OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,200
- 103,735
Kila nikijaribu kupitia maoni ya wananchi katika mitandao ya kijamii ni dhahiri wananchi wengi wanaonekana kukosa imani na serikali ya awamu ya sita. Ukiwasoma kwenye mitandao utaona wamekaa kimashaka-mashaka tu hivi. Kila serikali ikisema hivi kuhusu matumizi ya fedha na miradi basi wao wanahisi kuibiwa ibiwa tu.
Hali hii pia ipo katika maisha ya kawaida. Wameweka imani ndogo sana na uongozi wa mama.
Hali hii inachochewa sana na serikali kupinga katiba mpya. Wananchi wanajiuliza kwa nini hawataki katiba mpya, au wanataka wakiiba wasiulizwe?
Eti jamani kwa nini raia wamekataa mkao wa kuibiwa tu?