Nilitamani nijibiwe hayo madai yangu unless Zitto ni msaliti mkuu wa demokraamsia nchini
Ndugu mleta mada,
Sidhani kama ni mbaya tukijadiliana haya with common sense:
1. Wewe ukiwa katika kampuni flani unafanya kazi baada ya miaka kadhaa kwa sababu moja au nyengine ukaona kabisa hapa sina maisha marefu kazini kutokana na yaliyotokea. At that particular moment ukiwa unasubiria lile swala uliloliona kwa mtazamo wako la kufukuzwa kazi wewe unafanya nini? unasubiri barua ya kufukuzwa kazi ije uichukue uende nyumbani ukaangaliane na mkeo nyumbani? Is that real in life?
Nionavyo: Kama ni mimi na naamini wengi watakuwa hivo wakikutana na situation kama hiyo jambo la msingi ni kuhangaika kutafuta kazi kabla barua unayoitegemea haijakufikia rasmi.Sina haja ya kueleza yote yaliyotokea kwa ZZK koz yanajulikana na kama nilivyosema source ya yote ni pale ZZK alipoamua kuonyesha nia ya kugombea uenyekiti mengine yaliyofuata ni yatokanayo,so kama mwanasiasa hakuwa na jinsi baada ya kuona kufukuzwa kwake kukija zaidi ya kuangalia option ya kisiasa huku akiwa anasubiria ufukuzwaji rasmi wa wenye chama.
2.
Swala la Kiongozi mkuu wa chama kuwa juu ya mwenyekiti: Huo ni mfumo tu ambao Chama na wanachama wamejiamulia,na kama kwao haina shida iweje iwe na shida kwako au kwa kuwa nafasi ya juu amekaa mtu unayemchukia?,koz mfumo wa utawala ni makubaliano,ni kama ndoa,sasa wanandoa wamekubaliana waishi hivi wewe inakuuma does that make sense?
3.
Chama cha upinzani kufadhiliwa na CCM: Ingekuwa vizuri ukizungumza jambo kama hilo ungeweka wazi na evidence ya hicho unachokizungumza ili watanzania waweze kujua ukweli sio kutoa tu maneno ya mdomoni yasiyo na mashiko ukitegemea watanzania wakuamini,ni sawa na pale Chadema walipoiita CUF ni CCM-B bila vigezo,kwa wenye akili walipuuza na kuendelea kuamini kuwa CUF ni upinzani halisi usio na uhusiano na CCM,too bad leo CHADEMA hao hao wamekuja ku proof kuwa CUF is a genuine Opposition.Kwahiyo hoja kama hii inahitaji evidence kuwa na mashiko.
4.
Hoja ya wanachama wa ACT kuwa wa Chama tawala: Maelezo yake yanafanana na ya 3 hapo juu: Ndugu are you sure you are in the right place? JF ni Valley ya Great Thinkers usiigeuze kijiwe cha kahawa.
5.
Kuamua kumuita ZZK msaliti: Hiyo ni haki yako kikatiba hakuna anayekukataza,nimeshakupa mfano hapo juu,Chadema waliamua kuiita CUF ni CCM-B lakini kilichotokea na kuendelea leo itabaki kuwa historia.
Kwa hiyo wewe uliyeamua kumuita ZZK ni Msaliti uko sawa kama walivyo sawa wale ambao mpaka dakika hii wanaomuona kuwa shujaa na mkombozi na mtetezi wa wanyonge katika Taifa hili.
BY: Independent-Mind