Kwanini Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha R na L kwenye kuandika Kiswahili na si Kiingereza?

ukifuatilia vizuri walio wengi ni vilaza hajaenda shule au kama amenda basi ameunga unga na akifuatilia kwa ukaribu maisha yake atakuwa ameishi uswahilini.

Msomi aliye elimika vizuri tungu mwanzo wa elimu kamwe hawezi kushindwa kutofautisha kati ya "R" na "L" chunguza utaona.
Acha ulimbukeni watu wanaathirika na lugha mama zao.....ata uwe ushuani kiaje lazima utakuwa na lugha mama
 
Kuna wakili mmoja huwa namsikia sana kwenye Amplifaya ya Millard pale Clouds..yaani anavyoweka hizo L kwenye R ni hatari..utamsikia akisema Lapa badala ya Rapa..yaani kichefuchefu kabisa.
 
Mkuu haya mambo yanaenda na kizazi(generation).

Waliozaliwa 80' kurudi nyuma hauwezi kuta hilo tatizo mtu analo, labda kwa bahati mbaya.

Na pia tangia kazi ya ualimu ifanywe ni kijiwe cha kutafutia kazi kwa waliofeli, ndiyo yamejitokeza yote haya.
Kuna ukweli hapo.
 
Hili tatizo lipo kwa watz wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si kiingereza. mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri. hivi tatizo ni nini haswa. hebu wadau nipeni majibu ya maana
Kinachosababisha ni lugha za makabila. Mother tongue language inaweza kuharibu au kuboresha matamshi ya mtu anapozungumza lugha nyingine. Mfano angalia Kiingereza kiingereza wanachozungumza wanaigeria, wahindi, waarabu, wapakstani kimeharibiwa na lugha zao za makabila.
 
Hili tatizo lipo kwa watz wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si kiingereza. mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri. hivi tatizo ni nini haswa. hebu wadau nipeni majibu ya maana
Huwa wananikera sana aise.
 
Mwalimu; kaandika neno ubaoni "thelathini, theluthi, serikali, rasilimali, ujasiri, ujasiriamali

Mwanafunzi anaona kilichoandikwa ubaoni ila yeye anaandika tofauti "selasini, selusi, selikali, lasiliamali, ujasili, ujasiliamali" (mikoa ya pwani morogoro)

Tusilaumu walimu, mzizi wa hili tatizo ni mazingira ya matamshi ya lugha Mama ambayo mtoto anapitia kabla ya kuanza shule.
 
Sasa kama utamuacha maana ya kufundisha ni ipi hasa!
 
Jiulize Walimu wa Secondary kipindi fulani walivyokuwa wanalalamika Kupelekewa wanafunzi hawajui kusoma itakosekana vipi Graduate kuandika Mararamiko badala ya Malalamiko?
 
ukifuatilia vizuri walio wengi ni vilaza hajaenda shule au kama amenda basi ameunga unga na akifuatilia kwa ukaribu maisha yake atakuwa ameishi uswahilini.

Msomi aliye elimika vizuri tungu mwanzo wa elimu kamwe hawezi kushindwa kutofautisha kati ya "R" na "L" chunguza utaona.

ni bora kuanzisha darasa rasmi la kuwafundisha hawa wasio jiweza kutofautisha kati ya " R" na "L"
tena kuwa na mtaala maalum.

hawa ndio wale tunashindwa kuwaelewa mfano;

Lais badala ya Rais
plesident badala ya Presedent.

sasa watu wa aina hiyo unaweza kusema wamesoma kweli?!
 
Mwalimu; kaandika neno ubaoni "thelathini, theluthi, serikali, rasilimali, ujasiri, ujasiriamali

Mwanafunzi anaona kilichoandikwa ubaoni ila yeye anaandika tofauti "selasini, selusi, selikali, lasiliamali, ujasili, ujasiliamali" (mikoa ya pwani morogoro)

Tusilaumu walimu, mzizi wa hili tatizo ni mazingira ya matamshi ya lugha Mama ambayo mtoto anapitia kabla ya kuanza shule.
Tusijifiche kwenye kichaka cha lugha mama na kutafuta excuse, nakubali lugha mama zinatuathiri sana lakini ni kwenye matamshi zaidi. Chunguza watu wengi wa kuanzia 80s kushuka chini hawana makosa hayo ya R na L kiuandishi kama ilivyo kwa watu wa 90s kuja juu, mtu anatamka 'gali' lakini anaandika 'gari' vizuri tu.
Mi nadhani ni hiki kizazi cha sasa ndo kimeshahalalisha hayo makosa ya kiuandishi na kuonekana ni kawaida kabisa, na kwenye kufupisha maneno ndio balaa zaidi
 
Hili tatizo lipo kwa watz wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si kiingereza. mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri. hivi tatizo ni nini haswa. hebu wadau nipeni majibu ya maana
wanakera sana. eti mtu anatamka Lafiki
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom