Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa

Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa

Miradi ya serikali huwa haina ufanisi na ushindani. Ipo ipo tu.
Serikali yetu ina vyanzo vingi sana ya kujipatia mapato lkn haijali. Wao wanaona njia nzuri za kupata mapato ni kupitia PAYEE, makosa ya barabarani, Tax & Vat.
Ww angalia TTCL liko ovyooooo mpaka huruma, na miradi mingine yaan bora liende.
Tanzania kuendelea ni ndoto sbb viongozi wetu ni wanafiki halafu wanajali matumbo yao.

Tumeambiwa hii nchi itakuwa ya viwanda, halafu baadae wanasema kazi ya serikali ni sound tu ili wawekezaji waje.
NI NCHI GANI IMEWEZA KUWA NCHI YA VIWANDA KWA KUWATEGEMEA WAWEKEZAJI?

SERIKALI INABID IJITAFAKALI UPYA KUHUSU MIRADI YAKE.
 
Mimi nimeingia kwenye site yao na nimeona kuwa kwa sasa wapo na safari moja ambapo ndege inaondoka dar 17:00 na kuwasili Mwanza 18:45, kuanzia mwezi December watakuwa na flight itayotoka Dar saa 06:00 na kuwasili Mwanza 07:45, kwa maoni yangu sio mbaya kwa kuanzia na huku ukipima upepo wa biashara, hata nauli yao ya 199,000 sio mbaya sana kwa kuazia ukichukulia kuwa tunaenda katika pick season. Ninachowashauri 1. wawe na maamuzi ya haraka wanapoamua jambo (waziri husika awape nafasi board wafanye kazi) bila ya maamuzi ya haraka kwenye airline business siku zote utaachwa nyuma. 2. waboreshe sana website. i.e najua archive yao ipo very rich kwenye information ya mambo ya ndege na culture za miji tofauti lakini wajue biashara kwanza na waache kuweka kila kitu pale front page. 3. kuna root zingine ni hot cake kwa mfano mwanza/Bukoba, ama Znz/Pemba maeneo haya kijiografia yametengwa na mikondo ya maji na hivyo kuwa vigumu kufikika kwa meli waende huko haraka. 4. Waingie kwenye biashara ya kuruhusu kununua tiketi kwa njia ya mitandao ya simu haraka sana.
 
Naomba JPM anipe kazi ya kuwapiga Risasi hadi kufa watu kama ATCL, naamini tukianza kupiga watu Risasi kwa Uzembe na kutokufikiri vizuri basi akili zitatukaa sawa.
 
Kwenye domestic flights, routes za Dar - Mwanza ndizo zenye wateja wengi na zinalipa. Mashirika ya Precion air na Fast jet kila moja lina route tatu za Dar- MZA yaani saa 2 asubuhi, saa 6 mchana na saa 2 usiku. Trip za asubuhi na saa 6 ndizo hot cakes zenye wateja wengi na bei yake ni kubwa. Trip ya usiku siyo hot, kwa maana mkazi wa Mwanza kufika Dar usiku kama hana makazi Dar ni usumbufu na gharama zaidi ya usafiri toka airport kwenda kusaka hotel za kulala.

Cha ajabu tangia ATCL waanze kutoa huduma hii wao wameamua kufanya route moja tu ya usiku, tena usiku wa saa 3 na nusu, yaani kufika Dar saa 5 usiku. Zile route nzuri wamewaachia washindani wao. Bei za ATCL ni nusu ya bei za washindani wao, hivyo wakaona waachie hizo route maana washindani wao hawangepata wateja au ingebidi nao wateremshe bei.

Sasa kwa nini wasitumbuliwe?

Cc: Rais wa JMT
Waziri Makame Mbarawa
 
Mkuu kusema kweli hata mimi siwaelewi ATCL kwa hii trip ya Mwanza. Ndege moja kwa siku kwenda Mwanza ni shida kubwa. Kama wanapeleka ndege moja tu Mwanza kwa siku ina maana kuna muda mwingi ndege zitakuwa zimepaki ardhini. Biashara ya ndege inataka muda mwingi ndege iwe angani badala ya nchi kavu. Ningekuwa mimi Mwanza ningepeleka ndege hata mara nne kwa siku. Ndege mbili kwa trip za humu nchini zinaweza kufanya kazi kubwa tu kama zitapangiliwa vizuri.
Ndege mbili aziwezi kutimiza matakwa unayoyataka ukiacha root ya mwanza, root ya Arusha ndege utua katika uwanja mdogo wa Arusha Airport ambapo Precision na Airtanzania utua na uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA hizi root zaina abiria wengi sana sasa ndege ni chombo ikiwa mbili azitoshi kuruka mara tatu kwa siku kuja mwanza wakati inatakiwa iende Arusha,Mtwara,Kigoma,Chato,Comoro,Dsm,Znb n.k je kwa ndege mbili watazigawanyaje?,usisahau delay kutokana na matengenezo,hali ya hewa n.k japo mashirika ni matatu usafiri bado ni wachangamoto sana nilichogundua japo nauli za Atcl niza chini precision bado ina abiria wengi hivyo bado tunaitaji kuwa na ndege nyingi za ndani na zikiwa nyingi choice inakuwa kubwa na mtu unamua usafirije,kumbuka customer care ni kitu kizuri sana hivyo ATCL wajipange kwa hilo.
 
