Wanasema hatujui Kizungu, lakini tumeshajitathmini kwenye Kiswahili?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Madai kuwa Watanzania hawajui lugha ya Kimataifa, "English", si sahihi kwa asilimia mia. Lakini nakubali kuwa kuna Watanzania ambao kwa nafasi zao, walipaswa kufahamu Kizungu kwa ufasaha lakini kwa "bahati mbaya", imekuwa kinyume chake.

Wapo Watanzania wenye Elimu ndogo sana lakini wanaongea Kizungu kizuri utadhani wamekulia Uzungni, na kuna Watanzania wenye Elimu kubwa lakini "Vingereza" vyao ni vichekesho.

Kwa bara la Afrika, Tanzania ndilo Taifa linaloongoza kwa watu wake wengi kuongea Kiswahili. Ni Watanzania wachache sana, kama wapo, wasiofahamu Kiswahili.

Inafahamika hata kwa majirani zetu kuwa sisi tunafahamu Kiswahili. Lakini sisi tumeshajitadhmini katika hilo?

Kuna baadhi ya watu wanaosumbuliwa sana na matumizi ya R na L, madhalani, watu wa Kanda ya Ziwa na Pwani.

Utamkuta mtu anatamka neno "Buseru", lakini ukimwambia aandike, linakuwwa "Buselu". Mwingine atakuambia ametoka Isingiro, lakini kwenye maandishi, utalikuta Isingilo. Au Rwamgasa lakini akiandika linasomeka Lwamgasa. Mahali fulani, nikiambiwa kuna Sekondari inayoitwa Lubiri, lakini nilipofika maeneo hayo, nilikuta kibao chake kimeandikwa Lubili.

Mwingine, atataja jina la mtu kama Lama, lakini kwenye maandishi linaandikwa Rama.

Kurwa linatamkwa Kurwa, lakini kwenye maandishi, utalikuta Kulwa.

Mwingine, atatamka neno Mchele, lakini kwenye maandishi, ataandika "mchere".

Mwanzoni, nilifikiri hilo tatizo lipo kwa watu ambao hawajasoma.
Lakini sivyo, lipo na kwa wasomi wakiwemo Walimu.

Ikiwa Mwalimu anaongea na kuandika Kiswahili chenye matamshi "broken", si inaweza kuwa chanzo cha "ubroken" wa matamshi kuendelea kutamalaki kwenye Kiswahili?

Wakati mwingine, "ubroken" wa matamshi ya Kiswahili huathiri hata matamshi ya Kingereza. L hutumika sehemu ya R na R badala ya L.

Najua hata kama tutakidhiri kuongea Kiswahili "broken", majirani zetu hawataweza kutuzodoa katika hilo kama wanavyotusimanga kwenye Kizungu. Wataanzia wapi, hasa ikizingatiwa kuwa wako chali katika utumiaji wa hii lugha adhimu?

Pamoja na kwamba hatuna mshindani kwenye hii lugha nzuri, Kiswahili, isingekuwa vizuri zaidi kama tungeendelea kujiboresha zaidi na zaidi? Kwa nini kusingewekwa kigezo kuwa Walimu kuanzia Chekechea mpaka Sekondari sharti wawe na k3 fasaha?

Kuongea Kiswahili fasaha!
Kuandika Kiswahili fasaha!
Kusoma Kiswahili fasaha!

Naamini sababu mojawapo ya mwanafunzi Tanzania kumaliza Kidato cha Nne akiwa "hajui" Kizungu, ni kwa sababu Walimu wake nao "hawakijui". Isingekuwa vyema kama mamlaka husika ingehakikisha kuwa Walimu wote kuanzia Chekechea hadi "High School" wanafahamu kwa ufasaha Kiswahili cha kusoma, kuandika na kuongea?

Majirani zetu wamepata kile wanachokiita sababu halali ya kutukosoa kuwa hatujui Kizungu, na sisi tusijipe sababu yoyote ya kutokujua Kiswahili fasaha.
 
Majirani zetu wamepata kile wanachokiita sababu halali ya kutukosoa kuwa hatujui Kizungu, na sisi tusijipe sababu yoyote ya kutokujua Kiswahili fasaha.
Maisha sio magumu kihivyo, SEMA Wahuni wachache wanataka tu kutuongezea stress 😬, nina mambo mia kidogo then nianze kufanya mashindano ya lugha? Lengo la lugha ni kuwasiliana, kama tunawasiliana basi inatosha.
 
Maisha sio magumu kihivyo, SEMA Wahuni wachache wanataka tu kutuongezea stress 😬, nina mambo mia kidogo then nianze kufanya mashindano ya lugha? Lengo la lugha ni kuwasiliana, kama tunawasiliana basi inatosha.
😀
 
➡️ sisi tumeshajitadhmini katika hilo?

➡️ madhalani watu wa Kanda ya Ziwa na Pwani.

➡️ Najua hata kama tutakidhiri/b] kuongea Kiswahili "zaidi?

Wewe mwenyewe hapo tayari th na dh zinakuchanganya 😁😁😁

Unachokiongelea ni athari za lugha ya mama katika lugha ya pili na ni jambo la kawaida. Kwa mfano Kisukuma hakina /r/ kwa hivyo haishangazi Msukuma kukuta anatumia /l/ kila mahali. Kikurya nacho hakina /l/ na hivyo haishangazi kumkuta Mkurya akitumia /r/ kila mahali. Mhaya na Mkerewe hata asome vipi bado atakuwa hana uhakika wapi pa kutumia /h/ na wapi asitumie. Msomi kabisa wa Kihaya ni kawaida tu kumkuta akisema [husiniambie] au [kwa akika].

Kwa kawaida matatizo haya huwa hayaleti shida sana labda tu mpaka pale athari hizi zinapobadilisha maana [mahali ~ mahari], [kula ~ kura]...na mkanganyiko unaoweza kuletwa na kikanushi /h/ hasa kinapotumika vibaya...

Hata Kiingereza kina matatizo haya kwa watumiaji wake; na wanatambuana hivyo kwamba huyu katoka New York, New Orleans n.k.[/b]
 
Back
Top Bottom