Kwanini Wazanzibari wanampiga vita Rais Hussein Mwinyi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
887
4,133
Huku Zanzibar kuna mgawanyiko mkubwa kisiasa. Mzee Mwinyi anafanya vizuri sana kuleta maendeleo lakini hakubaliki. Baadhi ya factors zinazofanya asikubalike ni hizi hapa.

1. Siyo Mzanzibari
2. Anadaiwa kudharau kila kiongozi aliyepo chini yake
3. Anawafokea na kuwanyanyapaa viongozi wenzake hata wale wanaomzidi umri
4. Anaamini zaidi kwa wazanzibari waliopo nje ya nchi kuliko wakaazi wa Zanzibar hasa kwenye utawala
5.Anatumia zaidi mfumo wa kijeshi kuliko mfumo wa kiraia kusimamia mambo

Mfumo wake umemsaidia sana kuachana na lele mama ya wazazibar wengi na kuwalazimisha wawe strong. Pamoja na maendeleo itamlazimu kutumia zaidi jeshi na Tume ya Uchaguzi kumrejesha madarakani la sivyo anatarajiwa kutawala kipindi kimoja.
 
Siasa haina akili, Zanzibar inatawaliwa na Raisi Mbongo, Tanganyika inatawaliwa na Mzanzibari, Watanganyika wanamkataa Mzanzibari kuwa Raisi wao. Na Wazanzibari wanamkataa Mtanganyika kuwa Raisi wao.

Hii ndio kuna yule jamaa hapa JF anasema "Job true-true"
 
Duuh!
Politics!
 
Mm napinga dpw maisha.ila simpingi mama samia ni bahati hii bonge la rais
 
Wazanzibari wamejawa na fikra za kibaguzi. UbaguI huu upo mpk kwenye katiba yao. Katiba inaupa nguvu ubaguzi kwa uwaziri kabisa kwamba " ili mtu agombee uongozi lazima awe mzanzibari, na awe ameishi Zanzibar mfululizo kwa miaka 5 kuelekea uchaguzi husika".

Kwahiyo kuwa mzanzibari tu haitoshi. Ni lazima mtu awe ameishi kwa miaka 5 mfululizo huko Zanzibar..

Kwahiyo Dr. Mwinyi kubaguliwa, haishangazi.
 
Atuache tule tende yakhe, mambo ya mpera mpera kuvuja jasho hatujazoea sie! Ushan'fahamu?
Acheni dharau kwa taarifa yenu sasa Raia wa JMT ni Mzanzibari baraza la mawaziri cheki wako wangapi kweye chama chenu cha ccm na taasisi za serikali Wazanzibar kibao na wanapiga kazi freshi tu kuliko hao Mafisadi wenu
 
Tangu lini Wananchi wakaamua Viongozi kupitia boksi la Kura?

Huko Zanzibar wanaweza kupelekewa hata Mwijaku ama Baba Levo na wakawa Rais wao

Tena saivi wamezidi kuwa legelege baada ya Kifo cha Maalim Seifu
 
10% hata Tz Bara.

Masanja Mkandamizaji anaweza kusa Rais na Dr Tulia akahusudu😂😂
 
10% hata Tz Bara.

Masanja Mkandamizaji anaweza kusa Rais na Dr Tulia akahusudu😂😂
Sahihi kabisa

Sijajua kinachoendelea Chamani ila nimepata za kunyapia nyapia kama Wasemavyo Shilawadu eti Former RC wanataka awe PM ama mwenza Mwakani baada ya huyu aliyepo eti kusema hajachangamka jukwaani

Yaani pamoja na Vurugu zake zote zile wampe dhamana kubwa hivyo utasema wamekosa Viongozi wenye hekima zao
 
Back
Top Bottom