Kwaya ya Barabara ya 13 Ulyankulu

Kwaya ya Barabara ya 13 Ulyankulu

Kwaya ilitikisa hiyo. Mungu awabariki wanakwaya wale.
 
samsonii mna-dhiri wa Munguu....anampenda msi-chana Delilaaah..... naye Delila................
 
Hii kwaya bado ipo,lakini haivumi kabisa kama zamani,walioimba hizo nyimbo nasikia wote waliisha rudi Burundi na awa waliopo walichukua ilo jina lakini wako butu sana.

Haa kumbe na wale ni kwetu pazuri? Nilipenda sana nyimbo zao utotoni!!
 
Kuna ule wimbo walikuwa wanaimba ''Mungu katuumba kwa mfano wake katutofausisha na vingine,katutofausisha na wanyamaa wasio na akili.................
Huu wimbo title yake ni ipi?

Title ya Albamu yenye hizo nyimbo zote alizoleta Baba Enock inaitwa siikumbuki, lkn walioimba ni Kwaya ya Barabara ya 13, Ulyankulu, na ilikuwa ni Vol. One. Ukienda maduka yanayouza Vitabu vya Kikristo utapata.
 
ni kati ya kwaya bora kabisa kuwai kutokea Tanzania.!
 
Kuna kwaya nyingine ya Arusha iliimba:

Kila atauchukua Mzigo wake mwenyewe
Kilamtu atabeba, habari zake mwenyewe mbele za Mungu
Siku hiyo ikifika

Wataalam Nyamayao, Baba_Enock saidia ilikuwa inaitwa kwaya gani?
Huo wimbo nikiusikia lazima nitubu dhambi zangu zote,na bia inageuka divai chapchap sana
 
Last edited by a moderator:
Ni ARUSHA TOWN CHOIR ya Wakatoliki. Ni lile Kanisa kubwa la Katholiki la pale Arusha na si pale kwa Babu karibu na Arusha Tech. Nafikiri umeshakumbuka hiyo mitaa yetu ya Arusha....

Fundi mchundo unamaanisha ngarenaro? Mbona jipya sana lile ukilinganisha na umri wa huo wimbo?? Au ulimaanisha St.Thereza kule town? Pale karibia na kwa father Babu pia kuna kanisa la Kilutheri.
 
Last edited by a moderator:
Nina maanisha lile Kubwa kabisa la Wakatoliki pale Mjini Arusha. Nafikiri ndiyo hile Mt. Theresa.

Ni lile ambalo karibu Matajiri wote wa Kikatoliki enzi hizo, unawakuta hapo.

Sorry, kwa Babu lilikuwa la Walutheri kama sikosei.

Hahahaha mkuu inaelekea hujaacha familia Arusha LOL
 
sijakupata hapa Sikonge, kwamba kanisa la kwa Babu ni la walutheri?
 
Ahh, huyu Asprin alinichanganya. Mwanzo niliandika sawa kuwa kwa babu ni Wakatoliki.....

Ni miaka mingi sasa zaidi ya 20 sijafika Arusha na kumbukumbu zinaanza kukimbia.

Ila karibu na Kanisa la babu, kulikuwa na kanisa jipya la Walutheri na nakumbuka kwenda kuimba hapo na Mwalimu wetu wa Kwaya, Somobody Mbajo, mdogo wake Mwalimu wa kwaya ya pale Kariakoo aitwaye pia Mbajo kama sijakosea.

Scan_20140208 (2).jpg

CD zake zinatolewa na Redio Habari Maalum - Arusha
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1391804202.556994.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1391804202.556994.jpg
    99.5 KB · Views: 164
  • ImageUploadedByJamiiForums1391804259.203327.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1391804259.203327.jpg
    134.4 KB · Views: 152
Wakuu wimbo wa kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe uliimbwa kwa mara ya kwanza na kwaya ya Uinjilisti KKKT Usharika wa mjini kati Arusha.Wimbo huu ulirekodiwa nchi Kenya enzi hizo Tanzania hapakuwa na studio yenye uwezo wa kurekodi muziki.Mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti zama ikijulikana zaidi kama kwaya ya vijana alikuwa akiitwa Bwana Msuya mfanyakazi wa idara ya kodi siku hizi TRA mpaka leo bado ni Mwalimu wa Kwaya ingawa alihamia kwaya ya KKKT Usharika wa Kijenge.Kwaya ya St Theresia mkabala na Usharika wa KKKT Mjini kati nayo iliupiga tena wimbo huu katika vionjo vya kikatoliki (Nadhani mtanielewa ninaposema vionjo vya kikatoliki)

Kinanda kilichotumika kupiga wimbo wa Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe kilitengenezwa Ujeruman sasa hivi ni kibovu tayari juhudi kubwa za kukipata aina ya kina hicho zimeshafanyika ingawa kiwanda kilichotengeza hakipo tena na juhudi za kupata spare kwaajili ya kukifanyia ukarabati zimeshindikana.Zipo nyimbo nyingine nzuri ambazo zilitumia kina hicho kama Bwana asema nitume mimi na nyinginezo nyingi.

Kama upo Arusha unaweza kupata kanda zenye nyimbo hizo katika usharika wa Mjini Kati KKKT ikiwa upo mbali na Arusha unaweza kuwasiliana na mimi nitakueleza utaratibu mzuri wa kuzipata kanda hizo ambazo hazijachakachuliwa na pia fedha zako zitatumika kuiendeleza kwaya ya Uinjilisti badala ya kuishia kwenye mifuko ya wajanja wachache wanaotafuna jasho la wasanii bila aibu.

