Kwanini wazungu husaidia haraka kwenye majanga?

Ndugu yangu Mwanakijiji hii ni bongo bwana hatuaminiani wachangishaji wenyewe ndoo hao hao, nasikia watu wamejenga kwa misaada ya mabomu ya Mabagala, kile kitengo cha maafa kilicho chini ya PM wakipokea misaada 10% ndiyo inaenda kwa walengwa 90% hujui inakwenda wapi utakuwa na moyo tena wa kuendelea kutoa.

Umesema hapo ulipo watu wameanza kutoa misaada pamoja na nguo sasa ni tofauti na huku bongo leo nikitoa shati uwapelekee walengwa kesho yake nakuona wewe tena umelivaa ni kazi kweli kweli bongo.

Umenena Luteni. Hapo ndiyo kwenye mzizi.
 
Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!
Na mimi nimejiuliza sana nilisikia BBC nchi zikitajwa kama Marekani,canada,uingereza,ufaransa,china cha ajabu sikusikia hata nchi moja ya AFRICA nimejiuliza ila sina majibu.
 
kuna implication kubwa sana hata maisha ya kawaida wale wote ambao ni watoaji Mungu anawabariki sana ndio maana hata sisi tunachukua Michanga yetu ya dhahabu na kuwapelekea wao matani na matani ya mchango. Sasa kama sisi tunashindwa kusaidia hata kufundisha uchawi yaani haya ni matatizo makubwa sana. Wataendelea kubarikiwa na sisi kubaki maskini maana wao ni watoaji wakubwa
 
Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!

Wanajikosha kutokana na aibu ya wazungu kupingwa na jemedari mweusi miaka hiyo ya 1797, ni kweli jemedari mweusi aliyetokana na uzao wa kitumwa aliwashinda kivita mataifa makubwa ya enzi hizo Uingereza, Ufaransa na Hispania. Jemedari huyo ni Toussain L'ouveture na kujitangaza kama gavana jenerali wa Haiti na baadaye kutangaza uhuru mwaka 1804.

Kipigo hicho walichopata wazungu na hasahasa wafaransa kilisababisha mapinduzi huko France ya kuungoa ufalme wa France. Toka kipindi hicho nchi za ulaya zikala njama kuiwekea vikwazo, mikwala n.k nchi hiyo ya Haiti isiendelee kwa vile ni 'aibu' kupingwa na mweusi na itakuwa aibu kuiruhusu iendelee kiuchumi n.k Mfano Marekani ya kipindi hicho cha 1790 -1890 haikuwa nchi ya kibeberu, maana nayo ilitoka kuwatimua wakoloni wa Kiingereza huko USA, hivyo walikuwa na hamu ya kuwa na uhusiano na mwanamapinduzi mwenzao wa Haiti.

Lakini nchi za Ufaransa, Uingereza, Hispania zilihakikisha kitu hicho hakitokei, na sasa wanatoa coverage kubwa kujaribu kuonyesha kuwa mtu mweusi hawezi kufanikiwa katu, hasahasa kama ametoa kipigo kwa mabeberu.

Hivyo Hii kutoa misaada kwa kelele na mbwembwe nyingi ni mwendelezo wa mataifa beberu kukumbusha kuwa eti bila wao mataifa yasiyo ya kizungu kamwe hayawezi kufanikiwa. Tizama Venuzuela, Cuba n.k nchi zinazojitutumua zinavyopigwa vita na nchi beberu.

Pia hiyo ni njia ya kuzuia nchi zingine zenye mtazamo tofauti na nchi za kibeberu za ulaya/USA(nao walibadilika kuwa mabeberu toka 1945) kujipenyeza hapo Haiti. Nchi hizo zaweza kuwa Cuba, Venuzuela, Urusi n.k

Kwa hiyo hapo ni game-of-chance au chezo la chess mabeberu wanaweza 'kingi' kwa mgongo wa msaada wa maafa.

Hii ci
 
Nimetafakari sana hii maada, ikanifanya nianze kufanya assignment ya kwa nini tuko kama ambavyo MKJJ anasema

1. Geographic position

Tanzania and many other african countries are situated in very favourably geographic position(climate) that, issues like major disaster are rare to happen or experienced by majority.

