Kwanini wazungu husaidia haraka kwenye majanga?

Hivi wakulu mmesahau kama Bongo ni mtemi kati ya watemi wakusaidia? Bongo inasaidia wanapoweza kusaidia. Kwa mfano Bongo imewahi kusaidia wakimbizi wa Afrika kusini, Zimbabwe, Ruanda nk.
 
ukiacha uwezo walionao, wenzetu majanga yamewafika sana ukilinganisha na sisi. hebu fikiri matetemeko, vimbunga, mafuriko n.k kwa hiyo somo hilo linaeleweka vyema sana kwao kuliko sisi wenye ujuzi haba
 
Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!
Mwanakijiji,
Tafadhali hebu tuwe genuine kwa hili:
1. Niongelee kwa WaTanzania 90% ambao kuishi kwao ni kubahatisha tu, priority yao kubwa ni wao wenyewe kujiokoa kwanza. Mlo wa siku hujui utapata wapi na wanao utakuwa na muda wa kumkumbuka mwenye shida mwengine?

2. Haya majanga ni kweli yanatisha, lakini kwa nchi kama za kwetu Africa haya yapo kila siku, acha kuonyeshwa kwenye TV. Hata uwe genuine gani us huruma kiasi gani, wewe uko kama wale victims wa Haiti utatoa nini?? Je unakumbuka mwaka 1995 Japan kulitokea tetemeko, Senegal wakatoa dollar 2500; zikarudishwa; na kutoa ahsante nyingi sana; kwa sababu kwa Senegal zile dollar 2500 zilikuwa nyingi sana kwa matumizi yao wenyewe.

3. Pamoja ya kuwa kutoa si utajiri sawa kabisa, tukirudi kwenye grassroot, kule kwenye mila zetu, bado hadi leo tunasaidiana. Ila tu huu mchanganyiko wa mila na mila na dini na dini sasa hivi kweli hatujui culture yetu ipo wapi na wengi wameshpoteza hata culture zao, na kujiita vingine, kama wakristu,waislam, wapagani nk. Hiyo ndiyo kweli victimization ya culture zetu baada ya ile partition ya Africa. Mipaka haikujali culture.
 
Mwanakijiji,
Tafadhali hebu tuwe genuine kwa hili:
1. Niongelee kwa WaTanzania 90% ambao kuishi kwao ni kubahatisha tu, priority yao kubwa ni wao wenyewe kujiokoa kwanza. Mlo wa siku hujui utapata wapi na wanao utakuwa na muda wa kumkumbuka mwenye shida mwengine?
Kwa nini tuishi kwa kubahatisha? tunakosa nini kujiweka katika maisha ya uhakika?
3. Pamoja ya kuwa kutoa si utajiri sawa kabisa, tukirudi kwenye grassroot, kule kwenye mila zetu, bado hadi leo tunasaidiana. Ila tu huu mchanganyiko wa mila na mila na dini na dini sasa hivi kweli hatujui culture yetu ipo wapi na wengi wameshpoteza hata culture zao, na kujiita vingine, kama wakristu,waislam, wapagani nk. Hiyo ndiyo kweli victimization ya culture zetu baada ya ile partition ya Africa. Mipaka haikujali culture.
Sidhani kama hii ni kweli. Inapotokea michango wa harusi pale dar, utashangaa kuwa wachangiaji wanatoka sehemu zote za Tanzania. Nilishudia harusi moja ya ndugu yangu tukapokea michango kutoka kwa akina Mapunda, Rugemalila, Shekimweli, Mwakatumbula, Ole Saibul, Mrema, Shayo, Msuya, n.k
 
Kwa nini tuishi kwa kubahatisha? tunakosa nini kujiweka katika maisha ya uhakika?

Sidhani kama hii ni kweli. Inapotokea michango wa harusi pale dar, utashangaa kuwa wachangiaji wanatoka sehemu zote za Tanzania. Nilishudia harusi moja ya ndugu yangu tukapokea michango kutoka kwa akina Mapunda, Rugemalila, Shekimweli, Mwakatumbula, Ole Saibul, Mrema, Shayo, Msuya, n.k
Unajua hao ni Percent gani ya WaTanzania?
 
Kwa nini tuishi kwa kubahatisha? tunakosa nini kujiweka katika maisha ya uhakika?

Sidhani kama hii ni kweli. Inapotokea michango wa harusi pale dar, utashangaa kuwa wachangiaji wanatoka sehemu zote za Tanzania. Nilishudia harusi moja ya ndugu yangu tukapokea michango kutoka kwa akina Mapunda, Rugemalila, Shekimweli, Mwakatumbula, Ole Saibul, Mrema, Shayo, Msuya, n.k

Heck...kwani Lowassa alipoongoza ile harambee ya kuchangia Taifa Stars zilipatikana shilingi ngapi? Nadhani ni kama milioni 400 (kama hizo figure zilikuwa za kweli).

Kuweza tunaweza kabisa sema basi huwaga hatufanyi...
 
