Kwanini wazungu husaidia haraka kwenye majanga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wazungu husaidia haraka kwenye majanga?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 13, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

  Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

  Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

  Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

  Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hehehehehe..pole kwa kuhisi kuchanganyikiwa. Wengine tulishagachanganyikiwa siku nyingi tu.

  Tayari Wahispania, Waitalia, Wajerumani, Waingereza, Wamarekani na wengineo wameshaanza anza relief efforts....
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kutoa ni moyo si utajiri..wahenga walinena

  Nafikiri tumewafundisha watu wetu kusaidiwa na si kusaidia...(mistake)

  Source ni ujamaa wa nyerere na kawawa kwamba serikali itakusaidia huduma, itawasaidia waathirika na si mwananchi atajisaidia, na atasaidia na wengine kwa moyo wake wote

  Mindset for 26 years of ujamaa na fikra sahihi, kizazi kimeharibika vibaya..tujitahidi kuwaelemisha watoto wetu waondokane na mindset ovu.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Duuuh yaani watu hamkosi kitu cha kumlaumu Nyerere...
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........Utoaji ni roho ya mtu, ila hawa watu weupe wamejaliwa sana hii roho ya utoaji.
  Sisi weusi wapo wenye roho hii pia ila ni wachache, wengi wao hadi wasukumwe ndio watoe.
  Kutoa ni roho sio utajiri.
   
 6. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo waafrica wote walikuwa wametawaliwa na Nyerere na kuongozwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea!. Kazi kweli kweli.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Unajua Mkuu mwanakijiji kuna kitu kingine nimekinotice, utakuta News channel TV karibu zote katika siku ya jana zinatoa updates ya nini kinaendelea Haiti at least in every 30mins. Hizi si TV za serikali ati........ Sasa njoo kwetu TV tena ya serikali habari za maafa tena nchini mwetu mnapewa wakati wa taarifa ya habari tu, tena inaweza hata isiwe ya kwanza..............

  Sasa tujiulize inakuwaje TV za Marekani tena binafsi zinasuspend hata vile vipindi muhimu kuripoti maafa tena ya nchi nyingine???

  "I AM INCLINED TO BELIEVE WE DON'T VALUE A HUMAN LIFE"
   
 8. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chuki yako dhidi ya Nyerere (RIP) itakufanya uweuke sasa, kwani Nyerere alitawala Afrika nzima?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  siwezi kushangaa kuna Watanzania wamekaa na kusikitika kuona janga la Haiti na wako tayari kutoa msaada kule wakiitwa!
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Anavuna alichopanda, oh wala siwehuki..chochote nakunywa kahawa kama kawaida.

  Ndio faida ya kuweka misingi mibovu inakufuata popote.
   
 11. G.MWAKASEGE

  G.MWAKASEGE Senior Member

  #11
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi sishangai maisha ya watz wengi ni maafa tuu thus mtu akiona ivyo anatake easy tofauti na wenzetu maisha yao ni shavu kwa kwenda mbele.
  Above all kutoa ni moyo ila uwe nacho sasa cha kutoa!
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mwanakijiji hii ni bongo bwana hatuaminiani wachangishaji wenyewe ndoo hao hao, nasikia watu wamejenga kwa misaada ya mabomu ya Mabagala, kile kitengo cha maafa kilicho chini ya PM wakipokea misaada 10% ndiyo inaenda kwa walengwa 90% hujui inakwenda wapi utakuwa na moyo tena wa kuendelea kutoa.

  Umesema hapo ulipo watu wameanza kutoa misaada pamoja na nguo sasa ni tofauti na huku bongo leo nikitoa shati uwapelekee walengwa kesho yake nakuona wewe tena umelivaa ni kazi kweli kweli bongo.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hapa bongo hakuna utaratibu mzuri wa hayo mambo lakini wenzetu wana taratibu zao wanajua majanga yapo kwahiyo huwa kuna sehemu maalumu ya kupeleka misaada muda wowote, hata mitaani utakuta kuna maboksi special kwa kutoa misaada iwe nguo viatu nk. si kusubiri majanga kifupi huwa wamejiandaa. Sisi ni tofauti chukulia mfano pale Fire Dar utakuta magari yote ya zima moto mabovu lililo afadhari lina pancha ajari ya moto ikitokea ndo wanahangaika kuziba pancha baadae ndio wakajaze maji wapi na wapi, bado safari ni ndefu ndugu yangu MMJ
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Nani anayevuna Nyerere? My Dognesssss........uwiiiiiiiiiii.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Hili ni kweli lakini hili linatokea mahali pote duniani; hata Wamarekani wanaingizana mijini lakini haiwazuii wengine kusaidia. Ndio sababu ya mimi kuamua kusaidia kupitia Red Cross ya Tanzania kuliko kupitia serikali na ndio maana nadhani watu wa serikali wanaweza wasipende sana hii kampeni.

  Basi kuna uwezekano mkubwa kuwa ni kweli tumelaaniwa!
   
 16. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mtoto akililia wembe mpe. Wamelilia madaraka wakapata baada ya kushindwa kuongoza wanatafuta wa kumlaumu. Kama umeshindwa si unajiuzulu kuongoza sio lelemama ni lazima uwe na kipaji.
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji unauliza swali kubwa halafu unategemea jibu rahisi. Hakuna jibu rahisi hapo kazi kweli kweli. Nitajibu baadaye kwa sababu binafsi sikuzoea kuandika kurasa kadhaa za majibu lakini nitajitahidi give me two days.
   
 18. M

  Mende dume Member

  #18
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wenzetu system iko organised. there is always someone taking a lead. sisi mf tz, wenzetu wako kwenye maafa kilosa. amir jesh mkuu anaandaa futari ya akina Drogba, two weeks later ndo anaagiza majeshi yake kusaidia!

  of course watu wamesha kata tamaa wanatmani nchi iuzwe yote kila mtu apewe haki yake ajijue.
   
 19. l

  lukule2009 Senior Member

  #19
  Jan 14, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Duuh kazi kweli kweli ..... kwa ukarimu ni rangi ya mtu !!! Jamani mbona unajidharau kiasi hicho??? labda wenzetu wanan uwezo na nyenzo za kusaidia je? Umaskini una limit uwezo wa mtu kutoa. na hicho wanachotoa ukilinganisha na walichonacho ni maji ndani ya tone jamani tuelewe. Ni kama Bushi kumpa Kikwete Milioni 700 za vyandarau ili khari Bail out peke yake ni Bilioni Mia saba. Hii kutoa/ama kutokutoa haina uhusiano na rangi ya nguvu jamani ... hatat sisi tunakuwa na mawazo mgandoo hivyo na tupo JF. tafadhali jamani Kaaaah!
   
 20. l

  lukule2009 Senior Member

  #20
  Jan 14, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Kila kitu wanachofanya Marekani na sisi tufanye> JF sometimes kuna too much Negativity na kwa kweli mtu ukishinda sana humu utaishia kuwa negative.... kila kitu kulalamika oohoh wenzetu wenzetu wenzetu.Sasa hiyo si suala la programme tu na umuhimu wa habari . kwamba kwa sasa habari kubwa ni hiyo period haina uhusiano na huruma am kutokuwa na huruma. ndio mana baada ya mudda wataendelea na vipindi vyao. Pia kumbuka Haiti ni jirani na marekani sana na kuna wahaiti wengi wako America so it makes sense. lawama lawama kaaah!!!
   
Loading...