#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

msimamo wa watanzania juu ya corona ni

1,corona ni ugonjwa wa mafua kama yalivyo mengine,na yuko tayari kuishi nao.
hata mheshimiwa anajua hilo,labda kuna namna anatafuta kuridhisha watu fulani.
Don't generalize. Not all Tanzanians including myself are against the vaccine. "Ni wewe tu na wengine waina yako mliokaririshwa na kulishwa dhana potovu ndiyo mnaopinga". It is simple: Take or don't take it.
 
SAWA WALETE WASIJE WAKALETA MZIGO UTAKO EXPIRE PASIPO KUTUMIKA, NI HASARA KWA TAIFA
Kuna program inaitwa COVAX, chanjo za bei rahisi na kwa nchi nyingine wamepewa bure. Na wanaweza kuleta, zikauzwa;

Swala la muhimu, kina Gwajima wasizuie wenzao kupata chanjo kwa masuala ya imani. Ni kama nguruwe na pombe; kuna imani zinakataza, lakini zipo. Ukitaka kanunue.
 
Zamani kwenye history tulikua na vijipoint flani flani kwenye topic ya neo-colonialism kwamba wazungu bado wanaitawala Africa kutokana na baadhi ya viongizi wa africa ni purpet leaders.Enzi hizo bado nilikua sielewi hyo concept vizuri sasa saiv ndo naielewa na kuona uhalisia wake
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19,
Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania
Mapendekezo yangu
1)Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa
2)Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea
3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo
4)Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
Sababu kuu inayowafanya baadhi ya watanzania kukataa chanjo ni UJINGA
 
Yaani hawajui hata wanacholaumu.

Unalaumu wazungu kuhusu CORONA wakati Corona imeanzia China?

Huziamini chanjo: Je, huziamini chanjo zipi: Astra Zeneca, Moderna, Pfizer au Sinovac ya Mchina ?
Hivi katika hizi ulizotaja hapo aliyotengeneza muhindi ni IPI hapo?
 
Kuna program inaitwa COVAX, chanjo za bei rahisi na kwa nchi nyingine wamepewa bure. Na wanaweza kuleta, zikauzwa;

Swala la muhimu, kina Gwajima wasizuie wenzao kupata chanjo kwa masuala ya imani. Ni kama nguruwe na pombe; kuna imani zinakataza, lakini zipo. Ukitaka kanunue.
Sasa huo mpango wa COVAX FACILITY, watakuingizaji iwapo hauna taarifa za waathirika wanaoweza shawishi wakuingize kwenye huo mpango, bado mtihani kweliweli. Otherwise uje mpango wa kuanzisha ving'ola vya ambulance, na kufungwa majumba ya ibada, hata kwenda sokoni kuwe kwa muda maalum, hapo takwimu zitapatikana kiurahisi, na hapo kukithi vigezo
 
Kama ulisikiliza siku ya kukabidhi report ya Covid 19, serikali haikusema chanjo ni lazima, ilisema chanjo ni hiari. Wanajua bado kuna watu wako na njozi za mwendazake, kwa hiyo hawawezi kulazimisha. Muda utafiki hata wale wenye mawazo ya mwendazake wataelewa na maisha yatakwenda vizuri. Wapewe muda maluweluwe yawatoke kichwani.
 
Sasa huo mpango wa COVAX FACILITY, watakuingizaji iwapo hauna taarifa za waathirika wanaoweza shawishi wakuingize kwenye huo mpango, bado mtihani kweliweli. Otherwise uje mpango wa kuanzisha ving'ola vya ambulance, na kufungwa majumba ya ibada, hata kwenda sokoni kuwe kwa muda maalum, hapo takwimu zitapatikana kiurahisi, na hapo kukithi vigezo
Taarifa za waathirika zipo, na wala sio lazima kusemea TBC, wanaweza wakawapa WHO na CDC Afrika na mambo yakaendelea
 
Huyu nae anatuchanganya tu hapa ili tufe
 
Back
Top Bottom