Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

100% pigia mstari,

wala si yeye ni mzalendo na wewe pia kama ni mzalendo tu
 
Wanajukwaa mimi namchukulia Kiongozi Mkuu(ingawa anaonaa soo kujiita Kiongozi Mkuu) wa ACT Wazalendo kuwa ni mtu makini kuanzia juu mpaka chini,yaani kuanzia unywele mpaka unyayo. Naomba kuweka kumbukumbu ya kauli alizowahi kunukuliwa ili kuonyosha umakini wake

  1. 1. Nitakuwa wa Mwisho kuondoka Chadema VS Tulianzisha ACT Wazalendo kutokana na kubinywa kwa demokrasia kwenye chama.
    2. Sitagombea tena ubunge, nitagombea uraisi 2015 VS Sitagombea tena uongozi,ninataka kufundisha 3. Sitagombea tena uongozi,ninataka kufundisha VS Sitagombea tena Kigoma Kaskazini,nitagombea Kigoma Mjini 4. UKAWA wachumia tumbo VS Tupo tayari kuungana na UKAWA 5. Sitagombea uongozi ACT,waliotegemea wameumbuka VS Kiongozi Mkuu wa ACT 6. Ni kweli CHADEMA ni wadini na wabaguzi VS Kilimanjaro na Arusha zina maendeleo sana lakini hazipo juu katika kuchangia pato la Taifa
Aidha katika suala la uwiano kati ya mchango kwenye pato la Taifa na Maendeleo ya Mkoa husika, Kiongozi Mkuu ameonyesha umakini mkubwa sana. Msome Mwana Duru Nguruvi3 uone jinsi gani Supreme Zitto K alivyo makini zaidi

DAHANA POTOFU INAYOENEZWA NA ACT

NI KUHUSU MGAWANYO WA RASILIMALI NA MAENDELEO

MBEGU INAYOPANDWA NA ACT NI CHAFU NA HATARISHI

Sehemu ya I

Ilipojadiliwa kama Rwanda na Burundi zijiunge EAC, iliundwa tume kukusanya maoni.

Mjadala huo uliingia bungeni . Zitto alinukuliwa akisema Tanzania haipaswi kuhofua kujiunga EAC kwasababu tofauti za kiuchumi hazipo EAC tu, zipo nchini.

Akasema mbona Tanzania ni nchi moja lakini kuna tofauti ya maendeleo kati ya Kigoma na Kilimanjaro!

Zitto na ACT wamenukuliwa akiongelea mgawanyo wa rasilimali, kwamba mikoa inayochangia zaidi pato ipo nyuma kimaendeleo.

Ametolea mfano wa Arusha na Kilimanjaro ikiwa na mchango michache , kimaendeleo ikiwa mbele

Kauli ya supreme leader haina ukweli kuhusu maendeleo bali kutafuta siasa rahisi na umaarufu butu

Supreme ameficha ukweli akijua, kutumbukiza mbegu ya ukabila na ukanda, itasaidia ima kumnyanyua kisiasa, au chama chake .
Ni mbegu ile aliyoikataa alikotoka japo alikuwa ni sehemu ya uongozi

Kauli imelenga kuwagawa wananchi kwa hoja dhaifu bila ukweli ina matatizo si kwa taifa tu bali kwa ACT ya ‘kizalendo ‘inayogawa wazalendo kwa misingi ya kikandaKauli hiyo imekuja kwa shinikizo la kisiasa linaloikabili ACT.

Matarajio ya haraka yanonekana kuwa na ugumu , kila mbinu safi na chafu zitatumika. Wazungu wanasema ‘shoot any moving object’’

Tuangalie dhana ya kwanini kuna tofauti za maendeleo kutoka sehemu moja hadi nyingine

Inatosha kusema tatizo la uwiano wa maendeleo si la Tanzania tu. Nchi zilizoendelea zina matatizo hayo kutokana na sababu tofauti

MAENDELEO

Ni hatua ya mabadiliko chanya kwa mtu, watu, jamii na taifa na ni zao la jitihada .
Maendeleo yana vichocheo vingi, vikiwemo elimu, mwamko, mazingira, maeneo na rasilimali kwa uchache wa kutaja

Katika nchi yetu, maendeleo yanaelezwa kwa vigezo kama Historia, jamii, na jiografia.

Hivyo kuangalia maendeleo bila kuangalia chanzo na vichocheo ni kupotosha umma.

