Kwanini Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha R na L kwenye kuandika Kiswahili na si Kiingereza?

french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
3,525
3,649
Hili tatizo lipo kwa Watanzania wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si Kiingereza.

Mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri.

Hivi tatizo ni nini haswa. Hebu wadau nipeni majibu ya maana
 
Hili tatizo lipo kwa watz wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si kiingereza. mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri. hivi tatizo ni nini haswa. hebu wadau nipeni majibu ya maana
Mkuu haya mambo yanaenda na kizazi(generation).

Waliozaliwa 80' kurudi nyuma hauwezi kuta hilo tatizo mtu analo, labda kwa bahati mbaya.

Na pia tangia kazi ya ualimu ifanywe ni kijiwe cha kutafutia kazi kwa waliofeli, ndiyo yamejitokeza yote haya.
 
Ukiona umeshindwa kulitambua hilo jua ww nae pia unamapungufu kichwani.

Anavyo andika kitu tambua ndivyo anavyo kitamka hio utokana na mazingira aliyo kulia lugha mama ya ilo eneo imauwezo mkubwa wa kuathiri kiswahili chake.
Mfano. Sisi tuliokulia maeneo ya Mara si rahis kutumia "l" kwenye kiswahili chetu maana kwenye native language maneno yenye "l" nimachache ama hayapo kabsa kwaiyo wakati wa kujifunza lugha anajifunza kwa rafudhi ya lugha eneo husika
 
Mkuu haya mambo yanaenda na kizazi(generation).

Waliozaliwa 80' kurudi nyuma hauwezi kuta hilo tatizo mtu analo, labda kwa bahati mbaya.

Na pia tangia kazi ya ualimu ifanywe ni kijiwe cha kutafutia kazi kwa waliofeli, ndiyo yamejitokeza yote haya.
Ujachunguza tu ata hao wa miaka ya 80 walikuwa kama sisi tu sema wao walikuwa hawana platforms zinazo weza kufanya mtu akujua uwandishi wa kila mtu kama ilivyo hv sasa.

Kuhusu walimu hapo ni upotoshaji tu hakuna ukwel wowote ule
 
Hili ni tatizo linalokua,
Kuna wale kuweka au kutoa "H" sehemu isiyo sahihi ila hawa nimewaona humu JF...

Mfano, badala ya
Haya anadika Aya,
Hakuna anaandika Akuna,
Hapana anaandika Apana,

Ili Anaandika Hili,

Kikubwa turekebishane, ni makosa ambayo naamini wengi hufanya bila kujua...
Na yeyote hukosea.
 
Hili tatizo lipo kwa watz wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si kiingereza. mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri. hivi tatizo ni nini haswa. hebu wadau nipeni majibu ya maana
Moja,kutamka na kuandika mara nyingi ni vitu tofauti kabisa ,km utatamka neno ambalo hujawahi ona limeandikwaje ni rahisi kukosea kuliandika.

Pili matamshi huwa yanabadilika kuendana na lafudhi ya makabila mbalimbali si jambo la ajabu kumsikia Mkurya akachanganya r na l.
Tatu ni exposure kwenye ustaarabu na Elimu kuna shape vile unavyoongea na kuandika,usitegemee mtu aliyekulia kijijini ndani ndani ataona kuna Umuhimu wa kutofautisha r na l?

Mwisho ni athari ya lugha za kitaa,chukulia mfano hili neno "kwendraa"sasa kwajinsi linavyoenea kuna siku za baadae kizazi kilichopo kitaamini ni neno sahihi.

NB nimefuatilia mabandiko mengi humu pamoja na kuamini tunajua kuandika lkn wengi wetu hawajali punctuation kbs,yaani uzi umemwagika utadhani maji korongoni hauna koma wala fuli stopu!
 
Walimu wabovu wa kiswahili tu mkuu.

Wamelilea tatizo huenda nao ni wahanga wa tatizo hilo.

Hilo tatizo lisingekuwepo kama walimu wangekuwa vizuri
 
Hili tatizo lipo kwa watz wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si kiingereza. mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri. hivi tatizo ni nini haswa. hebu wadau nipeni majibu ya maana
ukifuatilia vizuri walio wengi ni vilaza hajaenda shule au kama amenda basi ameunga unga na akifuatilia kwa ukaribu maisha yake atakuwa ameishi uswahilini.

Msomi aliye elimika vizuri tungu mwanzo wa elimu kamwe hawezi kushindwa kutofautisha kati ya "R" na "L" chunguza utaona.
 
Back
Top Bottom