Kweli mzungu acha aitwe mzungu...

Kweli mzungu acha aitwe mzungu...

Zamani kidogo, nilijaribu kutengeneza satellite receiver yangu binafsi pale home. kwakuwa nilivutiwa sana na maswala ya ubunifu electronics, kilichonikuta bwana, nilipata mikwaju ya kufa mtu, matusi na mavitu yangu yote yalichomwa moto, but now nimekuwa juu hadi wazee wakikumbuka wanaona aibu. This Is Africa.
Hapo ndipo wanapotuacha, wazee wako walitakiwa wakuendeleze kwa hcho ulichokuwa unakipenda wao wakataka usome uwe na degree full of theories waanze kujisifu, wakati degree yenyewe haina msaada wa moja kwa moja kwa jamii zaidi ya kupata mshahara mwisho wa mwezi
 
Wanasema katika vitu vilivyo badilisha dunia ni 1. Umeme 2. internet.

Ninaamini bila wazungu tungeweza kugundua hivi vitu lakini ingetuchukua muda zaidi. Waarabu waligundua namba, Wagirikia waligundua demokrasia, tulikua wakwanza kugundua matumizi ya chuma.
Pia tumekua wa kwanza duniani kufanikisa kurusha helicopter kwa photoshop...

Pia tumekua wa kwanza duniani kupandisha pikipiki kwenye basi la mwendokasi

Pia tumekua wa kwanza pia kwa mbunge wetu kuomba alama muhimu za taifa zibadilishwe ( sanamu la askari kuwekwa la diamond)
 
Hivi ni kweli kuwa sie hatufanyi ugunduzi kama wazungu ni kwa sababu hatuna akili kama walizonazo wazungu au kuna sababu nyengine tu ambayo inafanya wale wawe vile na si suala la akili??
 
yap, unakuta mtoto anakuwa katika mazingira mazuri zaidi. kiukweli huwezi kuwa mahiri kufanya jambo fulani kama hukuwa na msingi imara wa jambo hilo, na ndio mana Phd, na mastars zetu zinaishia kwenye siasa!! utaki kijana wako akasome uhandisi wa majengo, then unamchagulia akasome vi kozi vya ujasiliamali pale IMF, then anataka kuajiriwa na sio kujiajiri, serikali yetu ichukue jukumu la kuvitafuta vipaji huko mitaani kisha vipewe kipaumbele kwa msaada wa taifa.
 
Na unajua sikuhizi internet inarahisha sana, unapata magazines, jounals, wikipedia. Ni muda wako tu kama unaamua kwenda kwa mama Fatuma kujua mtaa wa pili kama baba amepata kazi au unanamua kujaza ubongo wako mwenyewe kimya ndani.

Asante kwa kujitambua.Nina project ya Kifaa cha kupambana na mbu kwa nchi za Afrika.Kuna unaweza kuwa na input yoyote karibu uchangie utajiri wako.Napatikana kwa:sanctuss16@gmail.com
 
Hapo ndipo wanapotuacha, wazee wako walitakiwa wakuendeleze kwa hcho ulichokuwa unakipenda wao wakataka usome uwe na degree full of theories waanze kujisifu, wakati degree yenyewe haina msaada wa moja kwa moja kwa jamii zaidi ya kupata mshahara mwisho wa mwezi
 
Kuna kitu nilikuwa nawaza jinsi hawa jamaa walivyoweza kugundua umeme na kufanya kila mashine ili ifanye kazi lazima itumie umeme,huu uwezo wenzetu wameutoa wapi?

Kibaya zaidi walivyokuja kutengeneza mfumo wa malipo kwa njia ya kielektroniki,kwamba hauna pesa,haupigi simu au kuwasiliana.

Sisi weusi tulikosea wapi?

Mwenye chochote achangie hili tuzidi kueleweshana maana hapa pia tunawasiliana kwa nguvu ya umeme na pesa.

Nachanganyikiwa kiukweli uwezo wa hawa jamaa.
Tuna uwezo sawa kiakili, tatizo ni maumbile na resources tu wao ni wavivu sana na resource haziwatoshi ndo maana walikua wanatumia mda mwingi kufikiria njia rahisi ya kurahisisha kazi zao na ku-maximize matumizi ya resources zao. Wakati wao wanatakiwa kula matunda na mboga zikitokea kwenye friji kwasababu hazipatikani kirahisi, sisi tulikua tunakula matunda kutoka mitini moja kwa moja na kila msimu ukiwa na aina yake ya matunda na ukihitaji mboga za majani unaenda mabondeni kuchuma zilizojiotea zenyewe. Wakati wao wanahitaji na wanafikiria vifaa vya ku-purify maji yaliyochafuliwa na shughuli zao za kiuchumi, sisi tulikua tunajinywea maji kutoka kwenye chemi chemi za asiri zilizokua kibao na mpaka sasa bado zipo baadhi zinatoa maji safi na salama. wakati sisi tumezoea kila kitu kinawezekana kwa kutumia msuri kwa mfano ukitaka kushusha bei ya sukari unaagiza bei iwe shingapi na unavielekeza vyombo vya dola visimamie hilo, wao wanaanza kujiuliza nadhalia za Demand and supply zinasema nini Tehe!!
 