Hatuna shida kubwa zilizowahi kutokea zikaacha historia na makovu ya kudumu, hivyo vizazi vikapata kusimuliwa na wengine kushuhudia kwa macho, mathalani kijana wa Haiti sasa hivi akiwa mzee na ikatokea same problem, ni rahisi kusaidia kwa sababu alishaathirika mwanzoni.

2. Basic needs

Kutokana na sababu ya hapo juu, I can excerpt one aspect for further clarification. People call/consider us as we are poor, and in one way or another we all have passed through this poverty life or we have seen through other people.

wengi tumetoka na kukulia vijijini, na kamwe hatukujua kuwa tunaishi maisha ya dhiki mpaka tulipopata mwanga wa dunia nyingine. kwa walio vijijini wanaona maisha wanayoishi ni haki na halali. walio mjini tena wengi waliopitia the same life wanaona kuwa walio vjijini wanaweza kabisa ku-win maisha kama waliyopitia wao, hapa tumeweka concept ya self-struggling. Hii inatufanya , tusisaidie vijana maskini, mayatima, wenye shida mbalimbali; itakuwa kichekesho kama hawa watu watajitokeza kusaidia watu wanaokumbwa na maafa.

3. Ukarimu

This may sound weird; ukarimu wa watanzania una kikomo, na huu ukarimu unatokana uko kwa watu wachache wanaowameza wale wengi wasio na ukarimu. Kwa sababu ya sifa ya kuwa watanzania ni wakarimu na wana upendo. tumeweka akilini that may be a next door neighbor will act on some issues. Kuna dhana ya kutegeana, ya kuwa 'watasaidiwa' tu, hii dhana ya kuwa fulani atafanya, ndio imekuwa ina matatizo hata katika vitu personal some people demand that someone/government/leaders will do this for me.

4. Ubinafsi/kushindana/ showy life

Kuna mtu mmoja namfahamu, hakosia kusema yeye ana PhD, wala hakosi kutamba yeye ana uwezo sana. nimeona watu wakiishi maisha yasiyo yao, hayaendani kabisa na status yao. ni na rafiki ambaye alinunua gari na hakuwa na pesa ya kuliendeshea! story may go on, and on and on...

Nimesema hapo juu kuwa wengi wametoka kwenye maisha ya dhiki na maisha ambayo mtu hakujua kuwa kuna siku ataenda chuo kikuu na kuwa meneja.,in other words our successfulness in our life is beinge intepreted as lucky/ accident.. majority are not thinking that you can be success by being hardworker,innovative and mjasiriamali... sasa fikiria mtu aliyetoka kijijini kwetu leo kwa 'bahati' anajiona mkurugenzi, wengi upata 'kichaa' cha maisha. Sasa kwa sababu jamii yetu tumeshaweka concept za kushindana, kujionyesha n.k We will try our level best to maintain our status and even being more than that ili nifanane na waziri mkuu

Showy life inakuja katika jamii inayowaza sana wengine wanawaonaje, na ni dalili ya jamii yenye gossip,majungu, unafiki, uongo na hizi ni dalili za kutokuwa na 'business ya kufanya' -idle, lazy, sloppy, maana wanasema nini?

si fulani kanunua benzi?

how? ,

ameiba pesa,

ahaa..acha na mimi nikaibe..

Mtoto aliyezaliwa familia tajiri, hatashtuka kwenda chuo kikuu, hatashtuka kupanda gari nzuri, hatashtuka kwa mafanikio yoyote, yaani alijua tangu awali kuwa atakuwa navyo.

sasa mtu amweka bajeti ake ya kununua simu ya laki tano ashindane na sofia simba, ukimwambia kuna mchango wa mafuriko ataanzia wapi kutoa?

5. Utoaji

Ukiacha dhana zote hapo juu swala a utoaji ni natural; halitegemei ni tajiri au maskini. wenzetu wazungu wamefanikiwa sana swala la ku-value the human life. This concept of theirs, made them to succeed, their leaders thinks about society and how to help people.

Kuna vipindi huwa sitaki kuanagalia siku hizi huwa vinanitoa machozi, kuna watoto mayatima Iringa, na sehemu zinginezo wanaonyeshwa maisha yao na magumu wanayopitia, wapi? TAnzania? how they reached their? watu(wazeungu wanatoa misaada kuchangia ndugu zetu walioko TANZANIA, wapate chakula, maji, waende shule! wanatoa misaada watu walio MAELFU YA MILE kutoka Tanzania wanajua ndugu zaetu wanaishi vipi, wanalia, wanatoa michango, wakati tulio Tanzania, tunawaza kwenda beach na familia zetu!

