Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Wanajamvi heshima sana,

Ngongo wa JF ajiunga na ACT Wazalendo chama makini kinachoongozwa na Kiongozi Mkuu --------- Zitto Zuberi Kabwe.Zipo sababu nyingi zilizonifanya nijiunge na chama hiki makini leo nitazitaja sababu chache tu ila nikipata muda nitaongeza nyingine ambazo hata wewe zinaweza kukushawishi.

Mosi,Ngongo ni muumini wa siasa za kufuata watu usiniulize kwanini ndivyo nilivyozaliwa.Nimeamua kumfuata --------- Zitto kwasababu katika yeye nimeyaona matendo na misimamo yake isiyoyumba wala kutetereka.Ikumbukwe Zitto Kabwe katika nafasi ya naibu katibu mkuu alishiriki kuondoa minyukano ya kugombea madaraka,sikuwahi hata mara moja kumwona Zitto akitamani nafasi ya Mwenyekiti wa chama au kiongozi mkuu wa upinzani bungeni ndio maana hata alipojiunga na ACT alikataa katu katu nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha ACT.Katika Hili Zitto kawazima na kuwaacha hoi bin taabani wale wote waliokuwa wakimpakazia kwamba yeye ni mwenye tamaa na uchuu wa madaraka.

Zitto ni mjamaa mwenye kufuata misingi ya Mwl Nyerere na Mimi ni mjamaa mwenye kufuata mkondo huo huo ni kwanini nisijiunge na ACT Wazalendo.Mimi Ngongo namiliki Nyumba 6,Mashamba makubwa 3,Magari 5 si ya kiafahari a) Land Cruiser VDJ 201 b) Ranger Rover 2015 c) Hammer d) Bugatti Veyron e) Lamborghini Roadster.Vimali vyote hivi nimevipata kupitia siasa za Tanzania ikiwa ni pamoja na kukataa posho,kukataa misamaa ya kodi wanayopewa wabunge wote wa bunge la muungano.Bahati nzuri Kiongozi Mkuu si mpenda mali wala madaraka wote tunafuata siasa za kijamaa ingawa katika dunia ya leo zimeshindwa sijui ni jinsi gani mimi na Zitto tutaweza kulifanikisha hili labda kwakuwa sisi tutakuwa mfano na wengine watatuiga.

Pili Ngongo kaamuwa kujiunga na ACT kwakuwa kiongozi mkuu ni mkweli kila anachokisema ndicho anachokifanya hajawahi hata mara moja kusema kitu asichokimaanisha.Endelea kunifuata taratibu nikuonyeshe Kiongozi mkuu alivyo mkweli daima.Zitto alinukuliwa na wanahabari akikanusha vikali

a) Kwamba yeye haijui ACT wala hausiki na uanzishwaji wake.

b) Kwamba yeye hawezi kuhama CDM atakuwa mtu wa mwisho kuhama CDM

c) Kwamba amejipanga kugombea urais mwaka 2015 huku akijua kakosa sifa ya kugombea (umri) hata katiba pendekezwa haimruhusu

d) Kwamba ni Zitto Kabwe aliyeliibua sakata la ESCROW akina Kafulila walidandia tu.

e) Hajui chochote wala hana mahusiano na Prof Kitila & Samson Mwigamba.Leo ni wamoja labda ni kwa bahati mbaya nakuachia wewe msomajo kutengua hiki kitendawili ingawa sikupi mji katu.

f) Kwamba angeachana na siasa baada ya kipindi chake cha ubunge kwisha mwaka 2015.Zitto leo ni kiongozi mkuu tena baada ya kufukuzwa ubunge aliwaaga wabunge angerejea mjengo tena.Hii inapingana na kauli yake kwamba angeecha siasa na kwenda kufundisha chuo kikuu.Hii tunaweza kumsamee kwakuwa nafasi ya kiongozi mkuu si nafasi ya kisiasa sanaa anaweza kugawa muda wa kufundisha chuo kikuu na muda mwingine wa kiongozi mkuu usishangae hizi ndio siasa za kitanzania nchi ya watu wasiopenda kufikiri sana ukiweza kubwa bwaja utawasomba wengi.Mbona Gwajima anafufua wafu hakuna anayehoji wala kuuliza makaburi yao kanunua chopa mnaanza wivu wenu wa kike.Nasema nimeamua kumfuata Zitto ACT ndio habari ya mjini mengine kelele ebooo.

Zitto ndio mkombozi wetu bwana wengine wote njaa,Zitto ni mwanasiasa pekee aliyekataa kupokea posho hata akifanya ziara za kikazi NSSF,TANAPA..... na mashirika mengine mengi ya umma hachukui hata senti tano.Kuna kipindi Zitto na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF walisafiri na timu yetu ya taifa Zitto alijilipia nauli na malazi mwenyewe hakuchukua ndururu ya NSSF.

Zitto kama mwenyekiti wa PAC kila mara amekuwa mfano bora wa kukataa posho za mashirika ya umma wanayoyakagua ingawa kuwana kipindi payment voucher za Ngorongoro Creater Area Authority zilionyesha Zitto alikuwa akilamba allowances hiyo haitoshi kumfanya Zitto fisadi labda hizo voucher ziligushiwa kumchafua kiongozi mkuu.

kuwasilisha afya hoja kwa hoja na si viroja.