Haiwezekani kuongelea Tanzania bila kuzungumzia ukoloni na athari zake, elimu, mwamko wa jamii, matumizi ya rasilimali na eneo husika kwa kuitazama jiografia ya nchi yetu.

Kauli za rahisi za eneo fulani ni tofauti na jingine bila kufafanua, ni za kichochezi, kufilisika kisiasa na dalili mbaya kwa jamii yetu.

Inaendelea…

Tumeishafunga mijadala ya huyo jamaa

Sorry.

Swissme
 
sifa mojawapo ya msaliti ni umakini, japo hakika ZZK sio makini kama unavyodhani ndo maana alikamatwa na mkakati wake, USALITI MWISHO WAKE NI KUUMBULIWA
 
mtu anayechukuachukua hela ili asaliti ukombozi ni njaa inamsumbua hawezi kuwa makini wakti ana njaa kali, ndo maana anakatwa kila mara na mbinu na janja yake
 
- Sijawahi ona kokote siasa inakofanywa mwanachama wa chama kimoja kwa wakati huohuo ni mwanzilishi wa chama kingine cha siasa, sijawahi.

- Sijawahi kuona mtu anajiunga na chama fulani baada ya siku tano anapewa uongozi mkuu wa chama hicho, sijawahi

- Sijawahi kuona popote siasa inapofanywa, mwenyekiti wa chama yupo chini ya mtu fulani. Yahani kikatiba kabisa kuna mtu yupo juu ya mwenyekiti, hii pia sijawahi kuona.

- Sijawahi kuona popote pale chama cha upinzani kukipinga chama cha upinzani na si chama tawala. AGAINST CHADEMA TANZANIA(ACT). Kwa maneno au hata vitendo. Chama kinafanya sherehe kikipata wafuasi wa upinzani kuliko wa chama tawala.

- Sijawahi kuona chama cha upinzani kinafadhiliwa na chama tawala kiuchumi na kimikakati. Tumefanya uzinduzi wa chama chako Zuberi kwa gharama kubwa sana, air time ITV, chakula, ukumbi expensive, na mbwembwe nyingi. Lakini mbona hujawahi kuchangisha pesa toka kwa wanachama wako? Kama kuna mtu anachangia ni nani huyo? Mtamlipaje baadae?

- Sijawahi ona chama cha upinzani popote pale siasa inapofanywa, wafuasi wake ni wale wanachama na wafuasi wa chama tawala. Le mutuz, laki si pesa, musa alani n.k, hii nayo sijawahi ona.

Kwa yote hayo juu Zuberi kwa nini nisikuite kwamba wewe ni msaliti halisi wa demokrasia hapa nchini. Kama kweli wewe siyo msaliti mbona hujawahi kujitokeza na kukataa zile namba za simu walizozitoa chama chako cha zamani kuwa zilitumika katika ufisadi? Mbona sijasikia kuikana ile akaunti ya benki wa yule dada kule ujerumani?

UKINIJIBU HAYO KWA UFASHA WEWE KWELI SI MSALITI.
For wise people, his or her focus is to see how the man is able to express the matter but not how the man is looks like. Be a wise man. ACT is the pathway to revolution.
 
Aisee jamani tumeshachoka sasa, zito mmefukuza kaondoka bado maneno hayaishi?

Hivi mfano umempa talaka mke wako alafu akaondoka ww uliyetoa talaka unalalamika tuu, mara oohh ulikuwa unanisaliti, maara oohh mwananmke gani wewe? sasa talaka umeshatoa na mtalaka kaondoka wewe bado unalalamika nini?

Nyie Chadema acheni upuuzi tumeshawachoka na kulialia kwenu haaa

Nayeye afanye siasa bila kumzungumzia mumewake wa zamani, kashapata mume mwingine ambaye ni ccm hivyo amuongelee mume mpya ccm
 
Habari yako msomaji,

Napenda nifungue hoja hii Kwa kuelezea kidoogo kuhusu ufahamu wa demokrasia na mageuzi duniani.

Zitto kama msomi kijana katika karne hii hakupaswa kutenda kosa hili la kiufahamu katika siasa. Tena katika muongo Huu tunaotaka kufanya mageuzi Kwa maslahi ya mamilioni ya Watanzania. Huu ni utovu wa nidhamu kisiasa na ataadhibiwa na siasa yenyewe.

Katika sehemu ya PILI ya hoja hii ni uwazi au usiri wa matakwa ya mabepari. Nikizungumzia mabepari kwa wataalamu wa siasa za kimataifa watakubaliana nami kwamba hii inayoitwa anakiki lazima uishi Kwa kusurrender baadhi ya mambo yako Kwa Mataifa makubwa. Zitto kuunda upinzan ndani ya upinzani anachimba shimo ambamo hawezi kuchomoka.