Blessing from bible point of view inakuja kwa watoaji, na hii in other words is a divine principle, haijalishi umeokoka kama mimi , mchungaji au mwislamu

'' ukitoa unapokea' this is supenatural law ya Mungu, hata kama hauamini Mungu!! mwangalie Bakhresa anavyotoa misaada, anagalia ana make sh. ngapi!

So hata umaskini wetu nao ni kwa sababu hatutoi! I like to prteach this very word to christians, na uishia kukasirika

6. Makanisa

There are so many challenges facing churches and other religions right now, one being the participation of these churches to help mankind , not spiritually only even materially.

Nimeona na nimshuhudia makanisa kadhaa ya kikristo ambayo mchnguji wa kanisa ana gunia la mchele, wakati kuna muumini analala na njaa!

I have seen by my naked eyes, kuna waumini wanajipendekeza kwa wachungaji na kutoa mali nyingi, sadaka kubwa kubwa, hali wakijua kuwa kuna watu in the very same churches wanalala njaa!

So if these things happening in churches? nje ya hapo tunategemea nini??

Kweli yapo makanisa na wachungaji wanatoa sana na wanasaidia mno, lakini ni wachache kulinganisha na majority ya hizo dini zao!

so what is these religions for?, if we can not practise what is written and what we believe, I doubt if these very same people wanaweza kuchangia wanaopata maafa!

I submit
 
Mwanakijiji,
Tafadhali hebu tuwe genuine kwa hili:
3. Pamoja ya kuwa kutoa si utajiri sawa kabisa, tukirudi kwenye grassroot, kule kwenye mila zetu, bado hadi leo tunasaidiana. Ila tu huu mchanganyiko wa mila na mila na dini na dini sasa hivi kweli hatujui culture yetu ipo wapi na wengi wameshpoteza hata culture zao, na kujiita vingine, kama wakristu,waislam, wapagani nk. Hiyo ndiyo kweli victimization ya culture zetu baada ya ile partition ya Africa. Mipaka haikujali culture.

Sidhani kama hii ni kweli. Inapotokea michango wa harusi pale dar, utashangaa kuwa wachangiaji wanatoka sehemu zote za Tanzania. Nilishudia harusi moja ya ndugu yangu tukapokea michango kutoka kwa akina Mapunda, Rugemalila, Shekimweli, Mwakatumbula, Ole Saibul, Mrema, Shayo, Msuya, n.k

Wakuu mmeongea hoja nzuri sana....

Watanzania tuna moyo wa kusaidiana sana. Angalia kwenye Grassroots...jirani na jirani, tunasidiana mpaka tunapitiliza...(tunaposaidiana mpaka chumvi na njiti za kiberiti)..ila majanga kama haya yanahitaji LEADERSHIP yenye sura ya Kitaifa kuhimiza na kusimamia utekelezaji wake.

Kukiwa na Leadership ni rahisi sana kuboresha kile ambacho tayari kipo kwenye Grassroots. Mfano: Jeshi likiwa na Solders wenye mafunzo wa hali ya Juu kuliko jeshi lolote Duniani, likikosa Leadership nzuri ni sawa na bure.
 
I'm really proud of those Tanzanians who waited not to come to the assistance of their fellow Tanzanians. I'm humbled and totally awed by your contributions and help in the hour of their needs. You have raised to the occasion and seized the moment! It just give me an idea of what kind of change we need.

As I have said several times now, change is not something we hope for or pray for; change is something we bring. This is just the beginning.

Mwaka huu tutatoka kwenye kulalamika na kuhamasika kifikra, tunataka tutende. Tumejaribu katika suala hili la majanga and I hope in the near future we will show leadership in something more substantial and transformational. We are putting those in power on notice; change or you will be changed!

Thanks a million for you kind heart.. we are not different from wazungu after all!!
 
Hapa unagonga msumari unapotakiwa. Marehemu Samora Machel RIP alikuwa anasema Aluta Continua.
 
