Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 612
- 1,131
Wanabodi, Asalaam Aleikhum, Tumsifu Yesu Kristo, Bwana Yesu Asifiwe, Shalom.
Ama baada ya salaam nilejee kwenye mada yangu ya siku ya leo ambayo msingi wake nikuongelea hizi zinazoitwa shule za madhehebu mbalimbali ya dini hususani Wakristo.
Tuwapo makanisani tumekuwa na michango na harambeee nyingi sana kuchangia miradi mbalimbali inayoendeshwa na makanisa yetu, kama vile ujenzi wa shule, vyuo na hospitali.
Mimi huyu huyu muumini unakuta natoa kwa moyo wa dhati kabisa kufanikisha miradi husika lakini wakati huo nikitoa asilimia 20 ya pato ghafi kama zaka na sadaka, baada ya hili nitatakiwa kuchangia ujenzi wa kanisa linalotarajiwa kuanzishwa mtaa wa jirani, nitatakiwa kuchangia ujenzi wa shule ya kanisa ambayo itaendeshwa kwa mchepuo wa kiingereza maarufu kama English media na shule ya sekondari.
Kibembe kinaanza pale shule inapokuwa imekamilika mimi nilie changia ujenzi sina uwezo wa kumudu kulipia ada inayotakiwa, matokeo mwanangu au wanangu watasoma Kayumba bila kujali kama mimi nilishiriki kujenga hiyo shule kwa mali zangu.
Na endapo nitamudu kulipa ada lakini kwa bahati mbaya ikatokea kipato kimeteteleka kidogo iwe kwa sababu zozote zile ikiwemo ugonjwa shule zimekuwa hazina subira wala msaada kwa mtoto zaidi ya kumtimua shule.
Nina ushahidi ambapo katika shule flani ya dhehebu ambalo sitaki kulitaja mzazi mwenzetu alipata ajali siku anatoka kumpeleka mtoto wake shule na akawa amefariki, term iliyofuata mtoto yule aliyefiwa na mzazi akasimamishwa shule kwa sababu ya ada bila kujali alikuwa anakaribia kufanya mtihani wa mwisho.
Hivo kupitia group la wazazi tukalazimika kuchanga ili angalau huyu mtoto amalizie pale alipoachia babake. Yumkini mtu huyu michango yake imefanya mambo makubwa sana kuimarisha taasisi.
Jambo lingine hizi shule zimekuwa na michango mingi mingi ili tu kutunisha mifuko, shule ya private nimelipa tution fee, bado unakuja na ngojera za remedial, mara taaluma, yaani wanabadilisha terminology ili hali kitu kile kile.
Ukiachana na hilo kuna suala la usafiri kwenda na kutoka shule wakati wa likizo, shule inaweka mashariti kuwa mtoto akitumia usafiri wa binafsi hatopokelewa shuleni, wakati wa likizo wengine tunawaruhusu watoto kutembelea babu zao.
Imagine mtoto anasoma Arusha au Moshi na bibi au babu yuko huko. Mzazi niko Dar au Mwanza kwamba lazima mtoto arudi tena kwenye domicile ili tu kupanda basi lilokodiwa na shule. UJINGA MTUPU.
ADA Unakuta ada ni shilingi milioni mbili laki saba, mhura wa kwanza ni milioni moja na laki tatu hamsini, nimeweza kulipa milioni moja na laki 2 imebaki tu laki moja na nusu mtoto anazuiwa kupanda basi la shule kwa sababu tu ya shilingi laki moja na nusu ili hali ndo kwaanza JANUARY.
Hawa ma headmaster wako serious kweli? Na wakati huo wengi wa Headmasters na Headministress kwa hizi shule ni ama wachungaji, Padri ama masista. Hebu acheni hizi roho za kishetani wapendwa.
Mtanisamehe kwa lugha niliyotumia, sina lugha nyingine zaidi ya hii kwa sababu nimevumilia hadi mwisho.