OkWaliwapa wageni ulaji wakawasahau wenyeji sijui walotaka wenyeji wakale wapi
Katika uzoefu wangu! PHD makaratasi ya uhakiki wa darasani hayajawahi kuondoa uzuzu wa mtu. Hebu ona Magu na PHD zuzu kabisa katika siasa!! hata kwenye PHD kumbe nayo aliiba!Hawa wawili Dr Bashiru Ally na Dr Wilson Mukama ndio makatibu wakuu wa CCM waliojaliwa PhD.
Wengine akina Kawawa, Kolimba, Gama, Kinana, Makamba nk...nk ni wasomi wa kawaida siyo wabobezi labda Gama ndio alikuwa na Udaktari wa zamani.
Najiuliza tu kwanini Bashiru na Wilson wamesahaulika kwa haraka sana tofauti na mzee Makamba au Kinana waliowahi kuitwa na kamati ya maadili ya Lumumba?!
Dominica Njema!
Ndiyo Dr. Bashiru alikuwa PhD holder lakini amefanya ccm kiasi Cha kumfanya watu kumkumbuka? Aliharibu chama Sana Sana kuimba mapambio, kuharibu uchaguzi na mengine mengi! Elimu si tija ya kumfanya mtu kuwa kiongozi mzuri na bora!
Huyo Wilson Mukama Ph.D kaipata lini na wapi?Dunia inaendakasi sana. nilishasahau kuwa CCM ilishawahi kuwa na katibu mkuu aliyeitwa Wilson Mukama
Walipewa nafasi wakaigeuza kuwa "a Road to hell"Siasa za bongo hazihitahi sana PhD bali ujanja ujanja ndivyo sivyo kibao, bla bla maneno meeengi na urongo pia. Ukiwa msomi umenyooka hutaweza kwenda nazo....pia uwe umekulia humo kujua fitna zoote hizo
Historia itamhukumu sana.Live long COMRED Dr Bashiru, historia itakukumbuka!