Ngongo asante kwa maelezo ila hebu subiri kidogo nikusumbue maana mie siyo mwenyeji tena Arusha.
Nakumbuka kulikuwa na Waalimu wawili wakali sana wa Kwaya KKKT hapo Arusha. Mmoja alikuwa anasemekana ni mtu aliyesomea Music kwelikweli na alikuwa na kichuma fulani cha kutune sauti wakati anaimbisha. Nimekisahau hicho chuma ila kipo hata kwenye Physics somo la SOUND. Huyu jamaa kama sikosei kwaya yao ilishinda kwenye mashindao ya Kwaya za Arusha mwaka 1988 kama sikosei yaliyofanyikia TENGERU huku watu wakiwatakia heri maana huko Dar, kulikuwa na Mwalimu Mbajo aliyekuwa akiogopwa sana kwa ufundi na utundu wake kwenye kwaya. Huyu Mwalimu alikuwa au wa Kijenge au Tengeru, sina uhakika kwa sasa maana miaka mingi.
Pia alikuwepo mwingine mwenye Madevu aliyekuwa Mwalimu wa kwaya ya kanisa kuu kama sikosei (kubwa lililokupo mjini). Nilikuwa nawapenda sana na kwaya yao hawa jamaa ila nilikuwa nasita kwenda kanisani hapo kusali kwani ukifika muda wa kutoa sadaka, ndiyo utagundua jinsi ulivyo masikini. Mie na hela yangu ya uanafunzi, nikaamua kukimbilia kanisa la Mzee Mtangoo (@Stephen Mtangoo, huyu ni Babu yako? Nakumbuka ile story ya kuku akisema "kamata nambaaa") na Mzee yule wa Kigogo alivyoniona tu akanifuata na kuongea na mimi na akasema ingawa mie ni Moravian na hapo Arusha hakuna Moravian, basi ananikaribisha sana kwake. Hapo nilijisikia kweli nyumbani ingawa walikuwepo matajiri pia kama Mzee Mollel sijui (Owner wa Tanalec, kampuni ya kutengeneza majiko na vifaa vya umeme) ila wengi walikuwa ni watu wa mikoa kama ya Dodoma, Singida na Iringa, masikini wenzangu.
Huyu Mwalimu wa hii kwaya mwenye madevu kwa kweli nilikuwa nampenda kwa sababu nyimbo zake zilikuwa zimetulia sana na Classic. kuna Kaseti walirekodi miaka hiyo ya 80 mwishoni kabisa na nilisikia tu baadhi ya nyimbo zake walipokuja Arusha Tech kuimba ila bahati mbaya sikubahatika kununua kaseti zao. Hii kwaya ya Mzee wa midevu ilikuwa inaitwaje? Ukisinisaidia hilo jina utakuwa umenisaidia sana kuzipata nyimbo zao. Ahhh, walikuwa wanampiga gitaa kijana mmoja ameweka Curl nywele zake...... na alikuwa akipigia gitaa sijui Band gani ya muziki hapo Arusha.
Again: Asante kwa maelezo yako ambayo naona wewe u mwenyeji kweli kweli wa Arusha.
BTW: Unaweza kunitumia jina la hicho kinanda na kifaa kinachokosekana/kilichoharibika kwenye Email? Naweza kujaribu kuwaulizia jamaa zangu fulani huko labda wataweza kukitafuta au hata kukitengeneza. Siahidi lolote zaidi ya kusema ntajaribu kama itawezekana.
