Kwanini wazungu husaidia haraka kwenye majanga?

Wote naona tunajilaumu zaidi sisi watu weuis hatuna utaratibu wa kuchangia maafa, kwanza tukubali wengi wetu ni masikini esp walioko vijijini. Mlo wa mchana ni taabu je wa jioni? na kama mtu anaishi kwa mlo 1 kwa siku ambao ni substandard huyu mtu atakuwa na moyo wa kusaidia?

Mazingira vilevile-umekuwa katika jamii ambayo mtu akikusaidia mpaka aakikkishe media imemcover kuanzia mguuni mpaka kichwani ili saa 2 usiku jamii imuone na apate umaarufu ili awe kiongozi au kwa sababu nyingine azijuazo je huyu mtu atakuwa na moyo wa kuchangia?

Kwa upande wa serikali mbona tumetoa mchango juzi juzi tu wa $200,000.00 kwa nchi ya Zimbabwe wakati huko Karatu watu wanakufa na maafuriko si msaada huu au nyie mnauitaje?

Kwa Watu weupe mliowamiminia sifa- Kwa nini wao wanasubiri majanga tu ndio wasaidie esp. vita utaona UNHCR wanakimbilia kuuza tents na vifaa vingine kwa refugees? bila kusahau na msaada wa silaha kwa upande wanauona unaweza treet maslah yao. Kwa nini huko Haiti hawakusaidiwa siku zote kumaliza matatizo ya umasikini na imani za kishirikina(vodooism).
 
Kutoa ni moyo si utajiri..wahenga walinena

Nafikiri tumewafundisha watu wetu kusaidiwa na si kusaidia...(mistake)

Source ni ujamaa wa nyerere na kawawa kwamba serikali itakusaidia huduma, itawasaidia waathirika na si mwananchi atajisaidia, na atasaidia na wengine kwa moyo wake wote

Mindset for 26 years of ujamaa na fikra sahihi, kizazi kimeharibika vibaya..tujitahidi kuwaelemisha watoto wetu waondokane na mindset ovu.
Siasa zile zilikuwa za ujamaa na kujitegemea. Zilikuwa zina aina mbili ya approach. Serikali ilikuwa itoe huduma muhimu za kijamii wakati wananchi wajishughulishe katika kuhakikisha wanazalisha mali. Sioni ubaya katika lile.
Ubaya nauona katika ubinafsi mkubwa tuliouanza baada ya kudharau ujamaa. Siku hizi tunaweza kuwa tunakaa mtaa mmoja na ni majirani bila hata kujuana wala kujuliana hali.Wakati ule wa ujamaa na kujitegema hali ilikuwa hivyo kweli?
Ubinafsi huu tulionao sio product ya Nyerere na Kawawa! Huu ni wa kwetu.
Tuubadili mfumo wa fikra na kuwaacha wafu wawazike wafu wenzao maana kama bado tatizo linalotusumbua sasa tunaona ni la marehemu, basi we have not subjected our minds to accept changes.
 
Source ni ujamaa wa nyerere na kawawa kwamba serikali itakusaidia huduma, itawasaidia waathirika na si mwananchi atajisaidia, na atasaidia na wengine kwa moyo wake wote

Mindset for 26 years of ujamaa na fikra sahihi, kizazi kimeharibika vibaya..tujitahidi kuwaelemisha watoto wetu waondokane na mindset ovu.

Si kweli ingekuwa ni nyerere, kawawa na ujamaa basi tungekuwa tunajali zaidi kuliko nchi za west ambazo ni za kibepari, ujamaa haukutaka hata mtu mmoja awe tajiri kuzidi wengine! kila kitu kilikuwa cha wote.
Kuendelea kuwalaumu wazee hawa ni kuonyesha kiwango cha hali ya juu cha ukomo wa uwezo wetu wa kufikiri. Tuikatae hali hii. Let us use our history to make a better future!!!!!
Tatizo sisi siyo watoaji na ndiyo maana hata kwa viwango binafsi hatubarikiwi.
 
Watanzania na Waafrika kwa ujumla wao wanapenda kuchangia pale ambapo kuna mnufaiko wa namna fulani utakaotokana na mchango atakaotoa. Manufaa hayo yapo ya aina nyingi kutegemea na anayechangiwa
 
Watanzania na Waafrika kwa ujumla wao wanapenda kuchangia pale ambapo kuna mnufaiko wa namna fulani utakaotokana na mchango atakaotoa. Manufaa hayo yapo ya aina nyingi kutegemea na anayechangiwa

wildcard.. tunaweza kusema that is the bottom line.. mtu anajiuliza "what is in there for me? "...
 
