Nilikuuliza swali la msingi hadi sasa hujajibu,taja hayo mashirika binafsi yaliyopata faida hapa Africa ?
Then usifananishe Tanzania/Africa na France hao wako dunia nyingine
Umewahi kujiuliza kwa nini licha ya hayo mashirika(SA,KQ,WB,MS) kutoingiza faida kwa nini hizo nchi bado zina hayo mashirika na bado yanapata support ya serikali ?
Airline industry inaingiza faida nyingine indirectly ukiacha faida ya mashirika ya ndege.Mkiwa na Airline itawabidi mjenge viwanja vya kimataifa kuna ndege toka nje zitakuja zitalipa kodi,wasafiri watakaa hotelini na ni fursa ya kutangaza utalii uliopo. Mafanikio ya Ethiopian Airline ni moja ya chanzo cha mapato ya uchumi wa Ethiopia
Kuhusu hao binafsi kupata faida au hasara hainihusu. Ya serikali inanihusu maana ni kodi yangu inatumika vibaya. Na kwa hapa PW wameanza hasara baada ya ubia wao na KQ. Again, hainihusu coz ni wao na biashara zao. Cha msingi serikali iwawekee usawa wapambane.
Halafu hao Kenya Airways wenyewe hata si serikali 100%. Ndo uone majirani ni wajanja wamehedge risk zao. Busara ya wahenga kutoweka mayai yote kapu moja unahusika. Zaidi ya 70% ya KQ sio serikali!!
Hiyo habari ya airline kuwa na faida zingine ni uongo wanaotengeneza wasimamizi uchwara wa hizo govt operated commercial airlines ili waendelee kufuja. Faida ya biashara iko bottomline. Mengine tafuteni kingine kiyalete.
Btw, kujenga viwanja vingi vya ndege ni demand km ipo. Sio kisa una ndege. We jamaa bana. Marekani hawaown mandege ya serikali na wana viwanja ile mbaya. Kadhalika, tulijenga Songwe International wakati ATCL imejifia. Your argument quashed just like that.
Halafu hii habari ya kusema tusijifananishe na Ufaransa na kadhalika wanapenda sana kutumia watawala wa awamu hii.
Kuna nini? Mnaogopa nini kujipima na walioweza? Mnang'ang'ania mikakati ya waliofeli badala ya kuiga waliofaulu? Pathetic. Kisa wao wazungu ndo hawafai kuigwa? Eti mmeenda kuchukua uzoefu Rwanda. Watu hawajawahi tengeneza faida tangu waanze operations. Kweli??? AIBU!!!!!!
Jamaa, amkeni bana. Dunia haitusubiri eti tutapata faida zingine kwa serikali kufanya biashara ya ndege. Zipi? Sasa mnatafuta suluhisho la utendaji mbovu. Mkimaliza hilo mtakuja kuchelewa malipo ya supplier. Then ufisadi utatamalaki na kupeleka ndege mazishini badala ya ruti husika n.k. n.k
Mkitoka hapo mnarudi nacho serikali haifai kufanya biashara mnauza tena shirika. Do it now ndege zingali mpya.
Umezungumzia Ethiopian kukukuza uchumi wa kwao. Sikatai. Tena ndo airline pekee kubwa Africa ina faida. Sasa kilichowanyima kwenda kujifunza kwao mkaenda kwa failures Rwandair ni nini? Inarudi kulekule, ATCL wameshindwa kabla hawajaanza.
Nipo hapa nakusubiri belo.