Mara Baada ya kupata Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere Aliwahi kuwataja Maadui watatu wa Taifa kuwa ni UJINGA, UMASKINI na MARADHI.
Hivyo alitutaka kama Taifa ili tusonge Mbele ni Lazima Tupambane na Vitu hivi Vitatu.
Mwl Alifahamu bila Elimu Bora hakuna Maendeleo, bila mtaji na kipato hakuna Maendeleo.
Na Bila kuwa na Afya njema na Nzuri kwa Watanzania hakuna Maendeleo.
Mambo hayo matatu yalikuwa Vikwazo Vikuu kwa Taifa kuendelea.
Hivyo Alipambana na Haya mambo matatu kwa kutoa Elimu Bora kwa Watanzania huku akisema " Ukitaka kumsaidia Maskini msomeshe mtoto wake"
Akiwa na Nia ya kumtoa katika Ujinga, maradhi na Umaskini kwa kuweza kuyatawala mazingira yake Vizuri.
Ila kwa sasa kama taifa Tuna Adui wetu mpya Chini ya Adui wetu mkuu mwingine Aliyeongezeka Ambaye ni Mbaya kuliko wote.
Anayetishia UHAI wa Taifa letu.
Adui huyu ni Ugonjwa hatari zaidi ya Ukimwi hasa hasa Anapojaribu kuwadumisha Wakulima wa korosho kujileta Maendeleo.
Tumekumbwa na Adui Mwingine Mbaya zaidi Kaongezeka naye ni ZITTO ZUBERI KABWE.
Nimjuavyo Zitto Asipodhibitiwa Mapema Ataturudisha katika Vifungo vya Umaskini, Ujinga na Maradhi.
Bila kujali Cheo chake au Chama chake cha siasa Zitto ni Adui Ambaye Anatakiwa Kudhibitiwa kabla Haja athiri Taifa.
Mpaka sasa Zitto Kabwe Kashalihujumu Taifa kwenye mambo yafuatayo:-
#ZITTO vs SGR:
Ni zitto huyu huyu Aliyepinga Uamuzi wa Serikali kutumia Fedha za Ndani kujenga Reli, Zitto aliona hakuna Umuhimu wa kujenga Reli ya kisasa ya SGR.
Zitto alitaka Fedha ziwekweze kwenye Kilimo, Kujenga Vyuo vya Ufundi na kwenye Stuntedness.
Kila siku Najiuliza Ni kweli Zitto ni Mrundi na Anatumiwa na Mabeberu wa EU?
#ZITTO vs BOMBARDIER:
Ni zitto huyu huyu na Tundulissu ndio Waliofurahia Bombardier yetu kukamatwa na wakanada.
Ni Zitto huyu aliyesema tunanunua Ndege mbovu na za mtumba.
Ni Zitto huyu Aliyesema Kipaumbele chetu sio Ndege.
Ni Zitto huyu Aliyesema Rais Magufuli amenunua Ndege kwa gharama kubwa kuliko bei ya kwenye Kampuni za Ndege.
Ndio maana Kila siku Najiuliza ni kweli Zitto ni Mrundi na Anatumiwa na Mabeberu wa EU?
#ZITTO vs STIRGEL GORGE:
Ni Zitto huyu Aliyepinga Bungeni kwa Uamuzi Wa Serikali kukata Misitu kwenye Selous Akidai ifanyike Tathimini ya kimazingira juu ya athari za Ukataji Miti.
Ni Zitto huyu Alisema Huu mradi ni Gharama na Hasara kwa Nchi kwani Tunayo Mradi wa Gesi kwa nini Tusiutumie?
Kila siku najiuliza hivi ni kweli Zitto ni Mrundi na anatumiwa na Mabeberu wa E.U?
#ZITTO vs MAKINIKIA:
1)Unakumbuka Juzi Alimuuliza swali la Mtego waziri wa Katiba na sheria Prof Kabudi kuwa kuna kesi ngapi za makampuni zimefunguliwa baada ya issue ya Makinikia?
2)Ni Zitto Aliyesema Tanzania haiwezi kuwadhibiti wawekezaji wa Uchimbaji Madini
3)Ni Zitto Aliyesema Makinikia ni Mali ya Barrick Anayejaribu kuzuia Makinikia yasisafilishwe kwenda nje ya Nchi wanakosea sana.
#ZITTO vs CHADEMA/UKAWA
Nakumbuka kauli ya John Mnyika Aliwahi kusema Adui mkubwa wa Ukawa ni Zitto.
Mnyika Aliona Adui mkubwa wake sio Ujinga, Umaskini wala Maradhi.
Aliona Adui mkubwa wa Chadema na Ukawa ni Zitto
2)Unakumbuka Zitto Alivyounda kundi la Uasi (MP7) ndani ya Chadema kwa Ajili ya kumpindua mwenyekiti wake Mbowe na Katibu mkuu Slaa.
#ZITTO vs ACT WAZALENDO
mpaka sasa zitto amekimbiwa na Mwenyekiti wake taifa Anna Mwigira ambaye sasa yupo CCm na ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mpaka sasa zitto ameshakimbiwa na katibu mkuu wake bw Samson Mwigamba kwa sasa yupo CCM.
Mpaka sasa Zitto ameshakimbia na Mwanasheria wake wa Chama bw: Albert Msando naye yupo CCM.
Mpaka sasa zitto Ameshakimbiwa na Mshauri mkuu wa Chama mh Prof kitila mkumbo yupo CCM na ni katibu mkuu wizara ya Maji.
Huwa nakumbuka maneno ya Afande Sele kwamba Aidha ACT hatueleweki au Hatujielewi.
Wakati wa kampeni Act kilijikita kushambulia Vyama vya Upinzani.
Mpaka sasa Act Haieleweki, Zitto pia Haeleweki.
#ZITTO vs KOROSHO:
1)alianza kwenye Export levy alijiaminisha kuwa anawaunga mkono wakulima wa korosho pamoja na Wabunge wao juu ya Mapambano ya kupinga Fedha zao Bilioni 201 Kudhulumiwa na Serikali.
2)Alipanga kufanya Maandamano ya Wabunge wa kusini na Wakulima wa zao la korosho yaliyopangwa kufanyika Juni 30, 2018.
3)Alipinga Mabadiliko ya sheria ya Korosho yaliyoletwa na serikali Bungeni.
4)Alihimiza Serikali kununua korosho za Wakulima, Baada ya Rais magufuli kununua korosho ghafi kwa 3300 Alijipanga Bungeni kumpinga kama Ataleta mswada wa kununua korosho Bungeni.
Hapa ndio maana nashindwa kumuelewa Zitto na ni Mrundi au ni Mtanzania?
Zitto ni Mtu hatari sana, hafai na ni mla Rushwa mkubwa Mno huku akiwalaghai wakulima wa korosho kuwa ni Mzalendo,
Ni Mzalendo gani Anamiliki Hummer?
Ni Mzalendo gani Anamiliki Ghorofa?
Unapoona Zitto Anapiga Kelele ujue kuna Sehemu Maslahi yake yameminywa na sio ya wananchi.
Hili tumeligundua baada ya Shamba lake la Ekari 4 za korosho kuchomwa moto na Wananchi wenye Hasira kali