1. Sense of entitlement. Tunaamini sisi ni watu wa kusaidiwa tu.
2. Hatutoi kwa asiyetuhusu. Tuko tayari kulala kwenye sakafu siku saba kwenye msiba wa mwenzetu;Kukaa usiku kucha nyuma ya pick-up, kwenye barabara mbovu, kumpeleka marehemu kijijini kwao;kuchimba kaburi na kutoa pesa kwa ajili ya kuwapoza wafiwa lakini hatuko tayari kutumia nusu saa kusafisha barabara iliyokuwa mbele yetu!

Amandla.....
 
Kwakweli tumekuwa masikini kwa sababu ya ubinafsi, tuwabinafsi sana, wazungu wananistaajabisha hasa wamarekani, i see hawa jama wapo makini ktk kusaidia, unajuwa mim naweza sema ni j.k nyerere tu alikuwa na moyo wakusaidia nakujitoa kwa mataifa mengine, huwez amin nimeamka asubuh nakusema if ningekuwa rais wa nchi hii ningeistaajabisha dunia kwakutoa kikos cha watu mia moja ktk jesh letu, chenye timu ya waokoaji, madaktari, mafundi, na wa taalam wa ujenzi, nina kiu taifa hili kuwa taifa kubwa na hili ni lazima litimie, watanzania tubadilike nakuwa watoaji ktk maswala ya msingi.
 
Kwa wote wanaotaka kufanikiwa ni lazima uwe na principle hii ya Utoaji.
Anayetoa ndiye anayepokea.Wazungu wengi kwa sasa hawamuamini Mungu lakini ni watoaji sasa tena bila unafiki wa kutaka kujulikana.
 
sisi waafrika tunachangia sana tu. kuna mtoto wa kaka yako anataka ada ya shule unachangia, shangazi yako mgonjwa anatakiwa kwenda india unachangia, usisahau mchango wa harusi wa besti yako, shule ya mwanao wanahitaji madawati unachangia, kuna mchango wa mwenge, zahanati inajengwa jirani unachangia, mtoto wa dada yako kapata shule ya day inabidi akae kwako unachangia, yule jamaa anaziba mashimo barabarani unachangia, kazini bosi kafiwa na babae unachangia, timu ya soka ya yoso mtaani wanahitaji jezi mpya unachangia, mlemavu amekaa kwenye kona ya ngazi unasaidia, kanisani sadaka ni raundi tatu au nne, uko baa meza ya jirani unawafahamu unawapa raundi...

sasa hili la kilosa, tena unaliona kwenye tv, hamna unayemfahamu, unajisechi huna kitu mfukoni, inabidi uminye tu!
 


Hillary Clinton cancels Australia visit


Emma Chalmers
January 14, 2010 09:12am


US Secretary of State Hillary Clinton has cancelled her weekend visit to Australia in the aftermath of the devastating earthquake in Haiti.
Her husband, former US President Bill Clinton, is the UN's special envoy to Haiti and is helping to coordinate relief efforts.

The couple reportedly spent their honeymoon in the Caribbean nation and have spoken of their fondness for the country.

The Federal Government this morning confirmed the AUSMIN meeting scheduled to take place next week has been postponed due to the devastation in Haiti.

A spokeswoman for the Department of Foreign Affairs and Trade said the talks will be rescheduled "at the next convenient opportunity''.

Secretary Clinton was due to meet with Prime Minister Kevin Rudd in Canberra on Sunday and with Minister for Foreign Affairs Stephen Smith and Defence Minister John Faulkner on Monday.

Mr Smith is due to give a press conference this morning to outline Australia's response to the earthquake, which has prompted an international aid effort
 
ni jukumu la kila concerned human being kusaidia panapoitajika ila pia msaada unatakiwa uendane na kuhakikisha jamii husika inajiandaa vema kukabiliana na tatizo kama ilo litapojitokeza siku za baadae.
katika kuhakikisha tatizo linatatuliwa ipasavyo inabidi ujue chanzo cha tatizo ili utibu kwenye mzizi, ukiangalia kwa umakini nchi zote zinazoizinguka marekani, typhoons, torrential rains, earhtquakes, strong winds, storms etc are very common na ukifuatilia chanzo cha mabalaa yote hayo ni uharibifu wa mazingira wa viwanda, je haiti na chi zinazoizunguka marekani zina viwanda vya kuchafua mazingira?
mabalaa wanayoyapata yaliwafaidisha mwanzoni? kwa iyo msaada wanayotoa wamarekani ni kidogo sana kulinganisha na mabalaa walioyasababisha wala siwapongezi!
si ni marekani haohao waliowashauri haiti waingie kwenye ubepari? angalia umasikini uliopo haiti haujawai onekana popote duniani hadi wanakula udongo, ili ni fundisho kwa nchi masikini tulioanza ubepari miaka ya karibuni, haiti walianza ubepari miaka ya 50, angalia walipo, na pia tujiulize tofauti kubwa kati ya cuba na haiti, nchi zote kwa pamoja cuba ikaanza ujamaa na haiti ikaanza ubepari, chambueni wenyewe!
 
Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.
 
Mwanakijiji
 
Aksante sana kwa swali hili, kwanza kabisa sio kweli kwamba wenzetu wako mstari wa mbele ki hivyo. Wenzetu kwa mfano UK ni nafsi ambazo zinawasuta, wakati wao wanapata kila kitu kutokana na system yao jinsi inavyofanya kazi. Na kwa viongozi ni zaidi kuona aibu jinsi wanavyowadhulumu nchi za dunia ya tatu katika price fixing nk. Na wao kutambua fika kwamba bila hawa masikini hawawezi kufaidi keki.

Kwa vipi? Ukiwa raia wa UK au una kibali ya kuishi UK bila mikwaruzo una uhuru wa kulipwa pesa za nyumba na chakula kama huna kazi. (Unapata fedha ya kutosha kwa mahitaji ya lazima kwa binadamu). Hiyo ni pamoja na Serikali ya UK kuona kwamba inapata mazao kutoka popote ulimwenguni kwa bei ambayo ni nafuu kwa raia wao. Wanawezaje kufanya hilo - ni kwa kukusanya kodi katika kila secta na kuitumia inavyotakikana. Kuwa na mtandao madhubuti wa kuzulumu nchi za dunia ya tatu hususan wakiwapata viongozi kama JK et al.

Sisi Tanzania kama huna kazi ni shauri yako hakuna cha serikali ya Chama Cha Majambazi kuangalia unapata vipi mahitaji ya lazima kwa binadamu - utajijua mwenyewe.

Charity shops zipo kila kona kwa volunteers kwenda kufanya kazi bure sasa sidhani kama Tanzania utaweza kupata watu wa kufanya kazi bure wakati hawajui jioni watakula nini? Kila kitu ambacho huhitaji au hutakitumia tena unaweza kuweka kwenye haya maduka na wao kuhifadhi na kupeleka popote ulimwenguni ambako kuna shida madhalani nguo, vitabu nk. Mfano mdogo ni vitabu vya hadithi nk ambavyo vinauzwa kwa £5 hadi £10. Kwa mwaka mtu unaweza kusoma vitabu 1000 na baada ya hapo huna haja navyo kwa hiyo anavipeleka kwenye charity shop. Unaweza kuona uwezo wa wenzetu kununua vitu vipya bila mkwara wowote kwa sababu serikali imehakikisha kwanza malipo ni ya halali kwa professionals na wafanyakazi wa kawaida i.e Engineers wanalipwa kati ya £20 hadi £150 kwa saa inategemea upo kwenye field gani, Walimu wakuu wa shule za msingi kwa mwaka wanalipwa wastani wa £70,000.00 nk. Hizo ni pesa ambazo zinamuwezesha kuishi maisha ya kawaida kabisa na kuwa na Holiday kila mwaka popote pale ulimwenguni.

Tanzania sidhani kama serikali inaona kama kuna haja ya kuwalipa wafanyakazi malipo halali. Bali ni kwa wabunge, mawaziri na wakuu wa mashirika ya serikali pia kwa wale wanaojiita ma-expatriate kama Maximo nk. Tanzania huwezi kuishi maisha ya kawaida kwa kutegemea mshahara wa serikalini au shirika la umma. Kazi zinazotafutwa kwa udi na uvumba BOT, TRA, nk. magendo ni kitu cha kawaida na hakuna anayejali ethics za kazi. Kama wewe sio mfanyi biashara au hupati kitu kidogo basi ni masikini wa kutupwa.

Tatizo lipo kwa serikali ya Chama Cha Majambazi ambayo imejikita kwenye wimbi la kukumbatia mafisadi na kufikiri wao ndio suluhisho la matatizo yetu. NO

Tanzania inatakiwa kuwa na wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma wachache ambao wanalipwa vizuri kuweza kumudu maisha yao na kukumbatia technologia ya computer na kuweka kipau mbele kwenye ajira katika kila sekta na kuona kwamba wakulima wanalipwa vizuri kutokana na kazi zao na kuhakikisha njia za uchumi yaani barabara na reli zipo katika karne ya 21, kuhakikisha hakuna mazao yanayooza vijijini. Kuwa more creative katika kupanua soko la bidhaa za Tanzania kuanzia mananasi yanayoza Chalinze na machungwa yanayooza Lushoto (mfano) nk.

