MANI
Platinum Member
- Feb 22, 2010
- 7,318
- 6,394
Wanasiasa wasio na hoja za kuwaambia watu hukimbilia kwenye uongo, matusi na propaganda.Hizi ni siasa za kale ambazo hazina faida kwa mwananchi.
ACT inasimama kwenye hoja za msingi za kumkomboa mnyonge wa Tanzania na kuharibu mifumo inayolea uongozi mbovu na usio na maadili.Watanzania wamekuwa na bahati mbaya ya kukosa sera wala hoja kwenye mikutano ya siasa kwa muda mrefu, kwa muda mrefu mikutano ya kisiasa imekuwa ni mipasho na mikutano ya taarabu za nani anaweza kuzodoa zaidi.ACT inaleta siasa za kisasa, siasa za kistaarabu na siasa za hoja tu.Watanzania wqmeendelea kukipokea na mtashuhudia mengi kadri siku zinavyokwenda.
Treni ya mabadiliko imeishaondoka kituoni, imeanza safari, upepo huu wa mabadiliko utawasomba wengi wanaoendekeza siasa za kale, Watanzania wanataka siasa safi, wanataka mabadiliko.
ACT WAZALENDO, TAIFA KWANZA, TURUDI KWENYE MISINGI
Ina maana hayo maneno kiongozi mkuu hakuyasema au kufanya?