- Sijawahi ona kokote siasa inakofanywa mwanachama wa chama kimoja kwa wakati huohuo ni mwanzilishi wa chama kingine cha siasa, sijawahi.
- Sijawahi kuona mtu anajiunga na chama fulani baada ya siku tano anapewa uongozi mkuu wa chama hicho, sijawahi
- Sijawahi kuona popote siasa inapofanywa, mwenyekiti wa chama yupo chini ya mtu fulani. Yahani kikatiba kabisa kuna mtu yupo juu ya mwenyekiti, hii pia sijawahi kuona.
- Sijawahi kuona popote pale chama cha upinzani kukipinga chama cha upinzani na si chama tawala. AGAINST CHADEMA TANZANIA(ACT). Kwa maneno au hata vitendo. Chama kinafanya sherehe kikipata wafuasi wa upinzani kuliko wa chama tawala.
- Sijawahi kuona chama cha upinzani kinafadhiliwa na chama tawala kiuchumi na kimikakati. Tumefanya uzinduzi wa chama chako Zuberi kwa gharama kubwa sana, air time ITV, chakula, ukumbi expensive, na mbwembwe nyingi. Lakini mbona hujawahi kuchangisha pesa toka kwa wanachama wako? Kama kuna mtu anachangia ni nani huyo? Mtamlipaje baadae?
- Sijawahi ona chama cha upinzani popote pale siasa inapofanywa, wafuasi wake ni wale wanachama na wafuasi wa chama tawala. Le mutuz, laki si pesa, musa alani n.k, hii nayo sijawahi ona.
Kwa yote hayo juu Zuberi kwa nini nisikuite kwamba wewe ni msaliti halisi wa demokrasia hapa nchini. Kama kweli wewe siyo msaliti mbona hujawahi kujitokeza na kukataa zile namba za simu walizozitoa chama chako cha zamani kuwa zilitumika katika ufisadi? Mbona sijasikia kuikana ile akaunti ya benki wa yule dada kule ujerumani?
UKINIJIBU HAYO KWA UFASHA WEWE KWELI SI MSALITI.
Kabla hatujaaminishwa hiki kilichoandikwa juu ya Zitto kabwe na ACT,ni bora tupate kwanza majibu ya maswali haya.
Nataka kurudi Chadema mara baada ya .....
Nitayaamini maneno yanayotolewa na
wanachadema siku siku haya maswali
yakipatiwa majawabu
Natamani sana kuwa Kamanda lakini haya
yananitatanisha,naombeni majibu ili nifanye
maamuzi magumu.
1.Walituambia kuwa chama cha wananchi CUF
ni tawi la ccm,wakaenda mbali kwa kuwaita
kuwa ni chama cha Mashoga ghafla wakasahau
matusi yao na wakaanza mashirikiano
Mapya,Je ile tuhuma iliishia wapi?
2.Chadema walituaminisha kuwa Chama cha
NCCR mageuzi kimejaa Usalama wa
Taifa,wakaenda mbali wakamkejeli Mbatia, tena
ndani ya Bunge kuwa,yupo Upinzani huku
akiitumikia ccm,ghafla tu Mbatia ni Mshirika
namba Mbili wa Ukawa bila watanzania
kuelezwa kama zile tuhuma zilikuwa za kweli
au za kutunga kwa nia ya kuwalaghai watu.
3.Chadema kwenye Ilani yake 2010
walituambia kuwa tukiwachagua hawatachukua
posho kama hatua mojawapo ya kuonyesha
kwa vitendo kuchukizwa na matumizi mabaya
ya serikali.Je Kwanini wamekiuka Ilani yao?
4.Chadema Mwaka 2011 walikataa kushirikiana
na vyama vya Upinzani ili kuunda kambi ya
Upinzani yenye sauti na nguvu,wakatuambia
kuwa Vyama vyote ni mawakala wa ccm
isipokuwa Chadema,hivyo kushirikiana nao ni
kurudisha nyuma harakati za ukombozi,ghafla
tu baraza kivuli la mawaziri likavunjwa na wale
vibaraka wa ccm wakaingizwa kwenye kambi
ya upinzani bila sisi wafuasi kuambiwa ni lini
ukibaraka wao umeisha mpaka wakaaminiwa.
5.Tuliambiwa kuwa David Kafulila ni mtu hatari
kwa ustawi wa Upinzani hasa
Chadema,tukaambiwa ni Sisimizi ambae hana
umuhimu wowote ndani ya Chadema ,ghafla tu
Sisimizi kageuka tembo,Mtu hatari kageuka
Shujaa na sasa ananadiwa na viongozi wa
Chadema kuwa ukawa imepata tuzo,Je ni lini
kafulila alianza kuaminiwa ?
6.Tuliambiwa tena kuwa ,Serikali kutumia
mashangingi huku Zahanati hazina dawa ni
kiwango cha juu cha Ubinafsi,Mbowe akalikataa
Shangingi la Kiongozi wa Upinzani....ghafla
nimemuona Bukoba akiwa na Shangingi lenye
maandishi KUB. Je ndio lilelile alilolikataa
hadharani au ni lingine?
7.Mbowe alituahidi kwenda mahakamani,na
kudai kuwa wanasheria wake wanaandaa
mashtaka dhidi ya Zitto Kabwe baada ya Zitto
kumtuhumu kuwa alipokea fedha toka kwa
makada wa ccm na kuwa alicheza dili ns
Kinana kuhusu deni analodaiwa na NSSF.Je
taratibu za ufunguaji kesi ziliishia wapi ?
8. Chadema Mwaka 2011 ilitangazia Umma
kutomtambua Rais Kikwete kwakuwa
alishindwa na Slaa,ghafla wanatangaza kuomba
mashauriano na Rais waliemkataa,wakafika
Ikulu kujadiliana juu ya maswala mbalimbali ya
Kitaifa,wakanywa Juice na kupiga picha,Je ni
lini Chadema ilianza kumtambua Rais na
kwanini sisi wananchi hatukuelezwa kuwa
kuanzia sasa Kikwete ni Rais?
Sina nia ya kuibua Marumbano yasiyotujenga
bali nataka mtu mwenye uelewa mkubwa kuliko
mimi anaondoe Uvulivuli ili nami nijitambue.
Naomba nijibiwe hayo ili nami niwe Kamanda
nitakaeitetea Chadema popote.
Hayo Majawabu yakipatikana,ndio utakuwa
mwisho wa Chama cha ACT-Wazalendo maana
umma utaiamini Chadema na hivyo kuiunga
mkono.
Kama Maswali yakikosa Majibu basi Chadema
itakosa uhalali wa kutuhumu ACT-Wazalendo na
viongozi wake na hivyo wananchi wataendelea
kujiunga na ACT-Wazalendo kwa kuamini kuwa
maneno yoyote yanayotolewa na Chadema ni
Ulaghai.
Karibuni kwa majibu Makamanda ili nasi tupate
chakuwaambia wananchi ili waipuuze ACT-
Wazalendo.