Kuna kwaya nyingine ya Arusha iliimba:

Kila atauchukua Mzigo wake mwenyewe
Kilamtu atabeba, habari zake mwenyewe mbele za Mungu
Siku hiyo ikifika

Wataalam Nyamayao, Baba_Enock saidia ilikuwa inaitwa kwaya gani?
Huo wimbo nikiusikia lazima nitubu dhambi zangu zote,na bia inageuka divai chapchap sana

Ni ARUSHA TOWN CHOIR ya Wakatoliki. Ni lile Kanisa kubwa la Katholiki la pale Arusha na si pale kwa Babu karibu na Arusha Tech. Nafikiri umeshakumbuka hiyo mitaa yetu ya Arusha....

Fundi mchundo unamaanisha ngarenaro? Mbona jipya sana lile ukilinganisha na umri wa huo wimbo?? Au ulimaanisha St.Thereza kule town? Pale karibia na kwa father Babu pia kuna kanisa la Kilutheri.

Nina maanisha lile Kubwa kabisa la Wakatoliki pale Mjini Arusha. Nafikiri ndiyo hile Mt. Theresa.

Ni lile ambalo karibu Matajiri wote wa Kikatoliki enzi hizo, unawakuta hapo.

Sorry, kwa Babu lilikuwa la Walutheri kama sikosei.

Hahahaha mkuu inaelekea hujaacha familia Arusha LOL

Ahh, huyu Asprin alinichanganya. Mwanzo niliandika sawa kuwa kwa babu ni Wakatoliki.....

Ni miaka mingi sasa zaidi ya 20 sijafika Arusha na kumbukumbu zinaanza kukimbia.

Ila karibu na Kanisa la babu, kulikuwa na kanisa jipya la Walutheri na nakumbuka kwenda kuimba hapo na Mwalimu wetu wa Kwaya, Somobody Mbajo, mdogo wake Mwalimu wa kwaya ya pale Kariakoo aitwaye pia Mbajo kama sijakosea.

Last edited by a moderator:
Ngongo asante kwa maelezo ila hebu subiri kidogo nikusumbue maana mie siyo mwenyeji tena Arusha.

Nakumbuka kulikuwa na Waalimu wawili wakali sana wa Kwaya KKKT hapo Arusha. Mmoja alikuwa anasemekana ni mtu aliyesomea Music kwelikweli na alikuwa na kichuma fulani cha kutune sauti wakati anaimbisha. Nimekisahau hicho chuma ila kipo hata kwenye Physics somo la SOUND. Huyu jamaa kama sikosei kwaya yao ilishinda kwenye mashindao ya Kwaya za Arusha mwaka 1988 kama sikosei yaliyofanyikia TENGERU huku watu wakiwatakia heri maana huko Dar, kulikuwa na Mwalimu Mbajo aliyekuwa akiogopwa sana kwa ufundi na utundu wake kwenye kwaya. Huyu Mwalimu alikuwa au wa Kijenge au Tengeru, sina uhakika kwa sasa maana miaka mingi.

Pia alikuwepo mwingine mwenye Madevu aliyekuwa Mwalimu wa kwaya ya kanisa kuu kama sikosei (kubwa lililokupo mjini). Nilikuwa nawapenda sana na kwaya yao hawa jamaa ila nilikuwa nasita kwenda kanisani hapo kusali kwani ukifika muda wa kutoa sadaka, ndiyo utagundua jinsi ulivyo masikini. Mie na hela yangu ya uanafunzi, nikaamua kukimbilia kanisa la Mzee Mtangoo (@Stephen Mtangoo, huyu ni Babu yako? Nakumbuka ile story ya kuku akisema "kamata nambaaa") na Mzee yule wa Kigogo alivyoniona tu akanifuata na kuongea na mimi na akasema ingawa mie ni Moravian na hapo Arusha hakuna Moravian, basi ananikaribisha sana kwake. Hapo nilijisikia kweli nyumbani ingawa walikuwepo matajiri pia kama Mzee Mollel sijui (Owner wa Tanalec, kampuni ya kutengeneza majiko na vifaa vya umeme) ila wengi walikuwa ni watu wa mikoa kama ya Dodoma, Singida na Iringa, masikini wenzangu.
Huyu Mwalimu wa hii kwaya mwenye madevu kwa kweli nilikuwa nampenda kwa sababu nyimbo zake zilikuwa zimetulia sana na Classic. kuna Kaseti walirekodi miaka hiyo ya 80 mwishoni kabisa na nilisikia tu baadhi ya nyimbo zake walipokuja Arusha Tech kuimba ila bahati mbaya sikubahatika kununua kaseti zao. Hii kwaya ya Mzee wa midevu ilikuwa inaitwaje? Ukisinisaidia hilo jina utakuwa umenisaidia sana kuzipata nyimbo zao. Ahhh, walikuwa wanampiga gitaa kijana mmoja ameweka Curl nywele zake...... na alikuwa akipigia gitaa sijui Band gani ya muziki hapo Arusha.

Again: Asante kwa maelezo yako ambayo naona wewe u mwenyeji kweli kweli wa Arusha.

BTW: Unaweza kunitumia jina la hicho kinanda na kifaa kinachokosekana/kilichoharibika kwenye Email? Naweza kujaribu kuwaulizia jamaa zangu fulani huko labda wataweza kukitafuta au hata kukitengeneza. Siahidi lolote zaidi ya kusema ntajaribu kama itawezekana.

Back
Top Bottom