Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa

Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa

Hata bila kupewa hongo, hivi ukiambiwa uende Mwanza kutoka Dsm ambayo ni safari ya saa nzima hadi saa nzima na nusu kulingana na aina ya ndege halafu ukaambiwa uchague kati ya jet ya Fast Jet, pangaboi kubwa ya Precision Air au pangaboi ya kubanana ya Air Tanzania hata kabla hujaangalia bei ya tiketi utachagua ipi hapo iwapo wewe ni mzoefu wa safari za ndege?
Ni wazi chaguo la mwisho litakuwa Air Tanzania. Nani akubali kusafiri kwa mateso na kujiminya bila raha yoyote kwa saa nzima na nusu eti kisa uzalendo?

Heeeeeeeeh...Watanzania tuko wa aina nyingi kwa mawazo na maoni.......si rahisi kumshinda Mtanzania kwa kejeli.....
 
Nilichokiandika ni kwa uzoefu wangu. Nimeshasafiri sana na rwandair nimefanya kazi Rwanda kwa vipindi tofauti tofauti. So I personally know how the said airline helps to promote/advertise the country internationally. Sisi kila siku tunaimba kubana matumizi tu. Ni lazima tujitangaze kimataifa, tutangaze fursa na vivutio vinavyopatikana nchini kwetu. Mashirika ya ndege yanayomilikiwa na serikali si jambo la ajabu sana kupata hasara lakini yana sustain. Tembea ujionee ndugu.
Sina haja kukwambia nimetembea wapi na nakuhakikishia hakuna ulazima hayo mashirika yamilikiwe na kuendeshwa na serikali.

Ona mkenge wa kwanza wa hapa kwetu serikali wakaamua kununua taslimu. Ndo ujue serikali haijupaswa kudili na hayo mambo maana wao faida sio ishu. Wanateketeza tu pesa yetu.

Kujitangaza utalii sio lazima ndege. Idadi ya watalii huku imeendelea kukua na shirika halipo. Unataka uthibitisho gani zaidi? Kenya wanalo shirika na idadi imepungua Mombasa hadi wakaanza kulalamika Znz wanawachukulia watalii.

Kama haitoshi, wanalo shirika (japo hawamiliki %100) na bado watalii wanaspend zaidi wakiwa huku kuliko wakiwa huko kwao wenye ndege. Narudia tena. Hoja ya kusema shirika likimilikiwa na serikali kuna faida za ziada km utalii si ya maana sana.
 
Ni kweli uamuzi wa kuweka route moja ya usiku sio mzuri. Lakini isingekua busara kila mara CEO anapofanya uamuzi mbaya atumbuliwe. Apewe mwaka mzima wa fedha au hata miaka miwili...akikosea ajisahihishe. Baada ya kipindi hicho tuangalie financial statement ya ATCL..kama ametengeneza faida basi aendelee...kama katengeneza hasara na maelezo yake hayajitoshelezi...basi atumbuliwe.
 
Tunaenda mbele na kurudi nyuma ukiulizwa maswali unaruka ruka,unatoa ushauri bila kutoa mifano.Nafanya kazi na watu wa airline ET sio wala rushwa au wapiga kelele kama sisi hapa ni wazalendo ndio sababu kubwa ya wao kufanikiwa.Faida ya kuwa na airline company sio lazima iwe directly nimekueleza pamoja na hizo airline kupata hasara lakini hakuna nchi inayofikiria kufuta shirika lake hao KQ pamoja na kubinafsisha still wanaingiza hasara mwaka wa 4 mfululizo

Kulinganisha France na Tanzania ni,sawa na na kulinganisha Taifa Stars na Timu ya Taifa ya France unalinganisha nchi zinazotofautiana kila kitu
Hakuna ambacho sijakujibu. Hao ET kuwa wanyoofu haiondoi ukweli kuwa Ethiopia inaongozwa kiimla zaidi. Na pengine ndio maana wanafanikiwa na hilo shirika.

Umesema hakuna nchi inafikiria kuachia shirika lake. Unatania labda. Uliza mswisi akuambie kwanini kauza lake Lufthansa.

Mimi nasisitiza tuna nafasi ya kuwaiga waliofanikiwa. Na hakuna ubaya Taifa stars kuiga ufaransa kwenye mafanikio. Kanuni za kufanikiw ni zilezile kwa tajiri na maskini. Wenye kuwahi kuzifuata ndio wanaofanikiwa mapema
 
Back
Top Bottom