Mkuu Sikonge
Ilikuwepo tena kwaya nyingine kali hapo mjini kati ikijulikana zaidi kama Kwaya Kuu hii nayo ilikuwa ikikimbizana sana na kwaya Uijilisti ni kwaya kongwe haswa ilianzishwa miaka ya 70s nayo ilikuwa ikirekodi nyimbo zake nchini Kenya Mzee Moi pia alikuwa akiwaalika sana hasa kipindi cha siku yake ya kuzaliwa na sikuuu nyingine za kiserekali.Mpiga solo wa Kwaya Kuu alikuwa jamaa mmoja akiitwa Sheggy yeye alikuwa akipiga copy za muziki wa majuu hotel 77 baada Kanda Bongo Man alipokuja Tanzania alimzimikia sana akamchukua katika maonyesho yake mbali mbali nchini na nje ya nchi sijui siku hizi yuko wapi jamaa alikuwa balaa katika mpini wa solo magita yote alikuwa akiyamudu sana labda ulikuwa unamzunguzia huyu alikuwa akjipenda sana.Kuna Mwingine jina limenitoka yeye alikuwa akipiga bass gita kabla ajajiunga na kwaya kuu alikuwa akipiga Maquiz enzi za Babu Seya akitamba sana hapa nchi.Nimejaribu kukupa kahistoria kafupi ili ujue hizi kwaya zilikuwa juu kiasi gani
Mkuu wangu nitawasiliana na uongozi wa kwaya wakinipatia jina la hicho kinanda nitawasilisha mara moja.Nipatie muda kidogo nitakutumia wasifu wa kila Mwalimu wa hizi kwaya akiwemo mwalimu aka Madevu.
Natanguliza shukrani.
Ngongo,
Sasa nina uhakika kuwa ilikuwa KWAYA KUU. Walikuwa na wimbo wao mmoja hadi leo naukumbuka maneno kadhaa ingawa nilisikia mara moja tu. "Njooni tumwimbie bwana......" ambao waliimba kwenye nyimbo zao za miaka ya 80 mwishoni. Huyu Mpiga gitaa atakuwa ni huyo Sheggy kijana mmoja anayejipenda sana na kweli alikuwa akipiga solo vizuri sana. Pia Mpiga BASS nilikuwa nimemsahau, ndiyo alikuwa mpiga Bass wa kwanza ambaye nilimuona akipiga Bass kama Professional wote duniani, yaani anapiga kwa kutumia vidole vitatu vya katikati vikiwa vyote vimeelekewa chini. Nilisimama na kuwa namshangaa upigaje wake huo wa ajabu huko Tengeru kwenye mashindao.
Mwaka huo Kwaya Kuu hawakushiriki mashindano, nafikiri ili kuwaachia kwaya nyingine wawakilishe Kanisa. Mwalimu wa hii Kwaya ndiyo alikuwa huyo jamaa mwenye Madevu. Tulikuwa na uhusiano mzuri sana na Kwaya Kuu na hasa ukichukulia kwa miaka nikiwa hapo, Mwenyekiti wa UKWATA Mkoa wa Arusha walikuwa vijana wa TCA. Pia hii ilifanya hata Chuo pia kikawa karibu sana na Askofu Alpha Mohamed na gari lake la Alpha Romeo 🙂
Basi ntamuagiza Mdogo wangu akija hapo Arusha mjini, anitafutie hiyo kaseti ya hii Kwaya Kuu.
Siku hizi wamebaki Wakata viuno na Ndombolo zao majukwaani. Anyway, wakati ukuta, ukipigana nao..... Itafika muda watu watawakumbuka hata Wapiga ndombolo Makanisani na kuwasifu na kusema, hawa wa siku hizi (mwaka sijui 2050) ndiyo wabovu sana heri yao........
Nakusubiri kwenye kesi ya Kinanda na habari zaidi.
Naburudika sasa tayari: Kwaya kuu Arusha - YouTube
Hivi ule wimbo wa upendo...uliimbwa na kwaya gani? Nijaponena kwa lugha.......za wanadamu na malaika....
Kama sinao upendooo..mimi si kitu kabisa.
Zipo nyingin mimi ninazo album zao zaidi ya 3 audiona VidepHizo nyimbo waweza kuzipata kwenye youtube...! Sina uhakika kuhusu CD/DVD zake kama bado zipo madukani
Vijana KKKT Mabibo ExternalHivi ule wimbo wa upendo...uliimbwa na kwaya gani? Nijaponena kwa lugha.......za wanadamu na malaika....
