Kweli Tanzania hakuna Pesa?: Huyu ndiye Mtanzania anaemiliki Gari la Tsh Bilioni Moja

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

"HII sasa ni kufuru!" Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.

Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.​

Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.​

Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.​

Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.

Ameinunua kwa bei gani?

"Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.

Alipolinunua

"Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.

Spidi ya gari

"Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.

Matumizi ya mafuta

"Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.

Usumbufu anaoupata

"Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.

"Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.

"Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha," anasema Mosha.

"Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha," anasema Mosha.

Sijawahi Kumsikia Huyu Mtanzania... Yuko kwenye SIASA? Kapataje PESA?

Ni mtoto wa Mkubwa? Anawajuwa Wakubwa wa CCM au CHADEMA?

Anatembeaje JIJINI Dar Mpaka anamiliki GARI GHALI kama hilo?

Niamsheni... Hata huku USA kumiliki hilo Gari sio Mchezo, Wengi walionalo hawaliendeshi kila SIKU
 
Mkuu kwani nani kasema kwenye nchi masikini hakuna matajiri wenye pesa,tatizo ni kama gap kati ya matajiri na masikini ni kubwa,hapo ndo serikali inabanwa na wananchi wake,kwasababu sera zake ndo zenye kusababisha hiyo inequality.Thas the reality,mataifa yote duniani matatizo hayakuanza eti tu kwasababu kuna watu wenye pesa,no,don't get it twisted,ni unequality inayosababisha classes.

Kwenye nchi masikini,na hata tajiri, hakuna shida kama kuzipata kazipata kihalali,ndo uhuru na upande wa "mazuri" ya "free market"
 
Aisee....napendekeza zitumiwe na Mawaziri ....ni muhimu kwa safari za Dar/dodma/Arusha

Ha ha ha ha ha ha! Sio mawaziri tu Mkuu. Hata waheshimiwa wabunge wetu wakopeshwe. Litawasaidia sana kuwahi vikao mbali mbali majimboni kwao pamoja na kukutana na wapiga kura wao na wakati huo huo kuwahi vikao vya kamati na bodi mbali mbali jijini Dar es Salaam ambako pia ni wajumbe. Pia litawasaidia sana kutoa misaada kwa wajazito hasa wakati wa kujifungua majimboni kwao. Kwa kweli lina hadhi ya 'uheshimiwa'. V8 wapewe madiwani.
 
Hapo kwenye madiwani umeniwahi........kuongezea tu Rais na Waziri mkuu watumie chopper
 
Mkuu kwani nani kasema kwenye nchi masikini hakuna matajiri wenye pesa,tatizo ni kama gap kati ya matajiri na masikini ni kubwa,hapo ndo serikali inabanwa na wananchi wake,kwasababu sera zake ndo zenye kusababisha hiyo inequality.Thas the reality,mataifa yote duniani matatizo hayakuanza eti tu kwasababu kuna watu wenye pesa,no,don't get it twisted,ni unequality inayosababisha classes.

Kwenye nchi masikini,na hata tajiri, hakuna shida kama kuzipata kazipata kihalali,ndo uhuru na upande wa "mazuri" ya "free market"

Mbongo huyu huyu mwenye ubongo??
Na huu mustakhabali wa Chukua Chako Mapema??
........labda!
 
Mbongo huyu huyu mwenye ubongo??
Na huu mustakhabali wa Chukua Chako Mapema??
........labda!

Wanasema alikuwa kiongozi wa "Young Africans" AKA "kandambili"Nthen kwamba gari kalinunuwa kutoka kwa mtoto wa Bakhressa,so wote sijui kama wana uhusiano na chukua chako mapema AKA. Gamba?That's another topic,navyojuwa kuna watu wana pesa bongo,however wengi wali "lay low" mara baada ya ile maneno ya epa na ingine.
 
Kama anafanya biashara halali haina tatizo,,,tumwache atumie jasho lake.Lakini kama ni kinyume na hivyo tuna haki ya kuhoji.
 
Exactly! Tena chini ya utawala wa CCM na mzigo anabebeshwa masikini kwa kuongezewa bei kwenye mafuta ya taa! Inauma sana, wala sio ufahari.

Tena kwa vile wako huru na pesa zao, alafu serikali yenyewe imejaa ufisadi........yaani wanajiamlia tu wanavyotaka!
 
Bongo biashara inalipa sana tatizo wabongo wengi mkimaliza vyuo mnakimbilia kutafuta kuajiriwa ukishakuwa Bank Teller unaona ushamaliza.
Eti unakuta mtu ana degree ya Horticulture then kaajiriwa NMB eti ni Bank teller.Shame on you all.
 
Wanasema alikuwa kiongozi wa "Young Africans" AKA "kandambili"Nthen kwamba gari kalinunuwa kutoka kwa mtoto wa Bakhressa,so wote sijui kama wana uhusiano na chukua chako mapema AKA. Gamba?That's another topic,navyojuwa kuna watu wana pesa bongo,however wengi wali "lay low" mara baada ya ile maneno ya epa na ingine.

Kama kuna baadhi ya viongozi wa Yanga wa ngazi zingine walikuwa wanalalamika kutokulipwa pesa zao.......yeye ndo aibuke na faranga kwenye hiyo nyanja, tena kihalali?? Hapana NO!!

Hapo in red,
Sikatai kuwa kuna watu wenye pesa na wengine wanaweza kuwa wamezipata kiuhalali.
But, why wengi wali 'lay low' baada ya maneno ya EPA.....as per your say?
 
Bongo biashara inalipa sana tatizo wabongo wengi mkimaliza vyuo mnakimbilia kutafuta kuajiriwa ukishakuwa Bank Teller unaona ushamaliza.
Eti unakuta mtu ana degree ya Horticulture then kaajiriwa NMB eti ni Bank teller.Shame on you all.

Zikiwemo za magendo!
 
Back
Top Bottom