Duuh kazi kweli kweli ..... kwa ukarimu ni rangi ya mtu !!! Jamani mbona unajidharau kiasi hicho??? labda wenzetu wanan uwezo na nyenzo za kusaidia je? Umaskini una limit uwezo wa mtu kutoa. na hicho wanachotoa ukilinganisha na walichonacho ni maji ndani ya tone jamani tuelewe. Ni kama Bushi kumpa Kikwete Milioni 700 za vyandarau ili khari Bail out peke yake ni Bilioni Mia saba. Hii kutoa/ama kutokutoa haina uhusiano na rangi ya nguvu jamani ... hatat sisi tunakuwa na mawazo mgandoo hivyo na tupo JF. tafadhali jamani Kaaaah!

......Don't get me wrong , read my post and try to understand it. Mie sikumaanisha rangi ya mtu, ndio maana mwishoni nilisema kutoa ni moyo sio utajiri.
BTW tujifunze utoaji wabongo, wangapi wana uwezo hawataki kusaidia wasiojiweza.
Wangapi mnatupa chakula, na wakati huo huo kuna watu wanalala na njaa.
 
Unajua Mkuu mwanakijiji kuna kitu kingine nimekinotice, utakuta News channel TV karibu zote katika siku ya jana zinatoa updates ya nini kinaendelea Haiti at least in every 30mins. Hizi si TV za serikali ati........ Sasa njoo kwetu TV tena ya serikali habari za maafa tena nchini mwetu mnapewa wakati wa taarifa ya habari tu, tena inaweza hata isiwe ya kwanza..............

Sasa tujiulize inakuwaje TV za Marekani tena binafsi zinasuspend hata vile vipindi muhimu kuripoti maafa tena ya nchi nyingine???

"I AM INCLINED TO BELIEVE WE DON'T VALUE A HUMAN LIFE"

Ahsante sana Nyambala umeandika kitu kikubwa sana hapo. Hata katika hizi jitihada za kuchangisha pesa na vitu mbali mbali ili kuwasaidia wenzetu waliokumbwa na maafa. Pia sidhani kama vyombo vya habari vya walipa kodi kama vinatumia muda wao mwingi katika kuwahamasisha Watanzania katika kila kona ya nchi wajipigepige ili kuwasaidia wenzetu waliopatwa na maafa ya mafuriko.
 
Kila kitu wanachofanya Marekani na sisi tufanye> JF sometimes kuna too much Negativity na kwa kweli mtu ukishinda sana humu utaishia kuwa negative.... kila kitu kulalamika oohoh wenzetu wenzetu wenzetu.Sasa hiyo si suala la programme tu na umuhimu wa habari . kwamba kwa sasa habari kubwa ni hiyo period haina uhusiano na huruma am kutokuwa na huruma. ndio mana baada ya mudda wataendelea na vipindi vyao. Pia kumbuka Haiti ni jirani na marekani sana na kuna wahaiti wengi wako America so it makes sense. lawama lawama kaaah!!!

Maandishi yako yanareflect ni jinsi gani unashindwa kujibu hoja kwa hoja, hakuna aliyesema kila kifanyikacho Marekani na sisi tufanye. Kwa taarifa yako the news trend has been the same kwa siku ya jana as far as to the land down under (Oz), ABC, SKY mpaka 7 was just Haiti. Sasa sijui nao wako karibu na Haiti? Na unaposema ni habari tu si kweli kwani wakati wa hizi news ndio kuhamasisha michango kunaendelea. Au mkuu maandishi ya chini ya picha huwa husomi?????????? If u can recall and can keep records jana kipindi cha Larry King CNN ambacho kilikuwa so important, maana alikuwa akutane na waandishi wa kitabu cha game change, kiliahirishwa. Sasa wewe unasema it's just a program.Wabongo bana. Haisaidii kupinga jambo ambalo liko wazi kabisa. We have a problem and we need to fix it.
 
Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!
Ngozi nyeusi tunapenda kukusanya na wala sio kutawanya. Hatujui kama kutawanya ni namna nyingine ya kuwekeza. Moyo wenye kutoa hupata kibali mbele za Mungu na huongezewa kupewa uwezo zaidi. Ni mtihani tosha kwa nini hatuendelei. Maisha ya mswahili ni kukusanya na kamwe hayuko tayari kupunguza hata alichokichakaza ampe jirani. Nguo ya ndani inaweza kuvaliwa miaka 20 mfululizo hata kama haisitiri kitu, moyo huma kutupa jalalani.

Leka
 
Maandishi yako yanareflect ni jinsi gani unashindwa kujibu hoja kwa hoja, hakuna aliyesema kila kifanyikacho Marekani na sisi tufanye. Kwa taarifa yako the news trend has been the same kwa siku ya jana as far as to the land down under (Oz), ABC, SKY mpaka 7 was just Haiti. Sasa sijui nao wako karibu na Haiti? Na unaposema ni habari tu si kweli kwani wakati wa hizi news ndio kuhamasisha michango kunaendelea. Au mkuu maandishi ya chini ya picha huwa husomi?????????? If u can recall and can keep records jana kipindi cha Larry King CNN ambacho kilikuwa so important, maana alikuwa akutane na waandishi wa kitabu cha game change, kiliahirishwa. Sasa wewe unasema it's just a program.Wabongo bana. Haisaidii kupinga jambo ambalo liko wazi kabisa. We have a problem and we need to fix it.

