Nasikitika na Wasanii wetu

HustlerD

Senior Member
May 15, 2021
131
425
Ni kweli Mwenyezi Mungu kaibariki nchi hii kwa kila kitu ambacho hata ukienda dunia ipi sidhani kama utakikuta (naongea kwa uzoefu wa kusafiri na kukaa nje)

Imagine nchi ina Mbuga za wanyama kubwa (Serengeti, Ngorongoro n.k) Maziwa makubwa (Victoria, Tanganyika, Nyasa n.k) Madini ya kila aina (almasi, dhahabu, Tanzanite n.k)

Wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, Ali kiba, Harmonize n.k

Sasa kinachoniumiza mimi, ni hawa wasanii wetu, na wengi wa watu maarufu wa mitandaoni, yaani wengi wao waliingia kwenye mziki baada ya kuitupa elimu mapema kabisa kwenye maisha yao, sasa inawagharimu, hilo siyo kosa lao

Tatizo linakuja kwamba hata akiandika kitu au kupost kitu bado haweza hata kutofautisha kati ya baadhi ya herufi za kutumia kwenye sentensi, siyo kiswahili wala kiingeleza. Mfano, Sehemu ya kuweka 'r' anaweka 'l' na kinyume chake, na maneno mengine mengi tu, yaani ukisoma wanachoandika unabaki kuumia moyoni maana unawapenda sana na unawaombea mema lakini sasa kwa style hii kama nchi tutafika wapi kimziki na umaarufu wa watu wetu.

Kama tunataka kufika mbali zaidi, Serikali irudishe elimu ya kusoma na kuandika kwa wasanii wetu, hao ni kioo cha jamii yetu pia.

Hatuwezi kuwakilishwa na watu ambao hawawezi hata kuunga sentensi ikakamilika bila makosa.
 
Bora kuwa na elimu au kuwa Kama diamond hasiye na elimu Ila anagonga viza tu, tunang'onjea birthday ya bi mkubwa tuone balaa lake.
 
vitu vyote hivi vinavyotuzunguka ukaona hii ni mada tuijadili?? unaanzaje kukereka na vitu havikuhusu?? sasa ulitaka umsomeshe wewe? pambana kuleta ugali mezani temana na mbanga hazikuhusu zitakupotezea muda jus listen to good music wanatupa hizo n maisha zao binafs
 
Kwanza wanamaisha mazuri kuliko sisi tulioenda mavyuoni miaka mitatu kitabu.
 
Kwanza wanamaisha mazuri kuliko sisi tulioenda mavyuoni miaka mitatu kitabu.
Wewe unaweza kuishi maisha yao ukaweza? Kukatika hovyo. Kushi kwa shikwa na mavideo vix. Kufanya mambo ya hovyo hovyo, kwenda kwa waganga.
Ukiweza hivyo basi hixo hela utapata.
Kama chaguo lako ni hela basi mambo mengi tu ya hovyo yapo unapiga hela fasta.
Kuna watu gata suasa tu hawawezi kufa ya kwa sababu ya mambo ya hovyo sembuze kujianika majukwaaani umevaa tunguo twa hovyo. Sikiliza wimbo wa sitaki tena muziki wa bwana Madee, ameeleza jinsi alivypoteza utu wake kwa kuwa mwanamuziki.
Ila sio kila aina ya muziki humtoa mtu utu wake.
 
Nahemimu mawazo yako, madee kafulia Yule, waganga gani? Kama ya kweli kila mwanamziki angekuwa hot, sio kila mwanamziki au msanii mshirikina, maneno hata kwenye kanga yapo, we ukienda kwenye sherehe huchezi mziki, mr blue au sugu, profesa j wanakata mauno miziki yao?
 
Nenda kajiunge basi unasubiri nini? Andika mashairi nenda studio upige hela uwe sugu.
Siku hizi kuna studio mpaka vijijini, we nenda tu imba upige hela, yani unajua kabisa kuna hela unawaachia tu wenyewe waendelee kupiga hela wakati unaweza kufanya wanayoyafanya!
 
Niwe sugu kwakuwa nimewasifia we unataka niwaponde wakati kila kitu na kuhusu ushirikina hata mzee yusuph alisemaga Kama mi naloga na nyinyi mkaloge, na kutunga mashairi ni Maisha na maamuzi ya mtu, kwakuwa fulani anauza magari ukimsifia na wewe ukauze, au fulani kapiga hatua na wewe usimsifie au upinge, ukibariki na wewe utabarikiwa.
 
Back
Top Bottom