Kwaya ya Barabara ya 13 Ulyankulu

Kwaya ya Barabara ya 13 Ulyankulu

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
7,076
Reaction score
2,465
Hizi ndizo nyimbo/muziki bora wa Injili nilipata kusikiliza
************************************
1. Katika Viumbe Vyote
2. Mmoja wa Wanasheria
3. Mtu Ajaribiwapo
4. Mtu Mkubwa Mmoja
5. Neno Alikuwa kwa Mungu
6. Nyumba Juu ya Mwamba
7. Samsoni Mnadhiri
8. Twasoma Mwezi wa Sita
9. Ufunuo wake Yohana
10. Wakati ule wa Nuhu
************************************
 
Hii kwaya nadhani waimbaji wake watakuwa ni watu wazima sana kwa sasa, niliwahi waona kwenye kipindi kimoja cha nyimbo za injili tayari walikuwa na umri umesogea kidogo. TUNAWASHUKURU SANA KWA NYIMBO ZAO NZURI AMBAO MPAKA LEO BADO ZINAENDELEA KUTUPA MAFUNDISHO.
 
Hii kwaya nadhani waimbaji wake watakuwa ni watu wazima sana kwa sasa, niliwahi waona kwenye kipindi kimoja cha nyimbo za injili tayari walikuwa na umri umesogea kidogo. TUNAWASHUKURU SANA KWA NYIMBO ZAO NZURI AMBAO MPAKA LEO BADO ZINAENDELEA KUTUPA MAFUNDISHO.
Hii kwaya bado ipo,lakini haivumi kabisa kama zamani,walioimba hizo nyimbo nasikia wote waliisha rudi Burundi na awa waliopo walichukua ilo jina lakini wako butu sana.
 
Ntapatia wapi kanda zao au cds za hizo nyimbo za zamani wakuu? ?
 
Nyimbo nzuri! Ila ukumbuke bwana hakuwahi nena wazi wazi kuwa yeye ni mungu, na hakuna ushahidi kwamba wanafunzi wake walimuabudu
 
Kuna ule wimbo walikuwa wanaimba ''Mungu katuumba kwa mfano wake katutofausisha na vingine,katutofausisha na wanyamaa wasio na akili.................Huu wimbo title yake ni ipi?
1. Katika Viumbe Vyote
 
Utakuwa unatoka Simiyu wewe si bure. kiukweli nyimbo nzuri
 
Nyimbo nzuri! Ila ukumbuke bwana hakuwahi nena wazi wazi kuwa yeye ni mungu, na hakuna ushahidi kwamba wanafunzi wake walimuabudu

Masahihisho kidogo:-

"bwana" <> "Bwana"
"mungu" <> "Mungu"

Kwahiyo yawezekana wewe unamaanisha kitu kingine tofauti...!
 
Mpaka sasa hii ndo number moja Tanzania ikifuatiwa na Mt.Sesilia Kurasin Enzi hizo
 
Mnaweza kujikumbusha hapa:



Mie nilikuwa Mpenzi mkubwa wa Nzega Mission Choir. Pia Kwaya ya Kanisa Kuu Arusha na yule Mwalimu wao mwenye madevu, walikuwa wananimaliza kwa uimbaji wao.

Ila kwa sababu fulani fulani, hadi leo ninapenda sana na kuzitafuta nyimbo za Mwanza Town Choir. Hii wengi wanachanganya na Kwaya ya AIC, hapana. Hii nasikia ilishakufa kama Kwaya na sijui wapi naweza kuipata kanda yao nzima yenye hizo nyimbo.

Waweza kusikiliza hapa chini kuanzia wimbo wa 141-145. Kama kuna mtu anazo basi ntanunua CD au kaseti yake na kuirekodi na kumrudishia copy ya CD akitaka.

https://archive.org/details/Injili
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka kati ya mwak 1995-2000 nikiwa kijana mdogo tulikuwa tunaangalia video kwa mzee mmoja ambaye alitoka Dubai na TV zake 2 inchi 21 na maspika ya enzi hizo .

Ilikuwa kabla ya kuangalia mkanda wa siku hiyo lazima kwaya ya ulyankulyu na baadae ikaja ya Tumaini choir ya ARUSHA
 
Sasa hivi wamebakia wakina Rose Muhando na mauno yao, hivi umeona video ya Rose ya wololo? huyu dada ananichefua hadi basi, sijui mshauri wake ni nani huyu mwanamke, na sijui halipiti kwenye mitandao likasoma maoni ya watu akajirekebisha?

Achukue mfano wa Bahati, Christina shusho etc, hizo nyimbo nilizisikia nikiwa mdogo but mpaka leo nikizisikia nasuuzika roho sana sana, hazichuji kabisaa.
 
Kuna ule wimbo walikuwa wanaimba ''Mungu katuumba kwa mfano wake katutofausisha na vingine,katutofausisha na wanyamaa wasio na akili.................
Huu wimbo title yake ni ipi?

katika viumbe vyote vilivyoumbwa binadamu kaumbika kuliko vyoteee, tumepewa masikio na macho ya kuona na akili ya kujua mema mabaya....mungu katuumba kwa mfano wake..... hiyo ya kwanza kama sijajichanganya.
 
Ntapatia wapi kanda zao au cds za hizo nyimbo za zamani wakuu? ?

Hizo nyimbo waweza kuzipata kwenye youtube...! Sina uhakika kuhusu CD/DVD zake kama bado zipo madukani
 
Sikonge

Natumaini Radio Habari Maalum Arusha wanazo VHC (waweza kuwasiliana nao)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom