Kama Tundu Lissu tulimchangia tena akiwa mbunge kwanini iwe nongwa kumchangia Profesa Jay ambaye hayuko Bungeni?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Kwanza kabisa niipongeze Serikali hususani Rais Samia, Waziri Ummy na Katibu mkuu Prof Makubi kwa Upendo mliouonyesha na hatimaye serikali kubeba jukumu la kumtibu Prof Jay.

Kadhalika niwaulize wale pingapinga, mbona Tundu Lissu alipopata mitihani ya kidunia na kulazwa Nairobi tulimchangia na ni Rais Samia huyu huyu akiwa makamu wa Rais ndiye kiongozi pekee wa dola aliyethubutu kwenda Nairobi kumjulia hali na kumchangia matibabu!

Kwanini leo anapomtibu Jay inakuwa nongwa?

Kwani Tundu Lisu wakati tunamchangia alikuwa hana fedha au watanzania tuliona lile tatizo ni kubwa hivyo tumpe ushirikiano?

Pinga pinga acheni hizo kuna maisha nje ya siasa bhana!
 
Akili zenu fupi na ndio maana hamna suluhu ya maana/kudumu kwa matatizo ya watanzania.

Jiulize ni watanzania wangapi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu?

Hamna mkakati wowote wa maana kuhusu vyanzo vya mapato kwa Bima ya kila mtanzania kwani akili zenu zinawaza kukopa tu na kujenga vitu vinavyoonekana machoni mwa watu(barabara, madaraja, n.k) ili mjitafutie umaarufu wa kisiasa na sio kubuni njia za kuwezesha kuwa na vyanzo vya mapato kwa Bima ya kila mtanzania na mambo mengine ya aina hiyo.

Halafu Lissu kama Mbunge unadhani alipaswa kuchangiwa au kutibiwa na Bunge kama sheria inavyoelekeza?

Kuhusu Bima kwa kila mtanzania, niliwashauri kupitia hapa JF ila akili yenu iliishia kwenye tozo za lazima tu.

Pathetic creatures!

Serikali si imeshampa matibabu bure?Lissu hakupewa matibabu na serikali pesa zake bunge waligoma kumlipa ulitaka atibiwe na mwawe, halafu ni two differwnt cases, yule alipigwa risasi na ccm kwa hiyo huruma ya wananchi kwake ilikua kubwa tofauti na J yeye anaugu magonjwa ya kawaida kama wananchi wengine jimboni kwake
 
Kwani serikali haijui kwamba kuna maskini ambao hawana hata uwezo wa kugharamia vitanda katika hospitali za umma na bado hawajasaidiwa?

Mara ngapi hata maiti zilizuiwa hospitalini kwasababu ya madeni?

Binafsi sipingi profesa J kuchangiwa na serikali lakini isionekane kwamba serikali imefanya jambo kubwa sana wakati imetumiatu kigezo cha umaarufu.

Ingependeza zaidi kama wangesema hii ni wiki ya serikali kuwasaidia wagonjwa wote wasiokua na uwezo waliolazwa hospitali za rufaa angalau kwa zaidi ya wiki.
Au ingependeza zaidi wasingeutangazia umma kwamba watachangia matibabu ya profesa J. Wanazidi kuleta matabaka kwa wagonjwa wasiojiweza kiuchumi. Bora wangekaa kimya

Namuombea profesa wa michano mzee wa vina apone haraka aendelee na majukumu take. Aaamin
 
Serikali si imeshampa matibabu bure?Lissu hakupewa matibabu na serikali pesa zake bunge waligoma kumlipa ulitaka atibiwe na mwawe, halafu ni two differwnt cases, yule alipigwa risasi na ccm kwa hiyo huruma ya wananchi kwake ilikua kubwa tofauti na J yeye anaugu magonjwa ya kawaida kama wananchi wengine jimboni kwake
Chadema walikataa Lisu asitibiwe na serikali Muhimbili.

Lakini pale Dodoma goverment hospital walipookoa maisha yake alitibiwa na serikali hii hii inayomtibu Jay!
 
Kwanza kabisa niipongeze serikali hususani Rais Samia, waziri Ummy na Katibu mkuu Prof Makubi kwa Upendo mliouonyesha na hatimaye serikali kubeba jukumu la kumtibu Prof Jay.

