Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Shida ni pale uolewe na mume ambaye ndio mwenye pesa kwao wengine wawe hawana kazi au pesa.hapo ndo uwifi mbaya unapoanzia naona
Tunakomaje usiombe upate ukoo wa panya baba mkubwa baba mdogo sijui shangazi sijui mjomba unaambiwa hatubaguani utaomba poo mtu anakuja kusalkmia anabeba mpaka majirani binamu huyu ni jirani yetu tunaishi naye kama ndugu
 
Mawifi wengi ( ndugu upande wa wanaume) wanaboa.
Unakuta wifi anataka anyenyekewe kama vile yeye ndiyo Mume.
Pia kumridhisha binadamu ni kazi sana maana mazuri 1000 hufutwa na baya moja.
Nyie hamjui kaka yenu akishaoa majukumu yanaongezeka? Mnataka mchote tuu hela tusiwe na maendeleo ? Mwishowe mseme mwanamke nuksi?
Binafsi mawifi huwa nawachukulia watu wa kawaida sana.

Aya sasa jembe kwa jembe,mwaka uu lazima tuvune ngano,
 
Naye akae kwa mmewe ili naye wakampige vibomu wenyewe kutwa mizigo kichwani kwa kaka wifi anavumilia[emoji23] [emoji106] [emoji106] [emoji23] [emoji106]
anakaa na mume basiiiii....yupo yupo tuu haishi majanga na kuomba pesa!
 
Mnajuana nyie mnashindanA kwa roho mbaya tu
Uwe dada yako halafu aolewe na familia yenye gubu utamuonea huruma au wewe dada zako wawe wana mpelekesha mkeo ukirudi jioni yupo hoi kisa wifi shemeji nafanya kazi wao wana angalia TV wanafatilia makinikia ya magu
 
mwenzie nahangaikaaaaa nauza mpaka ubuyu wa mia mia! ili mradi maisha yasonge...yeye anakula vya kaka tu! hana mda huo....yaani anatushinda matumizi! ukienda kwake utashangaaa hivi ni huyu anaesema hana hela hata ya kula...ana maisha mazuriiiii
 
Kusaidia lazima asaidie ndugu zake ,wazazi wake sio aegemee tu kwa mke,napinga kabisa hilo ,kumbuka wamemlea na ndugu zake wamekua pamoja
Kuhusu kunyenyekea hayo ni ya kurekebishana tu,,lakin mume kusahau kwao asisaidie haikubaliki hiyo
Cc Mwanamutapa
Unajua mambo haya yapo pande zote unaweza kuta hata huyo mke mwenyewe hapewi hata sent ila kwasababu mme hatoi hela anapeleka kwa mkewe wake wanabebaga lawama ambazo sio kabisa
 
Shost mie siwezi kubali kisa watoto waa hapana waanze wangu halafu wakisha maliza huwaoni hata salamu utasikia aunt mchoyo bila uncle tusingesoma simu kwa mjomba hapana kutoa tutoe inapowezekana sio mme anapata stress anashindwa mpaka majukumu, ila jamani family zetu za kiafrika ni pasua kichwa
Tutafanyaje sasa na sie ndio waafrika!! Akili tu kumkichwa.
Hatukatai kusaidiana lkn sio kwa kulazimishana na masimango juu!!!
 
Kusaidia lazima asaidie ndugu zake ,wazazi wake sio aegemee tu kwa mke,napinga kabisa hilo ,kumbuka wamemlea na ndugu zake wamekua pamoja
Kuhusu kunyenyekea hayo ni ya kurekebishana tu,,lakin mume kusahau kwao asisaidie haikubaliki hiyo
Cc Mwanamutapa
Tatizo sio kusaidia, tatizo ni kutambua mipaka ya hiyo misaada. Mwanaume akishaoa majukumu yanaongezeka, hivyo ndugu pia wanapaswa waelewe kuwa mambo hayatokuwa sawa kama zamani. Wakubaliane na mabadiliko, watasaidiwa kwa nafasi inayopatikana sio kwa kulazimishana.

BTW ukiwa na ndugu waswahili hilo somo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
heeee wifi yeye kila siku anaolewa na kuachwa! hakai na mume......anichosha hivyo vizinga kwa kakake.....kakake mwenyewe hali tete me mwenyewe huwa namuoneaga hadi huruma kwa kweli! lkn sister ake akitaka hata kukopa atakopa! after few dakika kaka unamuona kashika tama asema hela hana! namchombeza anakuwa normal! nmevumiliaaa sasa naona roho inaniuma! wifi haishi vi birthday party n.k full bata! sisi huku kwetu kajamba nani! wifiiiiiiiiiiiiii punguzaaaaaaaaaa unanikandamiza mm na wananguuuuuuuuuuu!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Halafu wengi wao wakishaolewa wanasahau kutoa zawadi hizo! Hawana tofauti na wanasiasa na mgao wa chumvi wakati wa kampeni wakichaguliwa nduki. Ila tuache utani kujipendekeza nako ni kipaji mm siwezi, wewe unaweza kuwa nafuu compared to me teh!
Nakweli kujipendekeza nako ni kipaji, unatakiwa watu wawe na shauku ya kukuona kila siku kiguu na njia hata barua bado kwa kweli ni moyo
 
Tunakomaje usiombe upate ukoo wa panya baba mkubwa baba mdogo sijui shangazi sijui mjomba unaambiwa hatubaguani utaomba poo mtu anakuja kusalkmia anabeba mpaka majirani binamu huyu ni jirani yetu tunaishi naye kama ndugu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Waafrika tuna safari ndefu kweli. Sijui nani alituroga!!
 
Unajua mambo haya yapo pande zote unaweza kuta hata huyo mke mwenyewe hapewi hata sent ila kwasababu mme hatoi hela anapeleka kwa mkewe wake wanabebaga lawama ambazo sio kabisa
Wakati mwingine unakuta pesa zinaishia kubet au kwa michepukooo, ila lawama kwa wifi!
 
mwenzie nahangaikaaaaa nauza mpaka ubuyu wa mia mia! ili mradi maisha yasonge...yeye anakula vya kaka tu! hana mda huo....yaani anatushinda matumizi! ukienda kwake utashangaaa hivi ni huyu anaesema hana hela hata ya kula...ana maisha mazuriiiii
Basi wifi yangu, sirudii tena jamani. Nisamehe tu
 
Back
Top Bottom