Wana JF,
ninaomba japo kwa kifupi sana tulijadili hili la zzk na act yake,mtu huyu ametokea cdm ambako ameondolewa baada ya kubainika kuunda mtandao ambao ulikuwa na lengo la kufanya mapinduzi ndani ya chama alichokuwa,akisaidiwa na kina kitila mkumbo na samson mwigamba,na bila ya shaka na wengineo wengi kulingana na filamu ilivyoanzia kwa kina mwampamba ,shonza,na wengi wengineo.
sasa basi,kwanza alikanusha kwa nguvu zote,lakini kwa wale tunaomjua tulielewa kilicho ndani yake na hasa baada ya tuhuma zile kuwekwa mtandaoni ikiwemo humu JF.siku si nyingi akatangaza kujiuzuru ubunge baada ya kukosa sifa hizo kulingana na hukumu ya mahakama iliyomvua haki hiyo.kwa kuwa iliridhia maamuzi ya cdm.
lakini hii haikuwa bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango mahsusi wa kukamilisha usaliti wake baada ya team A ya kitila na mwigamba kukamilisha uporaji wa madaraka ndani ya ACT-tanzania ya Kadau limbu na kumtupa nje ya chama kwa msaada wa nguvu ambayo hadi sasa haieleweki ni nani yuko nyuma ya mpango huo,maana bwana limbu amemlalamikia had msajili wa vyama kwa kumtendea ndivyo sivyo.
-zitto amegeuka na kauli ya kusema alikimbia cdm wakati si kweli bali alifukuzwa.
meengi yamekwishaandikwa humu kumhusu zitto,na hata saed kubenea tayari amejikuta matatani kisa kuanika ukweli kuhusu zitto na tayari ameanza kuandamwa na serikali kisa zitto.
-leo zzk amegeuka mtetezi wa wangwe wakati alishiriki vikao vyote vilivyochukua maamuzi juu ya wangwe ndani ya cdm wakati huo
wakati watanzania na wapenda mageuzi nchini tunafurahia kitendo cha vyama vya upinzani nchini kuunda ukawa kwa nia ya kuunganisha nguvu na kuikomboa nchi kwenye utawala wa kifisadi,yeye zzk anakuja na mpango mahsusi wa kuimegua ukawa.
wakati watanzania tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu,na wakati tume ya uchaguzi ikiwa inasua sua na BVR,hatumsikii zzk na ACT akitoa tamko lolote kuhusu hilo kwenye mikutano yake zaidi ya kuishambulia ukawa na kumkaribisha Lowasa kwenye ACT.
wakati zitto huyu akiwa chadema mbona hakuwa anaweka nguvu nyingi kama sasa? na hata wakati fulani aliacha mikutano ya cdm na kwenda musoma kukisaliti chama kwa mkono.na hata alipobanwa hakuweza kutoa maelezo ya ni kwa nini,
zitto huyu huyu amekula fedha za NSSF zaidi ya milioni mia sita na zaidi,kwa kushirikiana na ramadhan dau kupitia kampuni yake ya leka dutigite lakini hakuwahi kuyakubali hayo hadharani na wala hataki yaongelewe.zzk pia alipewa fedha takriban milioni 33,kutoka kwa Rugemalira wa V.I.P engineering,lakini ya kwake yalinyamaziwa.na hata baada ya baadhi ya watuhumiwa wa escrow kumtaja yeye pia lakini mpaka sasa hajatamka lolote zaidi ya kukaa kimya.
sasa kwa kutumia umaskini na njaa za baadhi ya kundi la watanzania wenye tamaa na wasioweza kuzizuia tamaa zao,na kwa kuwa anapewa sapoti kwa nguvu iliyojificha.anakuja na mpango wake huu wa kununua watu sambamba na mtindo anaoutumia lowasa na kundi lake,na hata baada ya mawasiliano ya kati yake na mwigulu kunaswa kwa njia ya e-mail,na kwa kuwa anajuwa ni ukweli na yameanikwa mbona hayakanushi ili tumuelewe alipo.
hitimisho langu kwa sasa nawaomba wale wote mliopangwa kama team ya mtandaoni na huyo zzk -------- mumrudie mungu na maombi yenu yanaweza kusikilizwa nae akawapa njia mbadala ya kujipatia kipato kingine tofauti na hii ya kupewa ujira kwa kuutumikia usaliti,maana utakiandama hata kizazi chenu kijacho
-