Kadhalika niwaulize wale pingapinga, mbona Tundu Lisu alipopata mitihani ya kidunia na kulazwa Nairobi tulimchangia na ni Rais Samia huyu huyu akiwa makamu wa Rais ndiye kiongozi pekee wa dola aliyethubutu kwenda Nairobi kumjulia hali na kumchangia matibabu!

Kwanini leo anapomtibu Jay inakuwa nongwa?

Kwani Tundu Lisu wakati tunamchangia alikuwa hana fedha au watanzania tuliona lile tatizo ni kubwa hivyo tumpe ushirikiano?

Pinga pinga acheni hizo kuna maisha nje ya siasa bhana!
Naunga mkono hoja.
P
 
Hii tabia ya wivu sijiu itaisha lini miongoni mwetu.... Watoe michango hatulalamiki why we usiyetoa unaumia ... na kuchangia sio mpaka usiwe na hela ni mshkamano wa jamani
 
Akili zenu fupi na ndio maana hamna suluhu ya maana/kudumu kwa matatizo ya watanzania.

Jiulize ni watanzania wangapi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu?

Hamna mkakati wowote wa maana kuhusu vyanzo vya mapato kwa Bima ya kila mtanzania kwani akili zenu zinawaza kukopa tu na kujenga vitu vinavyoonekana machoni mwa watu(barabara, madaraja, n.k) ili mjitafutie umaarufu wa kisiasa na sio kubuni njia za kuwezesha kuwa na vyanzo vya mapato kwa Bima ya kila mtanzania na mambo mengine ya aina hiyo.

Halafu Lissu kama Mbunge unadhani alipaswa kuchangiwa au kutibiwa na Bunge kama sheria inavyoelekeza?

Kuhusu Bima kwa kila mtanzania, niliwashauri kupitia hapa JF ila akili yenu iliishia kwenye tozo za lazima tu.

Lisu alipaswa kulipiwa na Chadema kwa sababu ndio walimpeleka Nairobi bila kufuata utaratibu wa Wizara ya afya.

Sisi tulimchangia kwa sababu za kibinadamu tu!
 
Sawa mzee wa gorofani drive in
Maana hata wewe uko kwenye list
Ya kuchangiwa,ikitokea

Ova
Hawajiulizi kuna watanzania wangapi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu na badala yake wanajisifu kwa kuchagua nani agharamiwe na serikali na nani aachwe afe kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.
 
Yaani unaongea kwa Roho iliyokosa Upendo utadhani huyo Prof Jay siyo kiongozi wako hapo Chadema!
 
Chadema walikataa Lisu asitibiwe na serikali Muhimbili.

Lakini pale Dodoma goverment hospital walipookoa maisha yake alitibiwa na serikali hii hii inayomtibu Jay!

Aisee. Unapenda sana kuanzisha ligi na “CHADEMA” wa JF. Seems siku ikipita bila kuwasikia “CHADEMA” kwako haijakamilika. Basi ni vyema sana.

Btw usisahau kuwa pinga pinga wa awamu hii ni kina polepole. Na Prof J bado ni CHADEMA. Wasiliana na Mnyika kupata mtazamo wa Chama.
 
Mkuu mrangi , duh...!. Umenikumbusha mbali, ma fletini Diraivini!. Wewe ulikuwa unakaa fleti lipi kwa nani?.

Hayo mengine ni kuomba tuu Mungu atunusuru maana...!.
P
Wapi bana sisi ndiyo tulikuwa wajanja wenu
Huko,nyie watoto wa magorofani si mlikuwa kama mabroiler😂😂
Unamjua Victor--- wazee wake nao kama wazee wako tu

Yah kweli magonjwa mengine syo ya kuyaombea ukipigwa basi mtihani

Ova
 
Aisee. Unapenda sana kuanzisha ligi na “CHADEMA” wa JF. Seems siku ikipita bila kuwasikia “CHADEMA” kwako haijakamilika. Basi ni vyema sana.

Btw usisahau kuwa pinga pinga wa awamu hii ni kina polepole. Na Prof J bado ni CHADEMA. Wasiliana na Mnyika kupata mtazamo wa Chama.
Hahahaaaa...... Sisi ndio tuliasisi Chadema pale kisutu majamatini Keys tours!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom