Kweli mzungu acha aitwe mzungu...

Kweli mzungu acha aitwe mzungu...

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
4,322
Reaction score
6,700
Kuna kitu nilikuwa nawaza jinsi hawa jamaa walivyoweza kugundua umeme na kufanya kila mashine ili ifanye kazi lazima itumie umeme,huu uwezo wenzetu wameutoa wapi?

Kibaya zaidi walivyokuja kutengeneza mfumo wa malipo kwa njia ya kielektroniki,kwamba hauna pesa,haupigi simu au kuwasiliana.

Sisi weusi tulikosea wapi?

Mwenye chochote achangie hili tuzidi kueleweshana maana hapa pia tunawasiliana kwa nguvu ya umeme na pesa.

Nachanganyikiwa kiukweli uwezo wa hawa jamaa.
 
kuna kitu nilikuwa nawaza jinsi hawa jamaa walivyoweza kugundua umeme na kufanya kila mashine ili ifanye kazi lazima itumie umeme,huu uwezo wenzetu wameutoa wapi?kibaya zaidi walivyokuja kutengeneza mfumo wa malipo kwa njia ya kielektroniki,kwamba hauna pesa,haupigi simu au kuwasiliana,...sisi weusi tulikosea wapi?mwenye chochote achangie hili tuzidi kueleweshana....maana hapa pia tunawasiliana kwa nguvu ya umeme na pesa....nachanganyikiwa kiukweli uwezo wa hawa jamaa.

Kwanza tuanzie kwenye signature yako ambayo ni "repitition is the father of learning". Hivi spelling za hilo neno la kwanza ziko sawa? Kama sio sawa basi umekosa kitu kinaitwa 'being critical for everything' au 'critical thinking' ambacho hao jamaa ndio kinawasaidia sana ingawaje sio wote.
 
Wanasema katika vitu vilivyo badilisha dunia ni 1. Umeme 2. internet.

Ninaamini bila wazungu tungeweza kugundua hivi vitu lakini ingetuchukua muda zaidi. Waarabu waligundua namba, Wagirikia waligundua demokrasia, tulikua wakwanza kugundua matumizi ya chuma.
 
kuna kitu nilikuwa nawaza jinsi hawa jamaa walivyoweza kugundua umeme na kufanya kila mashine ili ifanye kazi lazima itumie umeme,huu uwezo wenzetu wameutoa wapi?kibaya zaidi walivyokuja kutengeneza mfumo wa malipo kwa njia ya kielektroniki,kwamba hauna pesa,haupigi simu au kuwasiliana,...sisi weusi tulikosea wapi?mwenye chochote achangie hili tuzidi kueleweshana....maana hapa pia tunawasiliana kwa nguvu ya umeme na pesa....nachanganyikiwa kiukweli uwezo wa hawa jamaa.
Kabla ya kupost mada au wazo ambalo wewe unadhani ni jipya au kitu kigeni ebu fanya utafiti kwanza. Kwa jinsi nilivyokuelewa unadhani hakuna ugudunzi umefanywa na Waafrika??????? Fanyia kazi eneo hili na utashangaa mambo waliyoweza kugundua ambayo dunia inaendelea kuyatumia. Acha akili ya kujidharau
 
huku kwetu maji safi na salama bado ni tatizo kubwa.
 
Zamani kidogo, nilijaribu kutengeneza satellite receiver yangu binafsi pale home. kwakuwa nilivutiwa sana na maswala ya ubunifu electronics, kilichonikuta bwana, nilipata mikwaju ya kufa mtu, matusi na mavitu yangu yote yalichomwa moto, but now nimekuwa juu hadi wazee wakikumbuka wanaona aibu. This Is Africa.
 
Mtoa Mada, kwanza ugumu wa haya mambo inategemea na uelewa au akili ya mtu binafsi. Kama kidogo umepata nafasi ya kusoma haya mambo si magumu kama unavyodhani. Nataka nikuambie katika ugunduzi huu pia kuna watu weusi hasa wamarekani weusi ambao walihusika katika ugunduzi wa maswala ya computer na umeme, ingia google utaona kuna watu weusi ambao pia wamegundua mambo kadhaa hata katika vifaa vya kwenda mwezini
 
Zamani kidogo, nilijaribu kutengeneza satellite receiver yangu binafsi pale home. kwakuwa nilivutiwa sana na maswala ya ubunifu electronics, kilichonikuta bwana, nilipata mikwaju ya kufa mtu, matusi na mavitu yangu yote yalichomwa moto, but now nimekuwa juu hadi wazee wakikumbuka wanaona aibu. This Is Africa.
Ni kweli hii ni Afrika, wala usimlaumu msure kwake yeye alitimiza wajibu wake. Ingekuwa ulaya msure angekupeleka kwenye kituo cha TV na kuna kampuni au mtu angeweza kujitolea kwa elimu yako ili kilichoko kwenye damu yako kiendelezwe.
 
pia waligundua mlima Kilimanjaro na ziwa Victoria.... sisi tulikuwa hatuoni kabisaaa
 
Kwanza tuanzie kwenye signature yako ambayo ni "repitition is the father of learning". Hivi spelling za hilo neno la kwanza ziko sawa? Kama sio sawa basi umekosa kitu kinaitwa 'being critical for everything' au 'critical thinking' ambacho hao jamaa ndio kinawasaidia sana ingawaje sio wote.
mkuu una makengeza ama ujuaji umekuzidi?what?
 
Pasingekuepo kuingiliwa kwa waafrika na hawa wakoloni tungefika mbali sana.

Katika kipindi cha kuingiliwa Afrika na ulaya maandishi yanasema Afrika na Ulaya zilikua katika kiwango sawa japo sio sawia. "Same level but not similar "
 
mkuu una makengeza ama ujuaji umekuzidi?what?

Tatizo jingine ni kwamba baada ya kurekebisha spelling hutaki kuonekana ulikosea na kuwa mimi nimekusingizia; kwa kifupi, tatizo lako la 'ujuaji' na 'what' unataka liwe langu.
 
We ulisema umefundishwa kutoa namba tu.unataka nani aje kukufundisha kutoa herufi hebu jiongeze akili!
Au nawew ni mwanaume wa daslam
 
Aiseeee ona hata matamko ya rausi wetu utajua tu ngozi nyeusi ina kazi
 
Back
Top Bottom