Kutoa ni moyo si utajiri..wahenga walinena

Nafikiri tumewafundisha watu wetu kusaidiwa na si kusaidia...(mistake)

Source ni ujamaa wa nyerere na kawawa kwamba serikali itakusaidia huduma, itawasaidia waathirika na si mwananchi atajisaidia, na atasaidia na wengine kwa moyo wake wote

Mindset for 26 years of ujamaa na fikra sahihi, kizazi kimeharibika vibaya..tujitahidi kuwaelemisha watoto wetu waondokane na mindset ovu.

Unalaumu ujamaa. Waulize jirani zetu Kenya na ubepari wao ikiwa wanasaidiana kuliko sisi.
 
Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!?

Mwanakijiji labda unasahau tabia yetu ya kukimbilia kwenye ajali - mara nyingi si kuwasadia wahanga bali kuwaibia. Nimeshuhudia kwa macho yangu maiti akivuliwa saa baada ya ajali. Ndivyo tulivyo - tuna roho za korosho

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!

Jana nimemshuhudia Raisi wa Haiti akihojiwa na CNN - loo karibu nitoe machozi pale alipoulizwa atalala wapi usiku kwani ikulu na nyumba yake binafsi, zote zimeporomoka. Alipojibu akisema hajui atakwenda wapi, nikakumbuka nchi yangu ya Bongo - huyu ni Kiongozi wa nchi aliyeapa kuwa atailinda nchi yake na wananchi wake lakini sasa anashuhudia nchi yake ikiteketea asijue afanye nini. Sana sana anakaa kama mtazamaji huku mataifa mengine yakifanya jitihada za kuwasaidia na kuwaokoa watu wake.

Hivi sasa nchi yetu nayo inateketea kwa ufisadi lakini Raisi wetu aliyeapa kuboresha maisha ya wananchi kabaki tu kama mtazamaji - hivi naye anasubiri Marekani na Japan waje wawaokoe Watanzania katika janga hili ? Halafu eti tuna jeuri ya kuwakemea mabalozi wa nchi zilizoendela na tajiri kuwa wasiinglie mambo yetu. Yanikumbusha ya MV Bukoba serikali ya Tanzania chini ya Raisi Benjamin Mkapa ilipokataa msaada wa Uingereza na Marekani na matokeo yake tulipoteza maisha ya watu karibu elfu moja.
Kweli Bongo tambarare.
 
Celebs who are reaching outBrad Pitt and Angelina Jolie: Donated $1 million to Doctors Without Borders
Ben Stiller: Redirecting donations from his stillerstrong.org to emergency relief efforts
Madonna: Donating $250,000 to to Partners In Health
Wyclef Jean: Helping his Haitian charity Yele raise funds
George Clooney: Pairing with MTV to stage telethon for earthquake relief
Lance Armstrong: His LiveStrong foundation pledged $250,000 to relief charities
Eddie Izzard: Donated to the Haiti earthquake fund via Care.org
Coldplay: Donated to Oxfam.org
Hollywood Foreign Press Association: Donated $100,000 to Yele
Gisele Bundchen: Donated $1.5 million to the Red Cross
Alyssa Milano: Donated $50,000 to UNICEF
Sandra Bullock: Donated $1 million to Doctors Without Borders
Tyler Perry: Donated $250,000 via his foundation
 
Wako wapi wale wanaochangia milion 400 kwa mkutano wa ccm? Wafadhili wetu wa simba na yanga? Yuko wapi Mengi na wapiganaji? Yupo wapi mzee Ndesa?
 
Unalaumu ujamaa. Waulize jirani zetu Kenya na ubepari wao ikiwa wanasaidiana kuliko sisi.

Wenzangu mnisadie! Niliishi TZ miaka ya 80 na mwanzo wa 90, halafu Kenya. Niliona kweli tofauti moja:
Nairobi nilikuta vijana wengi kiasi waliojitolea kusaidia mipango mablimbali kama "mavolunteer". Yaani walijitolea kwa muda na kazi kusomesha watoto walemavu, watoto kwenye mitaa ya vibanda, kusafisha mazingira, kupanda miti na kadhalika. TZ sikuiishi Dar lakini mikoani ila tu rohi hii nilikuta kanisani tu siyo nje. (na hii iko Kenya pia!)

Sasa sijui kama ni wakati (labda roho hii imeshafikia TZ baadaye pia?) au utamaduni wa mji mkubwa pamoja na elimu ?

Sidhani ya kwamba ni swali la bepari au ujamaa...
 
Back
Top Bottom