Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,510
- 7,755
Huyu mwamba Dk Bashiru Ally Kakurwa unaweza kusema ndiyo mwamba wa siasa za Tanzania kwa sasa, licha ya matisho mengi ya kumtaka aombe radhi kutokana na kauli yake ya kuponda wanaosifia anaupiga mwingi lakini aligoma kuomba radhi na hajaomba mpaka leo na hawana cha kumfanya chochote!.
Spika aliyelazimishwa kuachia ngazi Job Ndugai baada ya kulikoroga alikaza siku mbili tu kutokana na presha kubwa ,siku ya tatu akaita waandishi wa habari na kuomba radhi kwamba nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana naomba mnisamehe lakini bado alitolewa, lakini si kwa Bashiru ambaye hakuomba radhi na hajatolewa popote.
Dkt. Bashiru ndiyo aliyeirejesha CCM kwenye msitari ,yani kutoka CCM ya kuzomewa mitaani hadi CCM ya kushangiliwa na kupokelewa kwa heshima mitaani, unapoona bunge limejaa wabunge wa CCM hiyo ni kazi ya Bashiru, unapoona mapato ya CCM yamepanda kutoka millioni 5 kwa mwaka hadi billioni 20 kwa mwaka hiyo ni kazi ya Bashiru!.
Kwa hiyo Dkt. Bashiru anawajua wabunge na viongozi wa CCM kuliko wanavyojijua ndiyo maana hawana cha kumbabaisha na hawamtishi kwa lolote.