Kwanini Watanzania wengi wanaonekana hawana hamasa ya kupiga kura uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019?

Najua wengi watanipinga ila ukweli ni kwamba watu wengi wanaonekana hawana mudi wala mpango wa kupiga kura wala kushiriki uchaguzi mdogo huu wa serikali jambo hili nimelishuhudia

Safari hii kuna gali linapita mtaani kwangu likihamasishe watu wakajisajili majina yao ili waweze kushiriki uchaguzi huu wa serikali mtaa kitu nilichoshangaa watu wengi wako bize na shughuli zao hata hawamsikilizi mtoa matangazo, wengi yaani tofauti na zamani nilikuwa na hamsha hamsha ya uchaguzi ila safari hiii sijui ni mini tatizo.
Hapa kazi tu ,tunachapa kazi kujenga taifa ndiyo maana tunataka magu tumpe miaka 20 pasipo uchaguzi wa raisi
 
Kutokupiga kura ni maamuzi, kinachonishangaza ni sababu inayokupelekea kufanya hayo maamuzi.

Hupigi kura sababu unahisi kura haitoheshimiwa na atatangazwa mshindi ambaye hamkumchagua, lakini maamuzi hayo yatasababisha huyo msiyemtaka atangazwe kirahisi zaidi na hamtaweza kuhoji maana hamkuhusika. Yaani unatoa msaada ili usilopenda, likamilike kirahisi zaidi.

Ndo maana nkakupa mfano wa ukabila wa umasaini na Mpare, Mpare ataweza kuiba kura za wamasai kirahisi? Na iwapo wamasai wasipopiga kura hata akitangazwa Mpare awaongoze watahoji?
Nachosema nikipiga kura au nisipopiga haitafanya tofauti yoyote kwa sababu tayari mamlaka inataka watu fulani ndiyo wawe washindi. Zoezi zima la upigaji kura ni "farce" na linafanyika ili kuhalalisha haramu. Mtu mwenye akili timamu hawezi kupiga kura kwa kurejea kauli na matendo ya viongozi wa hii serikali ya awamu ya 5.

Nadhani juzi umesikia majibu ya Mheshimiwa Rais kule Momba akimjibu yule mama. Na DC wa Dododma bila shaka utakuwa umemsikia.

Nawasikitikia sana wapinzani wanaoshiriki huu uchaguzi maana wanashiriki zoezi zima la kuhalalisha hujuma dhidi ya democrasia. Maadam CCM wameamua kufanya kila hila washinde cha msingi ni kuwaacha washinde ili labda watutoe kwenye huu umasikini uliotopea. Inawezekana Wapinzani ni kikwazo kwao kwenye kutekeleza sera zao. Sasa ili wakose sababu tuwaache washine kila nafasi ili tuone tofauti gani wataleta.
 
Waacheni mataahira ya Lumumba tu ndio wajiandikishe na kupiga kura kwani dikteta uchwara ameshapiga mkwara kuhusu mpinzani kutangazwa kua ameshinda!
 
Back
Top Bottom