MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Tanzania ilikuwa moja ya nchi kinara barani Afrika kutetea haki za Wapalestina. Nchi hii ilienda mbali na kuamua hata kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na nchi ya Israel mwaka 1973 baada ya shinikizo la nchi za kiarabu zilizokuwepo ndani ya O.A.U kuwa kubwa.
Ikumbukwe Israel walikuwa na mchango mkubwa kwa Tanzania kuliko hata Palestine, kwasababu wao ndiyo walisaidia katika kufundisha maafisa wengi wa jeshi la Tanzania, akiwemo Marehemu Generali Muhiddin Kimario, pamoja na kusuka JKT.
Mwaka 1973, baada ya vita vya Yom Kippur nchi nyingi za Afrika zilivunja mahusiano ya kidiplomasia na Israel, na kuanza kutetea haki za Wapalestina. Ukisoma nyaraka za OAU, moja katika falsafa inazozipinga ni UZAYUNI (ZIONISM) na UBAGUZI WA RANGI (APARTHEID).
Tanzania ilikwenda mbali na kuanza kutetea haki za wapalestina kule UN. Kinachoshangaza ni kwamba Palestine Liberation Organization (PLO), mbali na kuwa marafiki wa Tanzania, walijiunga na vikosi vya Libya katika kumsaidia Idd Amin ambaye alikuwa anapambana na Tanzania.
Ikumbukwe tu, mwaka 1973 Tanzania ndiyo ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuitambua PLO na kuruhusu kundi hilo kujenga makao yake jijini Dar es salaam. Ofisi za PLO jijini , Dar es salaam ndiyo yalikuwa makao makuu ya PLO barani Afrika. Katika moja ya nukuu ambayo Mzee Nyerere aliwahi kuitoa kuhusu Palestina ni hii:
"Kizazi chetu kilikuwa kizazi cha mapambano ya utaifa kwa ajili ya uhuru wa nchi zetu … lakini hali ya Wapalestina ni tofauti sana na mbaya zaidi, Wamenyang’anywa nchi yao wenyewe, Kwa hiyo wanastahili kuungwa mkono na Tanzania na dunia nzima"
Najiuliza tu, chanzo kikubwa cha PLO kuisaliti nchi ambayo ilikuwa inawatetea hivi ni nini ?