Kwa vile waafrika hasa weusi tulikosa maandishi yetu wenyewe, tulishindwa kuweka kumbukumbu ya maisha na ubunifu wetu kwa ajili ya kurithisha vizazi vyetu. Hivyo ilikuwa vigumu kurithisha tamaduni zetu ili ziwe endelevu. Mzungu alipokuja na vya kwake kwenye maandishi. Tulimeza kama dodoki! Hapo ndipo tulipojimaliza, hatukutaka tena kujishughulisha bali tulisubiri tuletewe na mgeni!

tabia hiyo mpaka leo tunayo na hatutaweza kujikwamua kamwe! Tunatawaliwa kiakili na tumekubali!
 
Tatizo ni fursa tu naamini Africa kuna watoto wanazaliwa wana akili sana lakini hawapati nafasi ya kujiendeleza. Mfano Albert Einstein angezaliwa africa angeishia kua mkulima tu ila alibahatika kuzaliwa Germany na kupata nafasi ya kuendeleza kipaji chake. Huenda hata Africa walizaliwa watu wenye akili kama Einstein lakini hawakubahatika kwenda shule. Pia tukumbuke wazungu sasa hivi wapo katika golden age yao lakini hawakua hivi miaka yote. Kuna kipindi ilikua waislamu ndio wana ongoza kwa kugundua vitu mfano algebra na algorithms viligunduliwa na waislamu. kipindi hichi kinaitwa "golden age of islam" wakati huo wazungu wengi walikua hata kusoma hawajui. So hata africa inaweza kufika wakati tukawa kama wazungu walivo leo
 
Kabla ya kupost mada au wazo ambalo wewe unadhani ni jipya au kitu kigeni ebu fanya utafiti kwanza. Kwa jinsi nilivyokuelewa unadhani hakuna ugudunzi umefanywa na Waafrika??????? Fanyia kazi eneo hili na utashangaa mambo waliyoweza kugundua ambayo dunia inaendelea kuyatumia. Acha akili ya kujidharau
ndugu hapa hakuna cha unchunguzi wala nini, we sema MUAFRIKA amefanya nini na nini.
 
Zamani kidogo, nilijaribu kutengeneza satellite receiver yangu binafsi pale home. kwakuwa nilivutiwa sana na maswala ya ubunifu electronics, kilichonikuta bwana, nilipata mikwaju ya kufa mtu, matusi na mavitu yangu yote yalichomwa moto, but now nimekuwa juu hadi wazee wakikumbuka wanaona aibu. This Is Africa.
Je ubunifu wako umesaidia nn katika taifa hili na jamii inayokuzunguka
 
Mi naona hapa wanasifiwa wazungu na kupondwa waafrika,sasa hebu tuambieni na hizo jamii zengine hali ikoje?
 
Tuna uwezo sawa kiakili, tatizo ni maumbile na resources tu wao ni wavivu sana na resource haziwatoshi ndo maana walikua wanatumia mda mwingi kufikiria njia rahisi ya kurahisisha kazi zao na ku-maximize matumizi ya resources zao. Wakati wao wanatakiwa kula matunda na mboga zikitokea kwenye friji kwasababu hazipatikani kirahisi, sisi tulikua tunakula matunda kutoka mitini moja kwa moja na kila msimu ukiwa na aina yake ya matunda na ukihitaji mboga za majani unaenda mabondeni kuchuma zilizojiotea zenyewe. Wakati wao wanahitaji na wanafikiria vifaa vya ku-purify maji yaliyochafuliwa na shughuli zao za kiuchumi, sisi tulikua tunajinywea maji kutoka kwenye chemi chemi za asiri zilizokua kibao na mpaka sasa bado zipo baadhi zinatoa maji safi na salama. wakati sisi tumezoea kila kitu kinawezekana kwa kutumia msuri kwa mfano ukitaka kushusha bei ya sukari unaagiza bei iwe shingapi na unavielekeza vyombo vya dola visimamie hilo, wao wanaanza kujiuliza nadhalia za Demand and supply zinasema nini Tehe!!
Very low. Kufikiri toka lini ikawa ni uvivu mkuu???
 
Kabla ya kupost mada au wazo ambalo wewe unadhani ni jipya au kitu kigeni ebu fanya utafiti kwanza. Kwa jinsi nilivyokuelewa unadhani hakuna ugudunzi umefanywa na Waafrika??????? Fanyia kazi eneo hili na utashangaa mambo waliyoweza kugundua ambayo dunia inaendelea kuyatumia. Acha akili ya kujidharau
Mkuu umenena kweli, nachukiaga sana watu wanaojidharau. Mungu ameweka kitu chatofauti kwa kila mtu bilakujali rangi ila mzngira anayoishi mtu na vitu vinavyo mzunguka ndoo humpelekea afikilie nn cha kufanya kpya.
 
Fikiria uzito wa ndege na watu ndani lile dude lina paa juu[emoji15] [emoji15] [emoji15]

Fikiria unavyoweza kuongea na mtu yuko marekani sauti unasikia muda uleule na sikuhizi video inaonekana..[emoji15]
 
Nikiwazaga kuhusu wazungu ndo naishia tu kusema DUNIA YA MUNGU , VITU VYA MZUNGU, alaf BAADA YA MUNGU NI MZUNGU, ..hawa jamaa cjui kama wamependelewa vile..
Mkuu hapa utasema "UJINGA WAKWETU"
 
Back
Top Bottom