Wamagharibi hawana Shida ya nani awe Rais lakini rais dhaifu atajuta. Udhaifu wa ZZK unaonekana pale anaposhindwa kusoma alama kwamba UPINZANI ndani ya UPINZANI kosa na disunity ambayo wamagharibi hata akiwa Rais 2030 watatumia udhaifu. Na ZZK atapigwa na watanzania kwa kosa hata dogo tu kwa kuwa ashasaliti CHADEMA. Kuondoka CHADEMA hakumaanishi CHADEMA ni chama bora au laa. Kikubwa ni Tabia yako ikoje.

Kikubwa katika hili ni kwamba ZZK hawezi kuunda chama kitakacholeta upinzani wa kweli kutokana na kosa la kiufahamu. Ondoka CHADEMA sawa lakini uwe na nidhamu katika siasa.
 
Mkuu mansakankanmusa, moja ya misimamo yangu humu jf, ni kuheshimu mawazo ya kila mtu hata ziwe pumba kiasi gani!, hivyo naheshimu mawazo yako japo una matatizo katika kujenga hoja maridhawa!.

The botom line ya bandiko lako ni Zitto hawezi kuusaliti upinzani bado akabaki salama!, lakini jee pale upinzani wenyewe unapojisaliti, unaweza kuuelezeaje?!.

Ndani ya familia yenye watoto wengi, watoto wote hawawezi kufanana, kuna watoto wazuri, watoto watulivu, watoto waelewa, na kuna watoto wasumbufu, watoto watukutu na watoto jeuri na viburi!.

Wewe kama baba wa familia, ukiishawajua watoto wako, na tabia zao, unajua kabisa mtoto huyu ni mtoto mtukutu, jeuri na kiburi!, ukiletewa kesi ya mtoto huyo wewe kama mzazi jukumu lako la kwanza ni kufanya nini?!. Kumshukia mtoto kwa kumkanya na kumrudisha kwenye mstari, au kumuadhibu na kumfukuza nyumbani jumla?!. Mzazi mwenye busara, atamkanya mwanae, atamrudi na kujaribu kumrekebishika kabla hajashindikana!.

Hiki ndicho kisa cha Zitto na Chadema, Zitto ni mtoto ambaye ni born and breed ndani ya Chadema!. Chadema ndie mzazi, kaletewa kesi ya mtoto, badala ya kumkanya, kumuonya na kumrudi, yeye kachukulia hasira na kutimua jumla!. Hivyo kwangu mimi, Chadema kama mzazi, ndiye aliyefeli kwenye malezi ya mtoto Zitto!, licha ya kuziona dalili zote za mtoto mtukutu laziki hawakufanya juhudi zozote za malezi mema kwa kijao wao!.

Hata Marekani ndio iliyomtengeneza Saadam ili aishughulikie Iran!, vivyo hivyo ndio waliomtengeneza Osama aishughulikie Saudi Arabia!. Watoto wakakuwa na kuamua kuwarudi baba zao!. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Zitto, ataisumbua sana Chadema and there is no way, but sasa Chadema has to pay a very high price!.

Pasco.
 
Nakuwa na furaha napoona watu wakihangaika juu za zitto kabwe.Kitu bora na kizuri ni kwamba zito ameikisaliti chama na sio wananchi.bikira za mawazo na uwezo finyu ndo hufanya watu kumuona kama msaliti.Suala la msingi mwanasiasa yupo kwa ajili ya wananchi na sio chama .Zitto ameonyesha kuwa alikuwa na nguvu chadema thats why mnatapatapa juu yake.Usoni mnamkaaa moyoni mnakubali.
 
lakin mbona zzt amejibu tu kiraisi njia mliyotumia kupata pesa na mie natumia njia hiyo hiyo sasa msinihurize na pata wapi pesa kwanza jihulizeni nyinyi mlipata wapi pesa
 
Zzk ni shetani wa kisiasa. Et naeanataka urais amwongoze nani.labda urais wa kuongoza mbuzi.na siyo mtu ka mm .
 
Chadema ipo na itaendelea kuwepo

CHADEMA NI MPANGO WA MUNGU
 
Attachments

  • 1429781374458.jpg
    1429781374458.jpg
    24 KB · Views: 141
Huyo dogo ni nuksi, mimi hata kumuona sitaki. Msaliti barabara imefikia mwisho
 
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania, utakubaliana na mimi CHADEMA imepitia misukosuko mingi mpaka kuwa chama chenye nguvu na ambacho sasa kiko tayari kuchukuwa nchi.

