Serikali iharakishe malipo ya fidia ya 6% kwa wananchi waliohamishwa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni kupisha upanuzi wa Terminal 3

Chikuvi2021

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
459
516
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kwenye hoja zake za Ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021;

- Miongoni mwa hoja alizotoa ni madai au mapunjo ya wananchi wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni ambao wanapaswa kulipwa fidia zao kwa mujibu ya matakwa ya kanuni ya 13(3) ya Ardhi (Uhakiki wa thamani ya fidia ya Ardhi) ya mwaka 2001 iliyofanyiwa marekebisho ya riba ya 6% kwa mwaka.

- Kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya Ukaguzi wa miradi ya maendeleo mwaka 2020/2021, tunanukuu; "Marudio ya tathimini yalizalisha thamani mpya kutoka deni la awali na kufika Tsh. Bilioni 29.78 ikiwa ni ongezeko la Tsh. Bilioni 22.35 sawa na asilimia 302 ikilinganishwa na deni la awali".

-Taarifa ya CAG, ilipendekeza "Ukokotoaji wa gharama za fidia uidhinishwe na Mthamini Mkuu wa Serikali".

- CAG alishauri, "Manejimenti ya Mamlaka ya viwanja vya ndege kushirikiana na Mthamini Mkuu wa Serikali kufanya mapitio ya kiasi cha fidia kinachopaswa kulipwa kwa kaya za Kipawa, Kigilagila na Kipunguni na kuhakikisha kuwa malipo yanafanyika bila kuchelewa kuepuka ongezeko zaidi la gharama za fidia".

Utekelezaji wa hoja za CAG

1) Mwisho wa mwezi July 2023 Waziri wa Fedha akifuatana na Wabunge wa Ilala, Segerea, Viongozi wa Chama na Serikali Wilaya ya Ilala waliitisha Mkutano na wananchi wa Kipunguni, na kuwaambia kuwa zoezi la tathimini kwa nyumba za kipunguni limekamilika na Serikali imejipanga kutoa fidia ya Tsh. Bilioni 140 ifikapo mwezi September 2023.

2) Wananchi wa Kipawa na Kigilagila hawakutajwa kwenye bilioni 140 za fidia, japokuwa CAG kwa tathimini yake aliona fidia ya kaya za Kipawa, kigilagila na kipunguni ni bilioni 29.78, wananchi wa Kipawa na Kigilagila wanaamini kuwa hizo bilioni 140 ambazo zilitamkwa kwenye mkutano na wananchi wa kipunguni zinawahusu (Kipawa na kigilagila).

3) Wananchi wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni walifanyiwa tathimini mwaka 1997 kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya 1969 na malipo ya fidia kwa Kaya za Kipawa na Kigilagila yalifanyika mwaka 2011 kwa Sheria ya 1969, kupisha ujenzi wa terminal 3. wape we maua wakazi wa kipawa na kigilagila kwa kuridhia kuondoka wakati wanasubiri fidia ya 6% kama walivyo ahidiwa na viongozi wa chama na Serikali wa wakati huo.

Ushauri
1) Serikali ya awamu ya 6 iharakishe inalipa fidia ya 6% kwa mwaka kuanzia 1997 mpaka 2023, kwa Wananchi wote wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni mapema kwa maana gharama za vifaa vya ujenzi vinapanda kila Mwaka.

2) Serikali ya awamu ya 6 iharakishe uhakiki wa mali za Kaya za kipunguni na ku-reconcile na orodha ya awali (1997) ili kulipa thamani halisi, vinginevyo kuna uwezekano wa watu wasio waadilifu wakachakachua orodha ya wadai.

3) Chama na Serikali kiitishe mikutano na wakazi wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni kuwapa mrejesho wa madai yao.
 
Siku zote mnaambiwa mtanzania usimtetee utashangaa utakapojikuta uko peke yako, ona sasa hawapo.
 
Hapana,wapo lakini wasemq na Julia mpaka sauti,zimewakauka.Juzi nimewasikia wakazi wa kipunguni wanallilia Wapo Radio,wanaulizia malipo yao,kwa maana hata wapangaji wanahama na huwezi kutoza Kodi, wakati hujui hatima yako.
-Lakini,unachosema inawezekana,unaweza kuta wamelambishwa asali wadai na watoa hoja,na hoja ikafungwa kimya kimya.
-Tanzania wajanja wengi,wakiona wananchi wako kimya na wao , wanakaa kimya.
 
Back
Top Bottom