Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa

Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa

ATCL bei yao ni nusu ya bei ya hayo mashirika mengine. Kwa mfano nauli ya ATCL Mwanz to Dar ni shs 160,000/ wakati nauli hiyo ni takribani shs 330,000/ kwa mashirika hayo mengine.
Sasa kwanini nauli hayo mashirika mengine nauli ipo 330,000/=bado watu wanalipa nauli nakupanda?ATCL waboreshe Customer Care hicho ndicho watu wanangalia sana wanapochagua huduma fulani hili wakipata hiyo huduma waweze kuridhika.
 
Mimi nimejaribu kuwaza zaidi na zaidi...
"Huenda ndege za Bangaboi za ATCL zina kasoro hizi:
1/Hazina uwezo wa kusafiri umbali mrefu mara nyingi kwa siku, hivyo inatakiwa safari moja tu kwenda Mwanza, halafu zipaki na kupumzika ili injine zake zipoe.

2/Zinapata shida sana kusafiri mchana, kwa sababu mchana huwa kuna Mwanga na Jua, zikiwa angani zinaweza kupata hitilafu!

3/Wahusika wanaogopa kuzichakaza mapema ikiwa zitapigishwa kazi nzito hivyo kumpa hasira Mheshimiwa rais ambaye ambaye amezinunua kwa gharama kubwa sana!"

Hayo ni mawazo yangu tu nje ya Box.
Biashara ya ndege sio kufanya route nyingi bali ni idadi ya abiria unaowabeba,kabla hawajaanza lazima uangalie challenge zilizopo kwenye hiyo route
 
Sasa kwanini nauli hayo mashirika mengine nauli ipo 330,000/=bado watu wanalipa nauli nakupanda?ATCL waboreshe Customer Care hicho ndicho watu wanangalia sana wanapochagua huduma fulani hili wakipata hiyo huduma waweze kuridhika.
Tatizo kubwa la ATCL ni poor business planning,poor marketing strategy & poor customer care.Shirika lilipaswa kutangaza nafasi za kazi waajiri staff wote waanze upya
 
Tatizo kubwa la ATCL ni poor business planning,poor marketing strategy & poor customer care.Shirika lilipaswa kutangaza nafasi za kazi waajiri staff wote waanze upya
I beg to differ. Tatizo la ATCL ni hili. Serikali haipaswi kufanya biashara ya ndege. Tayari tuna private wanajitahidi. Serikali wawawekee mazingira ya kushindana kwa usawa.

Hao ATCL wanapaswa kufutwa hizo ndege wauziwe Fastjet au precision. Then kama ni lazima serikali kufanya biashara hiyo, wawekeze fastjet au precision na kuwakuza kimtaji.

Hayo mengine ni sawa na kutafuta tope na kujichafua kisa una maji. Then baada ya hapo unagundua hakuna sabuni kikopo cha kuchotea na maji yenyewe yalikua ya kunywa. Matatizo ya kulazimisha!!!!!!!
 
Chadema, wazalendo wote na walio na mapenzi mema na taifa hawalalamikii kutumbua waovu, wazembe au wabadhirifu. Tunasema kununua ndege ilikua ni kosa.

Kipaumbele cha awamu hii tangu mwanzo wanasema ni kumhudumia mnyonge. Ndege haihusu wanyonge. Madawa na madawati ndio kumuhudumia mnyonge.

Kwa sasa tunasema hilo shirika ni la kufuta kabisa. Serikali haina haja kufanya biashara ya ndege. Ni anasa tupu. Waweke mazingira sawa kwa sekta binafsi wapambane.

Alipokua precision mwenyewe walisema kaua ATCL ili afanye kazi. Sasa kuna fastjet wasifiaji wanadai wameshirikiana precision kuhonga mameneja ili ATCL isishindane. Watu wana vituko balaa. Kwanini Fastjet walivyokuja precision hawajafa? Pamoja na wana matatizo lukuki.

Kununua ndege tena taslimu ilikua ni KOSA kubwa la kimkakati na litaigharimu hii awamu mpaka siku warudi kwa wanyonge kukiri kosa, kusahihisha na kuanza kutufanyia watu kazi tuliyowatuma na sio haya MAIGIZO.
Vipi mkuu uliishia darasa la 5 shule?
 