Kama sinao upendooo..mimi si kitu kabisa.
Hivi ule wimbo wa upendo...uliimbwa na kwaya gani? Nijaponena kwa lugha.......za wanadamu na malaika....
Kama sinao upendooo..mimi si kitu kabisa.
Mkuu Sikonge
Ilikuwepo tena kwaya nyingine kali hapo mjini kati ikijulikana zaidi kama Kwaya Kuu hii nayo ilikuwa ikikimbizana sana na kwaya Uijilisti ni kwaya kongwe haswa ilianzishwa miaka ya 70s nayo ilikuwa ikirekodi nyimbo zake nchini Kenya Mzee Moi pia alikuwa akiwaalika sana hasa kipindi cha siku yake ya kuzaliwa na sikuuu nyingine za kiserekali.Mpiga solo wa Kwaya Kuu alikuwa jamaa mmoja akiitwa Sheggy yeye alikuwa akipiga copy za muziki wa majuu hotel 77 baada Kanda Bongo Man alipokuja Tanzania alimzimikia sana akamchukua katika maonyesho yake mbali mbali nchini na nje ya nchi sijui siku hizi yuko wapi jamaa alikuwa balaa katika mpini wa solo magita yote alikuwa akiyamudu sana labda ulikuwa unamzunguzia huyu alikuwa akjipenda sana.Kuna Mwingine jina limenitoka yeye alikuwa akipiga bass gita kabla ajajiunga na kwaya kuu alikuwa akipiga Maquiz enzi za Babu Seya akitamba sana hapa nchi.Nimejaribu kukupa kahistoria kafupi ili ujue hizi kwaya zilikuwa juu kiasi gani
Natanguliza shukrani.
Hizi ndizo nyimbo/muziki bora wa Injili nilipata kusikiliza
************************************
1. Katika Viumbe Vyote
2. Mmoja wa Wanasheria
3. Mtu Ajaribiwapo
4. Mtu Mkubwa Mmoja
5. Neno Alikuwa kwa Mungu
6. Nyumba Juu ya Mwamba
7. Samsoni Mnadhiri
8. Twasoma Mwezi wa Sita
9. Ufunuo wake Yohana
10. Wakati ule wa Nuhu
************************************
Hizi ndizo nyimbo/muziki bora wa Injili nilipata kusikiliza
************************************
1. Katika Viumbe Vyote
2. Mmoja wa Wanasheria
3. Mtu Ajaribiwapo
4. Mtu Mkubwa Mmoja
5. Neno Alikuwa kwa Mungu
6. Nyumba Juu ya Mwamba
7. Samsoni Mnadhiri
8. Twasoma Mwezi wa Sita
9. Ufunuo wake Yohana
10. Wakati ule wa Nuhu
************************************
Hivi ule wimbo wa upendo...uliimbwa na kwaya gani? Nijaponena kwa lugha.......za wanadamu na malaika....
Kama sinao upendooo..mimi si kitu kabisa.
Nikiwa mjini Morogoro au Dodoma, ni wapi naweza kupata CD/DVD ya kwaya ya Vijana Arusha yenye wimbo wa 'Kila mtu atauchukua mzigo wake'?.
Kuna ule wimbo walikuwa wanaimba ''Mungu katuumba kwa mfano wake katutofausisha na vingine,katutofausisha na wanyamaa wasio na akili.................
Huu wimbo title yake ni ipi?
Ntapatia wapi kanda zao au cds za hizo nyimbo za zamani wakuu? ?
sasa hivi wamebakia wakina Rose Muhando na mauno yao, hivi umeona video ya Rose ya wololo? huyu dada ananichefua hadi basi, sijui mshauri wake ni nani huyu mwanamke, na sijui halipiti kwenye mitandao likasoma maoni ya watu akajirekebisha? achukue mfano wa Bahati, Christina shusho etc, hizo nyimbo nilizisikia nikiwa mdogo but mpaka leo nikizisikia nasuuzika roho sana sana, hazichuji kabisaa.