Wanasiasa wasio na hoja za kuwaambia watu hukimbilia kwenye uongo, matusi na propaganda.Hizi ni siasa za kale ambazo hazina faida kwa mwananchi.

ACT inasimama kwenye hoja za msingi za kumkomboa mnyonge wa Tanzania na kuharibu mifumo inayolea uongozi mbovu na usio na maadili.Watanzania wamekuwa na bahati mbaya ya kukosa sera wala hoja kwenye mikutano ya siasa kwa muda mrefu, kwa muda mrefu mikutano ya kisiasa imekuwa ni mipasho na mikutano ya taarabu za nani anaweza kuzodoa zaidi.ACT inaleta siasa za kisasa, siasa za kistaarabu na siasa za hoja tu.Watanzania wqmeendelea kukipokea na mtashuhudia mengi kadri siku zinavyokwenda.

Treni ya mabadiliko imeishaondoka kituoni, imeanza safari, upepo huu wa mabadiliko utawasomba wengi wanaoendekeza siasa za kale, Watanzania wanataka siasa safi, wanataka mabadiliko.

ACT WAZALENDO, TAIFA KWANZA, TURUDI KWENYE MISINGI
 
Mkuu Molemo haaa haaa nilikwapua cheo cha kiongozi mkuu wa Iran naona Mods wanamlinda sana Kiongozi Mkuu.


Mkuu Ngongo Hongera...

Hizo sehemu zimetokea dash unaweza kuandika cheo chake kingine cha CEO au Mfalme.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa sina chama ukitaka ushahidi muulize Pasco wa JF.
Hapa nakuamini...sihitaji kumuuliza mtu kauli uliyotoa mwenyewe tena ukiwa na akiri yako timamu...
 
Last edited by a moderator:
usitegemee kuitwa msaliti ndan ya ACT hata kama upo kimwili..... team wazalendo unaweza jiunga au la n kujipima tu
 
Mtahangaika sana na Zitto kishatoka kwenye saccos yenu kwanini msimuache? Kweli nimeamini mtu hushughulishwa na kile anachokipenda, mnashughulika mno na kijana wa mwandiga inaonyesha jinsi gani mnamkubali,
 
Last edited by a moderator:
Hata ktk msafara wa majoka na kenge wapo. Ktk utawala bora concesus haliepukiki kwa kiongozi makini. Misimamo lazima iwe neutral ili ileta matokeo chanya kwa kuwa hakuna binadamu aliekamilika. Msimamo wa mbabe mmoja (kiongozi mkuu) ktk taasasi fulani ni udikteta na hauleti impact chanya. Shtuka
 
Post yako nimeipenda sana na huo ndo ukweli wenyewe,ila watanzania tunapenda kuwapa kipaombele wale wanaobwabwaja sana huku matendo ni zero e.g --------.
 
Zitakapoanza chopa kukata anga, ZZK atasahaulika na ujamaa wake, nyie mnadhani nani anapenda umaskini? ujamaa ni umaskini ndio maana umeshindwa
 
Nataka kuweka kumbukumbu vizuri, wakati ule CDM inamwambia ZZK kuwa ameanzisha chama alikataaa na wafuasi wake ndani na nje ya JF walipinga, nataka niwakumbushe wafuasi wa ZZK wasiwe wapumbavu. Hii kauli aliitoa Nyerere akimwambia Kawawa asiwe mpumbavu kama Lowassa, wakati EL alitaka nyerere aende monduli kumpigia kampeni kusafisha hali ya hewa kwani kwa Mwalimu kumkataa EL kwa madai ya RIshwa na Ufisadi kwa maoni ya EL angehatarisha asipate hata UBUNGE.

Sasa jiorodhezesheni hapa wale ambao mlikuwa mnapost kupinga kuwa ZZK hajaanzisha chama.

Post zinaonesha kuwa nyinyi kweli mko tayari kusapoti msichokijua, sijui pia shida ni nini, tumbo? au magari hapa mjini? shida ni nini??? wafuasi wa ZZK je hawana uwezo wa hela na akili au? alikataa nanyi mkamuunga mkono kumbe intelegensia yetu Kubwa, haiwezi fanya makosa, jiorodhesheni kwa ajili ya kupata msaada wa ada mkaongeze maarifa. Maarifa madogo, huwezi ona jambo kabla halijatokea wewe ni sawa na mtoto mdogo wa miaka chini ya mitano, JF sio saizi yenu.

Nawasilisha
 
Wazee wa kimarangu na kishumundu kwanini msifanye yenu badala yake mnamdandia zitto kwani kawakosea nini.
 
Chadema wamechanganyikiwa kabisa na ACT, Zito amewashika pabaya
 
Chadema hawafuatilii tena maendeleo ya saccos yao. Macho na Masikio yao yako kwa Zityo na ACT
 
Mlipomfukuza mlitaka adharirike ili mseme chama ni zaidi ya zito.sasa nafikiri sasa mnaamini kwamba zito alikuwa ni zaidi ya chadema.wachaga naona hamuamini kilichotokea.
 
Wekeni orodha yenu vizuri, wambieni na wenzenu waliorodheshe (MLIDANGANYWA MKADANGANYIKA)
 
Back
Top Bottom