Kuna wakati hadi unawaza hizi huenda sheria zilitungwa wazembe, wavivu na wajinga ili kuwalinda dhidi ya ujinga wanaofanya. Ingekuwa goli lipo wazi wazembe kama hao ni kukata makofi tu ili mambo yaende kwa mtiririko unaofaa.
Serikalini ni Bora liende, watu wanataka salary tu, sio kazi, kwanza wengi hawana weredi wanachokifanya, pili hujiona wamepatia maisha kuliko wengine, hizi ni dalili za sheria za kazi hazifuatwi, ni ngumu Sana mtumishi wa umma kuwajibishwa,
Boss mwizi, salary milioni 2.5,ila ana gari ya milioni 700 baada ya miaka 5!!!
Kiboko yao ni idara ya utumishi wakikuzingua nenda idara ya utumishi, kwa mahakama ni tume ya utumishi waliwahi kuficha file la kesi yangu nilipowaripoti walifokewa kama watoto wadogo
Sisi ngozi nyeusi tuna shida kubwa sana ambayo wakati mwingine hatupendi kuikubali...ubinafsi, roho mbaya, ubaguzi na uchoyo vipo sana miongoni mwetu.
mzungu, Mhindi au Mwarabu akitufanyia jambo la kibaguzi, tunapaza sauti na kusema, “Tunabaguliwa!” Lakini tukijitazama kwa undani, kuna nyakati ambapo sisi kwa sisi tunabaguana, tunachukiana, tunanyimana fursa na kushindwa kufurahia mafanikio ya wenzetu.
Mtu upo ofisi ya umma ni wajibu wako kutoa huduma, viburi sasa na kununa vimetawala
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.