Ni vema Chadema ikaweka wazi jambo hili ili lieleweke , ni kweli kabisa kwamba kuna kampeni imesambazwa dunia nzima ya kumchangia Mh Lissu baada ya mawakala wa shetani kuzuia mshahara wake , watu wameanza kuchanga kwa kishindo sana , tunashukuru sana na kwa kweli tunamuomba Mungu awajazie palipopungua.
Lakini ni vema michango hii isitokane na wanaccm , na kama kuna mwanaccm amechangia mpaka sasa basi ARUDISHIWE PESA ZAKE , tunahitaji mchango lakini hatupokei pesa za majini , hatupokei hela zilizojaa damu , hizo hapana , hatuzitaki , Kupokea hela za mchango wa Mh Lissu kutoka kwa wanaccm ni sawa kukufuru Mungu , ni kumdhalilisha Lissu mwenyewe , hii haina tofauti na KUTAKATISHA PESA , Tusikubali
Naomba kuwasilisha.