hautogombana na Wifi yako ila ulitaka kujiona wewe ndio zaidi kwa kakako utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua
 
Yaan wangejua ni kwa kiasi gani tunavyofight kulinda ndoa zetu angalau tupate amani furaha na upendo japo kwa asilimia sabini tuu wasingejishaua kutaka kutuelekeza yakufanya, jamani mawifi zangu naomba niwaeleze ukweli hakuna kitu kinauma kama mume kwahiyo naomba msiingilie ndoa yangu kwakuitia dosari tuachani tuishi tupendavyo na sio tuishi nyie mtakavyo.
Ushauri wa bure
Jitahidini muolewe na nyie muonje tamu na chungu, ndoa sio lelemama tusichukuliane poa.
Ha haa sawa mama mawifi tumekusikia
 
Hahahahaha

Unakuta shemeji hata sahani aliyolia hatoi

Kama kapogwa superglue kwa kochi

Pembeni unakuta kikombe cha asubuhi cha chai na sahani ya asubuhi mchana na usiku

Bila kusahau glasi za maji na juicy[emoji15] [emoji15] [emoji15]
Kisha anainua pmb kwenda kulala, afu mtu wa hivi uishi nae umpende.....sijui unampendea nini
 
Kaa kwa mamako na babako kama unaye, kabla kaka hajaoa ulikuwa unaishi wapi hadii uumie roho hivyo? Wifi/ shemeji wa pande zote nendeni salimieni kaka/dada zenu kisha mrudi kwenu. Unakaaje kwa kaka/dada bila sababu ya msingi? Tuheshimu ndoa na familia za watu. Mawifi zangu hawajawahi kujuta kuolewa ukoo wetu nikienda kwake mda mchache nasepa wajuane na bwanake tunaishi vizuri sana maana siwakeri hovyo
 
Shida ni pale uolewe na mume ambaye ndio mwenye pesa kwao wengine wawe hawana kazi au pesa.hapo ndo uwifi mbaya unapoanzia naona
 
Hii thread kiboko ama kweli mawe yanarushwa gizani......ukisikia waiiiiiiiiiiwaiiiiiiii jua limewapata!!!!!!!!!!! Tehe tehe kaaaz kweli kweli....
 
Mi nina kaka mmoja, kwa hiyo wifi mmoja,
Nimeolewa pia kwa mume wangu nna wifi mmoja. .
Kila mtu na maisha yake, kufuatiliana NO
 
Back
Top Bottom