Kwanini wanawake na wanaume hawachanganyikani msikitini?

Kwanini wanawake na wanaume hawachanganyikani msikitini?

Ni utaratibu tu waliojiwekea Waislam wakiamini kuwa, kila jinsia wakikaa mahali pao wenyewe watapata fursa zaidi ya kuwasiliana na Mungu kwa unyenyekevu zaidi na kuepusha matamanio.
Fikiria upo kwenye Ibada halafu anapita mrembo mwenye figure la ukweli au anaketi karibu na ulipokaa, Unaweza jikuta muda mwingi unawazia Mrembo badala ibada iliyokupeleka.....
 
Kumeandika wapi ? Kuna utengano ila chumba kimoja wanaswali kabisa..Kwa itifaki ya wanaume kukaa mbele .

Wanavyofanya kutenganisha vyumba sio makosa ila pia sio sheria ..Lakini kumbuka, mwanamke anaweza kusali home bila ya wasiwasi ipo misikiti haina sehemu ya wanawake kabisa .Mfano hapa ibadhi ,ninaposali stendi ya zamani Tanga ,sijawahi kuona wanawake.
 
Ni utaratibu tu waliojiwekea Waislam wakiamini kuwa, kila jinsia wakikaa mahali pao wenyewe watapata fursa zaidi ya kuongea na Mungu na kuepusha matamanio.
Fikiria upo kwenye Ibada halafu anapita mrembo mwenye figure la ukweli au anaketi karibu na ulipokaa, Unaweza jikuta muda mwingi unawazia Mrembo badala ibada iliyokupeleka.....
Msikiti unaweza kuwekwa milango miwili na pande mbili kwa ndani, mfano wanaume wakawa upande wa kulia na wanawake wakawa upande wa kushoto.
 
Kumeandika wapi ? Kuna utengano ila chumba kimoja wanaswali kabisa..Kwa itifaki ya wanaume kukaa mbele .

Wanavyofanya kutenganisha vyumba sio makosa ila pia sio sheria ..Lakini kumbuka, mwanamke anaweza kusali home bila ya wasiwasi ipo misikiti haina sehemu ya wanawake kabisa .Mfano hapa ibadhi ,ninaposali stendi ya zamani Tanga ,sijawahi kuona wanawake.
Kama hakuna Aya au hadithi ni wao tu wamejiongeza sasa kwa nini badala ya kuwa na vyumba tofauti isiwe ni chumba kimoja tu ila kila jinsia inakaa upande wake?
 
Wanavyofanya kutenganisha vyumba sio makosa ila pia sio sheria ..Lakini kumbuka, mwanamke anaweza kusali home bila ya wasiwasi ipo misikiti haina sehemu ya wanawake kabisa .Mfano hapa ibadhi ,ninaposali stendi ya zamani Tanga ,sijawahi kuona wanawake.
Unamaanisha sio lazima wanawake wa Kiislamu kwenda kuswali misikitini??
 
Msikiti unaweza kuwekwa milango miwili na pande mbili kwa ndani, mfano wanaume wakawa upande wa kulia na wanawake wakawa upande wa kushoto.

Ipo misikiti mingi tu imegawanywa hivyo, ila pale katikati wameweka pazia au ceiling board. Lengo ni hilo hilo, kuwapa kila upande Fursa ya kuwasiliana na Mungu kwenye hali ya unyenyekevu na kuepusha kuchanganya Ibada na matamanio.....Wanaume tumeumbiwa kutamani....
 
Ni kwa nini katika Uislamu wanawake na wanaume hawachanganyikani katika chumba kimoja msikitini?
Mkuu swala hilo linaitwa Ikhtilat kwa lugha ya kiarabu..
sasa nini faida yake:

1. Kulinda Unyenyekevu (Khushui')
Unajua swala ya kiislamu inavyofanyika kuna kugusana baina ya vidole vya miguu na kuna kulinganisha mabega na zaidi kuna rukuu na sigda inayomtaka muumini kuinama na kuinuka na kuinamisha kichwa chini jambo ambalo kama utaswali na mwanamke pembeni linaweza kuondoa utulivu kwa kuamka matamanio na kukuondoa kwenye swala (unajua tena wenzetu wameumbwa na magnnetism)

2. Kuepuka Vishawishi (Fitna)
Uislamu unasisitiza kuzuia mazingira yanayoweza kuleta vishawishi kati ya jinsia mbili katika maeneo ya ibada. Kwa kutenga sehemu za kuswali, jamii inajenga mazingira ya heshima ambapo kila mmoja anaweza kuabudu kwa uhuru.

3. Sunnah
Wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W), wanawake waliswali msikitini lakini walikuwa nyuma ya safu za wanaume. Mtume alisema kuwa safu bora kwa wanaume ni za mbele, na safu bora kwa wanawake (katika mazingira ya pamoja) ni za nyuma. Baadaye, kadiri idadi ya watu ilivyoongezeka, kuta au vyumba maalum viliwekwa kwa ajili ya urahisi na faragha zaidi.

SASA mkuu nakurudishia swali kuwa je kwenye biblia au tamaduni za zmani hakuna hiki kitu namaanisha kabla ya uislamu yaani hiki kitu ni kipya ???

hapana sio ktu kipya
Katika nyakati za Wana wa israel na hata baada ya hapo, Hekalu la Yerusalemu lilikuwa na sehemu maalum iitwayo "Ezrat Nashim (עֶזְרַת נָשִׁים)" Yaani Court of the Women.

Wanawake hawakuruhusiwa kuingia katika maeneo ya ndani yaliyotengwa kwa wanaume wa Kiisraeli au makuhani. Huu ulikuwa mgawanyo wa wazi wa kijinsia katika ibada.

Japo kwenye Katika Hekalu la Pili la Yerusalemu (Hekalu la Herode), hili lilikuwa eneo la nje ambapo Wayahudi wote (wanaume kwa wanawake) waliruhusiwa kuingia kwa ajili ya ibada za kawaida na kusikiliza mafundisho. ila wanawake hawakuruhusiwa kupita eneo hili kwenda ndani zaidi kuelekea madhabahuni (eneo lililoitwa Ezrat Yisrael ambalo lilikuwa maalum kwa wanaume tu).

Hadi leo, katika madhehebu ya kiorthodox ya Kiyahudi (ambayo yanafuata sheria za kale za Torati), wanaume na wanawake hukaa sehemu tofauti, mara nyingi zikitenganishwa na ukuta au pazia liitwalo Mechitza.

katika ukristo kwenye Mila za Kale
Kwa karne nyingi, katika makanisa mengi ya kale (ikiwemo baadhi ya makanisa ya Orthodox na Katoliki ya Mashariki), wanaume walikaa upande mmoja wa kanisa na wanawake upande mwingine.

Ingawa Biblia haisemi waziwazi ila inasisitiza juu ya utaratibu na staha. Kwa mfano, katika 1 Wakorintho 14:34-35 na 1 Timotheo 2:11-12, kuna maelekezo yanayoweka mipaka ya ushiriki wa wanawake katika mazingira fulani ya ibada ya hadhara ili kudumisha utaratibu.

Ki ufupi Mgawanyo wa jinsia si jambo la kiislamu pekeeni utaratibu uliokuwepo katika dini zote za Ibrahimu (Uyahudi, Ukristo, na Uislamu) kwa lengo la kudumisha staha na heshima katika nyumba za ibada, ingawa Ukristo wa kisasa katika madhehebu mengi umeacha utaratibu huo.
 
Back
Top Bottom