20161120_094021.jpg


Jana saa 4 asubuhi, mbili ziko idle uwanjani.

Ndege muda mwingi zimepaki pale JNIA utafikiri ni za maonyesho...

Cha kushangaza hawaruhusu mtu ukate ticket kwenye website yao hadi ujisajili na Ku log in, utadhani wateja ni wajomba zao
 
Muda huu bila shaka unarudi na 'panga boy' yako kutoka kuwanga..
Vitengo vingi huko serikalini na mashirika ya umma wamepewa watu wasio na taaluma pia uelewa wa kawaida. Unakutana na mtumishi tena daraja la juu ila maamuzi yake anazidiwa na darasa la saba mwenye uelewa wa mambo.

Inanikumbusha jamaa alipata scholarship nje ya nchi ,alipokwenda kufuatilia visa ubalozi husika akaambiwa aende wizara ya elimu kwa mtu mmoja (akapewa hadi jina) agonge mhuri makaratasi yake ili visa yake iweze kushughulikiwa. Cha ajabu amefika wizarani yule mhusika anamwambia deadline ya kugonga mihuri ya namna hiyo imeshapita na hawezi kumgongea. Sasa mtu katafuta scholarship mwenyewe, serikali ya Tanzania haingii gharama yoyote juu ya masomo yake unakataa kupiga mhuri tu mtu akapate visa?

MAGUFULI endelea kutumbua bila huruma.
Siyo kweli kwamba hawana ujuzi wala taaluma. Tatizo ni rushwa. Mtu wala huhitaji taaluma ya anaerotical engineering kutambua kuwa routes za saa 2 asubuhi, saa 4 na saa 6 ndizo hot routes za watu wengi kwa ajili ya kwenda kufanya kazi. Kwamba routes za usiku ni kwa ajili ya watu wanaorudi makwao kulala. Sasa ATCL inapoamua kuwa shirika la kusafirisha tu watu wanaoenda kulala na kuacha wanaoenda kufanya kazi, tuwaeleweje kama si kuhujumu shirika?
 
Siyo kweli kwamba hawana ujuzi wala taaluma. Tatizo ni rushwa. Mtu wala huhitaji taaluma yaanaerotical engineering kutambua kuwa za saa 2 asubuhi, saa 4 na saa 6 ndizo hot routes za watu wengi kwa ajili ya kwenda kufanya kazi. Kwamba routes za usiku ni kwa ajili ya watu wanaorudi makwao kulala.


Kwa Mwanza route ya saa 12 asubuhi kutoka DSM ni HOT pia
 
Usiku ni Tulivu hakuna Upepo Kwahiyo Panga Boy zinaenda Vizuri
 
Nitoke nje ya mada kidogo; hivi ni kwanini route ya Dar - Kilimanjaro ambayo ni umbali mfupi ni ghali zaidi ya Dar - Mwanza ambayo ni ndefu? Naombeni kujuzwa wadau.
Kwa sababu gharama za ndege kurusha ndege kutok point A mpaka point B hazitegemei umbali tu. Kuna factors nyingine nyingi amabzo wanaangalia. Kwa kifupi wanachukua total costs over expenses in that particular route.
 
Aise.Mbeya Kasuku anaenda mara mbili kwa siku.Asubuhi na jioni.Katikati kwenye saa 6 hakuna ndege.ATCL ombeni route hapo.Mbeya ndege isipofika asubuhi,jioni watu wanagombania ndege hadi abiria wanaachwa.Come on ATCL!
 
Ndege muda mwingi zimepaki pale JNIA utafikiri ni za maonyesho...

Cha kushangaza hawaruhusu mtu ukate ticket kwenye website yao hadi ujisajili na Ku log in, utadhani wateja ni wajomba zao
Hata na hivyo ni za maonyesho. Ya nini ndege wakati madawa hakuna?
 
Mimi nimejaribu kuwaza zaidi na zaidi...
"Huenda ndege za Bangaboi za ATCL zina kasoro hizi:
1/Hazina uwezo wa kusafiri umbali mrefu mara nyingi kwa siku, hivyo inatakiwa safari moja tu kwenda Mwanza, halafu zipaki na kupumzika ili injine zake zipoe.

2/Zinapata shida sana kusafiri mchana, kwa sababu mchana huwa kuna Mwanga na Jua, zikiwa angani zinaweza kupata hitilafu!

3/Wahusika wanaogopa kuzichakaza mapema ikiwa zitapigishwa kazi nzito hivyo kumpa hasira Mheshimiwa rais ambaye ambaye amezinunua kwa gharama kubwa sana!"

Hayo ni mawazo yangu tu nje ya Box.
 