Katika kipindi chote hicho cha kukua kwa CHADEMA lengo kubwa lilikuwa ni kumkombowa mtanzania dhidi ya ufisadi, dhuluma pamoja na aina zote za kumnyima haki mwananchi, mambo ambayo CCM wameyashindwa. MALENGO hayo makuu ndiyo yaliyoijenga CDM.

BAADA YA KUONEKANA KUWA CHADEMA INAIMALIKA, Hapo ndipo kidudu mtu kikaanza harakati zake za usaliti kwa kutufitinisha wanachadema na wapenda mabadiriko wote. Kwanini naita fitina ? ni kwasababu walitumia waraka wa siri, ambao waandishi wake walitumia majina bandia mf M1, MM nk kitu ambacho kinadhihirisha wazi kuwa hawakuwa na nia nzuri na mshikamano wetu.

Nasema hawakuwa na nia nzuri kwa sababu kwanza mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa juu na kwa nafasi yake angeweza kujenga hoja kwa uwazi ili kutushawishi, pili hawakuwa na nia nzuri kwa vile walifahamu wazi kwamba kwa wakati tulionao ni rahisi kutugawa kwa kuleta hoja ndogo ndogo tena kwa njia ya panya na yakichonganishi hivyo kututoa katika lengo kuu la kupambana na mafisadi na ufisadi.

JE HUYU SIO WASALITI? Kiongozi bora na mwenye nia nzuri hujenga hoja na kuwashawishi wanachama/wananchi kwa uwazi ili kuimalisha umoja wetu. Kwa kujilidhisha usome waraka wao wa siri.

NAPENDA KUTOWA PONGEZA kwa wote waliowezesha kupatikana kwa waraka ule wa siri, halafu kuyabaini majina ya wahusika, na licha ya awali kukanusha hatimaye walikiri kuhusika na kujitetea kwa hoja dhaifu.

SABABU KUBWA YA KUANDIKA HAYA LEO
Ni kuwataadhalisha viongozi wetu wa UKAWA kuwa lengo letu kuu kwa sasa ni kumpigania mwananchi apate haki zake dhidi ya ufisadi na aina zote za rushwa. kama vyama kuna mambo tunatofautiana, hivyo vitofauti ndivyo vitatumika na mafisadi kutugawa. HIVYO BUSARA INAHITAJIKA.
 
ni wakati sasa wa kila mpenda mabadikiko kushikamana na kuepuka kila aina ya propaganda yenye lengo la kuturudisha nyuma
 
Kweli ni kidudu mtu maana ajui anacho fanya mwisho wa siku atajinyonga msalit ajawahi kudum
 
Nasiku zote dhambi ya usaliti haiishi, huyu ni hatari sana siyo mtu wa kushirikiana naye.
 
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania, utakubaliana na mimi CHADEMA imepitia misukosuko mingi mpaka kuwa chama chenye nguvu na ambacho sasa kiko tayari kuchukuwa nchi.

Katika kipindi chote hicho cha kukua kwa CHADEMA lengo kubwa lilikuwa ni kumkombowa mtanzania dhidi ya ufisadi, dhuluma pamoja na aina zote za kumnyima haki mwananchi, mambo ambayo CCM wameyashindwa. MALENGO hayo makuu ndiyo yaliyoijenga CDM.

BAADA YA KUONEKANA KUWA CHADEMA INAIMALIKA, Hapo ndipo kidudu mtu kikaanza harakati zake za usaliti kwa kutufitinisha wanachadema na wapenda mabadiriko wote. Kwanini naita fitina ? ni kwasababu walitumia waraka wa siri, ambao waandishi wake walitumia majina bandia mf M1, MM nk kitu ambacho kinadhihirisha wazi kuwa hawakuwa na nia nzuri na mshikamano wetu.

Nasema hawakuwa na nia nzuri kwa sababu kwanza mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa juu na kwa nafasi yake angeweza kujenga hoja kwa uwazi ili kutushawishi, pili hawakuwa na nia nzuri kwa vile walifahamu wazi kwamba kwa wakati tulionao ni rahisi kutugawa kwa kuleta hoja ndogo ndogo tena kwa njia ya panya na yakichonganishi hivyo kututoa katika lengo kuu la kupambana na mafisadi na ufisadi.

