Huwa wanawake wa hivyo Mimi siwatongozagi siku hio hio.
(Simu inaitwa na kupokelewa sauti ya kike upande wa pili inasikika).
Demu: Hello
Mimi: Hello mambo
Demu: poa.
Mimi: Nambie
Demu: Mmmmmh! (Kmya kidogo) kwani nani mwenzangu?
Mimi: ooh sorry. Nitakuwa nimekosea namba.
Demu: Ok.
Mimi: Poa. Bt sorry kwa usumbufu.
Demu: Usijali, kwani ulikuwa unampigia nani?
Mimi: Dada yangu.
Demu: Sawa, utakuwa umekosea namba.
Mimi: poa, ila nimeinjoi kuongea na wewe.
Demu: kwa nini?
Mimi: una sauti nzuri kweli.
Demu: Mmmmh! Ahsante.
Mimi: nadhani unafanana na sauti yako.
Demu: Badae Bhana coz sa hivi ninakazi.
Mimi: Daa samahani kwa kukupotezea muda jaman.
Demu: wala hujanipotezea muda. Badae jioni nipo free.
Mimi: Basi ntakutafuta hiyo jioni.
Demu: sawa ila angalia hiyo namba vizuri.
Mimi: Poa. Byyeee
Demu: oewky.(simu inakatika).
Jioni ikafika.
(Nachukua simu natuma text kwa yule demu).
Mimi: Mambo (inapita dakika tano text haijibiwi. Baadaye text inaingia kwa simu yangu).
Demu: poa nambie.
Mimi: niko fresh mrembo.
Demu: mmmh! Aliyekuambia Mimi mrembo ni nani na hujawahi kuniona?
Mimi: Nilikuambia Sauti yako inatosha kunijulisha kuwa wewe ni zaidi ya mrembo labda uniwie radhi kwa kukuita mrembo kwani wewe ni zaidi ya mrembo.
Demu: mmh! Makubwa(huku akicheka).
Mimi: Umenisamehe lakini?
Demu: nimekusamehe?
Mimi: ndio
Demu: kwani umenikosea nini?
Mimi: si nimekuita mrembo wakati wewe ni zaidi ya mrembo.
Demu: hahaahaaaaa!! Unamambo wewe. Sipati picha demu wako.
Mimi: unanisingizia tuu. Wala sina maneno zaidi ya kuongea ukweli.
Demu: (anacheka kidogo) tuachane na hayo. Ulimpata Dadaako.
Mimi: Ndio. Aah! Kumbe nilikosea namba ya mwisho.
Ila afadhali nilikosea.
Demu: afadhali ulikosea?
Mimi: ndio.
Demu; kwa nini?
Mimi: huoni naongea na mtoto mrembo Kama wewe.
Demu: mmmmh!
Mimi: yaani ni Kama bahati vile.
Demu: Bahati gani?
Mimi: kuongea na wewe.
Demu: wewe unamatatizo sio bure.
Mimi: matatizo kidogo.
Demu: kumbe umejiona eee!
Mimi: wahenga wanasema ukisikia sauti ya malaika lazima upagawe.
Demu: hahahaaaaa! Sasa wewe sauti ya malaika umeisikia wapi?
Mimi: nimeisikia leo tena ninaongea nayo.
Demu: unamaneno wewe.
Mimi: niotee jina lako.
Demu: huwezi kuotea.
Mimi: Na nikiotea...?
Demu: huwezi kuotea nasema.
Mimi: nambie utanipa nini?
Demu: Ntakupa zawadi.(kmya kidogo) ila usije kuwa unanijua alafu unanichora hapa.
Mimi: nikujulie wapi weeye.
Demu: haya otea.
Mimi: unaiii....twaaa...desh desh
Demu: hahaaaaa. Otea sasa.
Mimi: Unaitwa Neema.
Demu: huyooo umekosa.
Mimi: siwezi kukosa Mimi wewe.
Demu: Ndio umekosa sasa.
Mimi: haya nambie unaitwa nani?
Demu: muone mbwembwe zote umekosa.
Mimi: nambie sasa.
Demu: naitwa Grace.
Mimi: hahaaaa!! Huyoooo hata hajui maana ya Grace kwa kiswahili.
Demu: najua. Ila umejitahidi.
Mimi: zawadi yangu.
Demu: nitakupa.
Mimi: sawa.
Demu: Na wewe unaitwa nani?
Mimi: na wewe otea.
Demu: mi siwezi kuotea.
Mimi: basi usijali mtoto malaika, niite Michaelray.
Hiyo ngoma utaendelea kwa wiki zima mpaka mtoto anajaa mwenyewe.
Shida ya wanaume wengi wanaharaka na mbinu hii ambayo huhitaji muda.
Ninauzoefu nayo Sana hii. Kila mwanamke ananamna yake ya kuingiliwa.