Magufuli akitumbua viongozi kama hao wafuasi wa Chadema wanalalamika.
Chadema, wazalendo wote na walio na mapenzi mema na taifa hawalalamikii kutumbua waovu, wazembe au wabadhirifu. Tunasema kununua ndege ilikua ni kosa.

Kipaumbele cha awamu hii tangu mwanzo wanasema ni kumhudumia mnyonge. Ndege haihusu wanyonge. Madawa na madawati ndio kumuhudumia mnyonge.

Kwa sasa tunasema hilo shirika ni la kufuta kabisa. Serikali haina haja kufanya biashara ya ndege. Ni anasa tupu. Waweke mazingira sawa kwa sekta binafsi wapambane.

Alipokua precision mwenyewe walisema kaua ATCL ili afanye kazi. Sasa kuna fastjet wasifiaji wanadai wameshirikiana precision kuhonga mameneja ili ATCL isishindane. Watu wana vituko balaa. Kwanini Fastjet walivyokuja precision hawajafa? Pamoja na wana matatizo lukuki.

Kununua ndege tena taslimu ilikua ni KOSA kubwa la kimkakati na litaigharimu hii awamu mpaka siku warudi kwa wanyonge kukiri kosa, kusahihisha na kuanza kutufanyia watu kazi tuliyowatuma na sio haya MAIGIZO.
 
Hahaha!! Ngoja nijaribu kuwatetea ATCL nione kama italeta maana;
1. Ndege za ATCL hazidaiwi zimelipiwa cash hiyo ni kutokana na Mkuu wa nchi, hivyo nadhan wao wanaona ni sawa tu hata wakipata faida jiti kwa siku inakuwa poa tu.

2. Mkuu wa nchi yeye aliamini kuwa shirika lina tatizo moja tu ukosefu wa ndege hivyo akanunua na hakujua nini hasa niliuwa shirika hilo kwa kuanzia. Hali hii inawafanya hata wafanyakazi wa ATCL waone jukumu lao kubwa ni kuhakikisha uwepo wa ndege na ssio kutengeneza faida.

3. Mkuu wa nchi alishatangaza kuwa serikali yake tajiri imesha order ndege nyingine tatu kama sio nne. Hii inapelekea shirika kutokuwa na changamoto zozote zile kwan vyanzo vya hela ni serikali na sio mtaji waliopewa wa ndege mbili uwafanye waweze kununua ndege nyingine, hivyo basi faida hata ya shs 100 ni kubwa sana kwa shirika kwan wao wanatakiwa tuhakikisha ndege zipo

4. Jingine wao kama wafanyakazi wa shirika wako kwwenye payroll wa serikali hivyo hata wasipotengeneza faida mishahara yao ipo pale pale

5. Pia wakifanya safari nyingi kama mashirika mengine na wakitumia utaratibu wa kukata tiketi kama mashirika mengine halafu wakaja na faida ya milion kadhaa then mkuu yeye akaakwa uzoefu wake akahesabu idadi ya viti mara trip mara mwezi akiamini kila safani ndege inakuwa imejaa huon bado watatumbuliwa? Ndio maana wameweka utaratibu wa log in kuepusha kutumbuliwa na mkanganyiko kama huu

Kwa maana hiyo itakuwa rahisi sana kwa sisi kuwalaumu wafanyakazi wa shirika wakati hatujui lengo la kutoka kwa Mkuu wa nchi ni lipi juu ya shirika, kuna mkakanganyiko flani ukiangalia kiundani. Ni sawa na kukaa hapa na kumlaumu Mkuu wa mkoa wa dar na Arusha wakati wao wanatekeleza tu walio angizwa.
Bonge la satire na linaelimisha. Nimependa ulivyokonekti na wakuu wa mikoa 'vijana'
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Kwenye domestic flights, routes za Dar - Mwanza ndizo zenye wateja wengi na zinalipa. Mashirika ya Precion air na Fast jet kila moja lina route tatu za Dar- MZA yaani saa 2 asubuhi, saa 6 mchana na saa 2 usiku. Trip za asubuhi na saa 6 ndizo hot cakes zenye wateja wengi na bei yake ni kubwa. Trip ya usiku siyo hot, kwa maana mkazi wa Mwanza kufika Dar usiku kama hana makazi Dar ni usumbufu na gharama zaidi ya usafiri toka airport kwenda kusaka hotel za kulala.

Cha ajabu tangia ATCL waanze kutoa huduma hii wao wameamua kufanya route moja tu ya usiku, tena usiku wa saa 3 na nusu, yaani kufika Dar saa 5 usiku. Zile route nzuri wamewaachia washindani wao. Bei za ATCL ni nusu ya bei za washindani wao, hivyo wakaona waachie hizo route maana washindani wao hawangepata wateja au ingebidi nao wateremshe bei.

Sasa kwa nini wasitumbuliwe?
Hujuma za wazi kabisa, hapo kwenye ukataji wa TIKETI ndo tatizo linapoanzia kwa nini isiwe open online na siyo mfumo huo walio weka wa login......
 
Back
Top Bottom