Kuangalia jinsi ambavyo Watanzania wanavyoweza kuuza bidhaa zao sio Kenya tu na nchi jirani bali South Amerika Japan, Europe, North Amerika nk. Hatuwezi kuendelea kwa kukumbatia masikini wenzetu wa nchi jirani na kufikiria wao watatuwezesha. Tutaweza kujiwezesha sisi wenyewe kwa kufanya kazi na kutumia rasilimali zetu kwa asilimia 100. Gas, madini, utalii ni vitu tosha kabisa ambavyo vinaweza kutuondoa kwenye umasikini, tuanze kufikiria jinsi ya kutumia gas majumbani mwetu kwa kupikia nk. Vile vile kuisafirisha hadi Europe ambako wana shida ya hii mali ghafi.
 
Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!
Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!
 
Kama nilivyoeleza hapo juu utaona tayari wako kwenye gia nyingine charity shops kila kona, wao wapo tayari 24/7 kuwakumbusha wenzao kwamba kimetokea hiki tunaomba ushiriki wako. Tanzania hakuna hivyo na haiwezekani viwepo kwa sababu ya umasikini wa viongozi wetu kuwadhulumu raia kwa malipo duni nk. wakati wanakusanya kodi ya kutosha lakini wanakwenda ulaya kufanya shopping za nguvu kwa wake zao nk.
 
Hata hivyo bado Watanzania ni wakarimu pamoja na maisha yao kuwa magumu waliweza kuwasaidia Southern African contries kupata uhuru wao itakuwa sembuse maafa ya hapa na pale. Uvundo na uozo tuliojichagulia ndio tatizo na tukiweza kuusafisha na kuweka vipau mbele vyetu vema karne ya 22 itapiga hodi bongo. Tupo wengi tu weusi mbona tunatoa hata wewe umetoa, unakumbuka wakti unasoma Tanzania uliweza kuchangia ukombozi wakati ule hukuwa tajiri wewe au mimi sikuwa tajiri.

Mwanakijiji usichanganyikiwe bado sana tunakuhitaji na tupo wengi ambao tunataka kuona Tanzania yenye neema lakini ndugu zetu wa Chama Cha Majambazi wameamua kula sahani moja na kuwakaribisha kwenye hazina yetu akina RA, Sin bin Clair na mafisadi papa ambao wananyonya damu ya walipa kodi wa Tanzania.
 
Aksante sana kwa swali hili, kwanza kabisa sio kweli kwamba wenzetu wako mstari wa mbele ki hivyo.
Ni kweli wako mstari wa mbele na mifano iko mmoja baada ya mwingine. Rejea Tsunami na majanga mengine yaliyopita.
Wenzetu kwa mfano UK ni nafsi ambazo zinawasuta, wakati wao wanapata kila kitu kutokana na system yao jinsi inavyofanya kazi.
Nafsi zinawasuta kivipi? Na kwani sisi hatuna nafsi? Pengine hatuna maana tulikaa tukawaachia WaRwanda waune mmoja mmoja hadi kufikia milioni.
Na kwa viongozi ni zaidi kuona aibu jinsi wanavyowadhulumu nchi za dunia ya tatu katika price fixing nk. Na wao kutambua fika kwamba bila hawa masikini hawawezi kufaidi keki.
Hii ni victim mentality ambayo naipinga. Mtu unapodhulumiwa na unajua na kutambua kuwa unadhulumiwa lakini unaacha hiyo dhuluma iendelee, basi wewe ni mtu mwenye matatizo ya asili na unastahili kudhulumiwa hadi siku yako ya kufa.
 
Ni kweli wako mstari wa mbele na mifano iko mmoja baada ya mwingine. Rejea Tsunami na majanga mengine yaliyopita.

Nafsi zinawasuta kivipi? Na kwani sisi hatuna nafsi? Pengine hatuna maana tulikaa tukawaachia WaRwanda waune mmoja mmoja hadi kufikia milioni.

Hii ni victim mentality ambayo naipinga. Mtu unapodhulumiwa na unajua na kutambua kuwa unadhulumiwa lakini unaacha hiyo dhuluma iendelee, basi wewe ni mtu mwenye matatizo ya asili na unastahili kudhulumiwa hadi siku yako ya kufa.

Hapa nafikiri tuko level tofauti sifahamu nikusaidie vipi.
 
Back
Top Bottom