Most popular stories right now

Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!

Hii mkuu ni changamoto kwa Afrika nzima. Natamani Afrika nzima ingesoma ujumbe huu na kuufanyia kazi. Huenda ikawa ndiyo sababu hawa jamaa zetu wanatuzidi sana kimaendeleo.

Kwa hili Mzee MW...nimejifunza kuwa maendeleo huanzia moyoni. Kumbe basi mwenye moyo wa kusaidia wengine...awe nacho au asiwe nacho huyo kwa hakika atakuwa na maendeleo tu katika dunia hii. Kwa sababu kuna maana gani sisi tusiosaidia wengine tukawa na maendeleo makubwa kuliko wao walio tayari kusaidia wengine wakati wa taabu????

This( together with many contributions in it pro to the thread) is one of the best threads ever!
 
Wakati wowote yanapotokea majanga, aidha ndani ya nchi zao u hata nje ya nchi zao raia wa nchi zilizoendelea wamekuwa na haraka ya kusaidia na kutoa misaada kwa haraka zaidi. Ninauliza hili nikilinangisha na mwitikio wa watu wetu kwenye majanga vile vile.

Leo hii wakati Haiti imekumbwa na tetemeko la ardhi, tayari wenzetu wameshaweka utaratibu wa watu wa kawaida kuchangia taasisi mbalimbali ikiwemo chama cha msalaba mwekundu. Na tayari hadi watoto wa shule hapa nilipo wameanza kukusanya nguo na vyakula vya makopo kupeleka huko Haiti!

Kwanini sisi, inakuwa mbinde sana kujitokeza kusaidia!? Yawezekana ni kweli Mungu amewapendelea wenzetu hawa kwa kuwapa moyo wa ukarimu zaidi kulikop watu weusi? Yawezekana wenzetu wanajali wenzao hata wageni zaidi kuliko sisi wengine? Yawezekana labda sisi tunapenda sana kuzungumza na kuonesha madhaifu kuliko kuonesha mfano wa kutenda?

Na wale Watanzania ambao wamejitokeza kuchangia hadi hivi sasa ndugu zao waliopatwa na mafuriko yawezekana wamefanya hivyo kwa sababu ni matajiri zaidi au ni moyo wao wa kutoa?

Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa!

Kwa kifupi ni kwamba, Kanuni ya Mungu ina sema ukitaka kubarikiwa Duniani basi toa. KUna mifano milioni ya watu walioprove hiyo. Wenzetu wamelijua hilo na wanalifanyia kazi sisi kama kawaida tunapenda kupokea na sio kutoa. Hizi baraka ni kwa nchi, taasisi na mtu binafsi
 
tatizo ni kwamba wananchi hawana imani na uongozi, je msaada unaotoa utawafikia walengwa??? na hii ni kwa sababu ya viongozi wetu kuwa na hulka ya kutafuta namna ya kujitajirisha wakati wa majanga. mnakumbuka mbagala? kulikuwa na complains kibao kuwa mamluki waliwekwa wakati wa kupokea misaada. nadhani hiki ndio kinawafanya watu wawe wazito kujitolea.
 
Unalosema naamini linawakilisha hisia za wengi. Hii ndio sababu mojawapo ya kuamua kusaidia Chama cha Msalaba Mwekundu kwa sababu kina rekodi ya kimataifa ya kujihusisha na majanga ya aina hii. Lakini ukweli wa binadamu ni kuwa haijalishi ni wapi wanadamu watachukua nafasi kujinufaisha.

Sasa hivi nimetoka kufuatilia suala la Haiti na FBI wameshatoa onyo kwa watu kuangalia watu au taasisi zitakazoibuka na kuanza kudai zinataka michango ya kuwasaidia walioathirika. Pendekezo lao ni mara zote kusaidia kutumia taasisi inayotambulika na kuaminika.
 
Mimi bado natafakari, inawezekana usambaaji wa taarifa ukawa ni tatizo. Uaminifu nalo ni tatizo. Ukienda kuwapa nguo utaambiwa unataka ubunge.
 
Ngoja nitafute dala dala lenye radio.

Kuna michango isio safi ila nimemuomba MUNGU alie juu anisamehe na dhamira yangu inasema nimesamehewa.

Kila mobile ninayoiona na kuikamata naandika TPN kwenda 15522.

Mtanisamehe mliochukia lakini siondoi tendo langu. Wengine hawana muda ati
 
unaeuliza hupendi misaada?sasa mfanyweje mkipewa mnakuwa na wasiwasi mkinyimwa mnalilia uvunguni.binadamu tufanyiwe nn?shukurani ni ziro minuz
 
Back
Top Bottom