JE HUYU SIO WASALITI? Kiongozi bora na mwenye nia nzuri hujenga hoja na kuwashawishi wanachama/wananchi kwa uwazi ili kuimalisha umoja wetu. Kwa kujilidhisha usome waraka wao wa siri.

NAPENDA KUTOWA PONGEZA kwa wote waliowezesha kupatikana kwa waraka ule wa siri, halafu kuyabaini majina ya wahusika, na licha ya awali kukanusha hatimaye walikiri kuhusika na kujitetea kwa hoja dhaifu.

SABABU KUBWA YA KUANDIKA HAYA LEO
Ni kuwataadhalisha viongozi wetu wa UKAWA kuwa lengo letu kuu kwa sasa ni kumpigania mwananchi apate haki zake dhidi ya ufisadi na aina zote za rushwa. kama vyama kuna mambo tunatofautiana, hivyo vitofauti ndivyo vitatumika na mafisadi kutugawa. HIVYO BUSARA INAHITAJIKA.

Mungu yupo pamoja na wote wanaopambana dhuluma za wanyonge.WABARIKIWE WOTE WENYE NIA NJEMA NA CHADEMA.MUNGU ANAJUA MEMA YOTE MLIYOIFANYIA NCHI MPAKA SASA.Binafsi sitampenda maisha yangu yote huyo msaliti Wa mabadiliko ya kweli.
 
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania, utakubaliana na mimi CHADEMA imepitia misukosuko mingi mpaka kuwa chama chenye nguvu na ambacho sasa kiko tayari kuchukuwa nchi.

Katika kipindi chote hicho cha kukua kwa CHADEMA lengo kubwa lilikuwa ni kumkombowa mtanzania dhidi ya ufisadi, dhuluma pamoja na aina zote za kumnyima haki mwananchi, mambo ambayo CCM wameyashindwa. MALENGO hayo makuu ndiyo yaliyoijenga CDM.

BAADA YA KUONEKANA KUWA CHADEMA INAIMALIKA, Hapo ndipo kidudu mtu kikaanza harakati zake za usaliti kwa kutufitinisha wanachadema na wapenda mabadiriko wote. Kwanini naita fitina ? ni kwasababu walitumia waraka wa siri, ambao waandishi wake walitumia majina bandia mf M1, MM nk kitu ambacho kinadhihirisha wazi kuwa hawakuwa na nia nzuri na mshikamano wetu.

Nasema hawakuwa na nia nzuri kwa sababu kwanza mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa juu na kwa nafasi yake angeweza kujenga hoja kwa uwazi ili kutushawishi, pili hawakuwa na nia nzuri kwa vile walifahamu wazi kwamba kwa wakati tulionao ni rahisi kutugawa kwa kuleta hoja ndogo ndogo tena kwa njia ya panya na yakichonganishi hivyo kututoa katika lengo kuu la kupambana na mafisadi na ufisadi.

JE HUYU SIO WASALITI? Kiongozi bora na mwenye nia nzuri hujenga hoja na kuwashawishi wanachama/wananchi kwa uwazi ili kuimalisha umoja wetu. Kwa kujilidhisha usome waraka wao wa siri.

NAPENDA KUTOWA PONGEZA kwa wote waliowezesha kupatikana kwa waraka ule wa siri, halafu kuyabaini majina ya wahusika, na licha ya awali kukanusha hatimaye walikiri kuhusika na kujitetea kwa hoja dhaifu.

SABABU KUBWA YA KUANDIKA HAYA LEO
Ni kuwataadhalisha viongozi wetu wa UKAWA kuwa lengo letu kuu kwa sasa ni kumpigania mwananchi apate haki zake dhidi ya ufisadi na aina zote za rushwa. kama vyama kuna mambo tunatofautiana, hivyo vitofauti ndivyo vitatumika na mafisadi kutugawa. HIVYO BUSARA INAHITAJIKA.

Wewe pamoja na akina Lema wote hamjielewi, waraka wa akina Mwigamba ulikuwa na kosa gani? Kwani kupanga mkakati wa ushindi unapoingia kwenye ushindani ni kosa? Mbona hata sasa CHADEMA inapanga mikakati ya ushindi pamoja na UKAWA katika uchaguzi mkuu?

Mbowe alikuwa na hofu gani ya kuogopa kupata mshindani, kama alikuwa anajiamini si angewaacha na mkakati wao alafu awashinde kwenye kura? Mnasema oho oo walitaka kufanya mapinduzi, umewahi kusikia wapi mapinduzi yanafanywa kwa kupiga kura?
 
Back
Top Bottom