Mimi nimeingia kwenye site yao na nimeona kuwa kwa sasa wapo na safari moja ambapo ndege inaondoka dar 17:00 na kuwasili Mwanza 18:45, kuanzia mwezi December watakuwa na flight itayotoka Dar saa 06:00 na kuwasili Mwanza 07:45, kwa maoni yangu sio mbaya kwa kuanzia na huku ukipima upepo wa biashara, hata nauli yao ya 199,000 sio mbaya sana kwa kuazia ukichukulia kuwa tunaenda katika pick season. Ninachowashauri 1. wawe na maamuzi ya haraka wanapoamua jambo (waziri husika awape nafasi board wafanye kazi) bila ya maamuzi ya haraka kwenye airline business siku zote utaachwa nyuma. 2. waboreshe sana website. i.e najua archive yao ipo very rich kwenye information ya mambo ya ndege na culture za miji tofauti lakini wajue biashara kwanza na waache kuweka kila kitu pale front page. 3. kuna root zingine ni hot cake kwa mfano mwanza/Bukoba, ama Znz/Pemba maeneo haya kijiografia yametengwa na mikondo ya maji na hivyo kuwa vigumu kufikika kwa meli waende huko haraka. 4. Waingie kwenye biashara ya kuruhusu kununua tiketi kwa njia ya mitandao ya simu haraka sana.
Good, ushauri mzuri.
 
Waanzishe pia route ya Mwanza TO ARUSHA kupitia KWA UHURU KENYATA INALIPA kuliko ya Mwanza straight to ARUSHA.
 
Labda uongozi wa ATCL wanapewa mgao na Precision na Fast jet kuwa wasipange ratiba saa 2 na saa 6 .
Kitulo kuna la ziada linatakiwa kufanywa hapo, ukidhani kutumbua ndio solution pekee utatumbua mpaka itafika mahali utajitumbua mwenyewe
Kwenye biashara yenye ushindani kama hiyo unatakiwa uwe mbunifu zaidi na hasa Kwenye matangazo na kuboresha maslahi ya wafanyakazi
Ukiangalia historia ya makosa ya watendaji ktk nchi hii, mengi yanaepukika. Hata kama ni mtu ambaye hukusomea mambo ya bussiness, huwezi kuwa mjinga ukaweka ndege yako kuwapisha wenzako, wakati kuna opportunity ya kushindana nao. Hata mmiliki wa daladala anafahamu hayo.

Tatizo wanatumbuliwa bila kushitakiwa. Hawa wanasingizia ignorance lakini kumbe wanakula pesa za mashirika shindani. Wamejifunza toka Precision na vituko vya Mramba. Zuia ATCL ili ndege zao zifaidi. Hata kule MWanza meli za ziwa Victoria sasa hivi zote ziko nje ya service na sababu kubwa ni sabotage ambayo hata rais alishaizungumzia. Hawa wanaojiita wawekezaji binafsi ni watu wanaotakiwa kutiwa adabu na tusipojiangalia, sabotage itahatarisha hata usalama wetu. Si uliona hata mashine za Muhimbili?
 
I beg to differ. Tatizo la ATCL ni hili. Serikali haipaswi kufanya biashara ya ndege. Tayari tuna private wanajitahidi. Serikali wawawekee mazingira ya kushindana kwa usawa.

Hao ATCL wanapaswa kufutwa hizo ndege wauziwe Fastjet au precision. Then kama ni lazima serikali kufanya biashara hiyo, wawekeze fastjet au precision na kuwakuza kimtaji.

Hayo mengine ni sawa na kutafuta tope na kujichafua kisa una maji. Then baada ya hapo unagundua hakuna sabuni kikopo cha kuchotea na maji yenyewe yalikua ya kunywa. Matatizo ya kulazimisha!!!!!!!
Kwanza unatakiwa ufahamu faida za nchi kuwa na Airline company yake,

Fastjet hawajawahi kupata faida tangu waanze biashara hapa Tanzania halafu unasema kwamba serikali iwekeze huko,baada ya ATCL kufufuliwa ndio kumewazindua Fastjet wakafanya redundancy na kuondoa zile ndege kubwa
 
Watanzania hatuipendi nchi yetu ila tunavithamini sana vyama vyetu vya siasa na kuvithamini vya wenzetu vilivyotengenezwa kwa jasho lao. Sie ni wavivu wa kutumia jasho kupendezesha vyetu ila vikitengezwa kwa majirani tunatamani na kubaki tunalaumiana wenyewe kumbe sote tabia ni moja ..sote tuna uvivu wa kupigiwa mfano
 
Back
Top Bottom