Kwanini Wabobezi wa siasa za CCM na wasomi wa falsafa Dkt. Bashiru Ally na Dkt. Wilson Mukama wamesahaulika haraka sana?

Hawa wawili Dr Bashiru Ally na Dr Wilson Mukama ndio makatibu wakuu wa CCM waliojaliwa PhD.

Wengine akina Kawawa, Kolimba, Gama, Kinana, Makamba nk...nk ni wasomi wa kawaida siyo wabobezi labda Gama ndio alikuwa na Udaktari wa zamani.

Najiuliza tu kwanini Bashiru na Wilson wamesahaulika kwa haraka sana tofauti na mzee Makamba au Kinana waliowahi kuitwa na kamati ya maadili ya Lumumba?!

Dominica Njema!
Katika uzoefu wangu! PHD makaratasi ya uhakiki wa darasani hayajawahi kuondoa uzuzu wa mtu. Hebu ona Magu na PHD zuzu kabisa katika siasa!! hata kwenye PHD kumbe nayo aliiba!
Nionavyo mimi ukiwa fundi sana wa kukariri na kuchambua mimambo ya wazungu unakuwa zuzu katika real life. Ukienda SUA, Mlimani na kwingineko utakuta mazuzu ambayo hata familia hayawezi kusimamia!
 
Ndiyo Dr. Bashiru alikuwa PhD holder lakini amefanya ccm kiasi Cha kumfanya watu kumkumbuka? Aliharibu chama Sana Sana kuimba mapambio, kuharibu uchaguzi na mengine mengi! Elimu si tija ya kumfanya mtu kuwa kiongozi mzuri na bora!

Dr. Bashiru ndiye aliyeurudisha utajiri wa ccm mikononi mwa chama! Ndiye aliyefuatilia mali za ccm na kuzisajili RASMI. Mali nyingi za ccm zilikuwa zinaliwa na watu binafsi!! Hiyo ndiyo sababu mafisadi ndani ya chama yanamchukia Sana Bashiru! Kazi hiyo ya kufuatilia Mali za chama ndiyo iligomfanya Magufuli kuridhika na uzalendo wa Bashiru na kumpa nafasi ya katibu mkuu Kisha katibu mkuu kiongozi!!
Alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Magufuli 2025! Bashiru ni mwaminifu, Bashiru Hana tamaa ya Mali, Bashiru hana tamaa ya madaraka! Bashiru ni mzalendo wa kweli! Live long COMRED Dr. Bashiru!! Bashiru ni aina ya kina Nyerere, na yule makamu mwenyekiti wa ccm waliyempiga chini!
 
Dunia inaendakasi sana. nilishasahau kuwa CCM ilishawahi kuwa na katibu mkuu aliyeitwa Wilson Mukama
Huyo Wilson Mukama Ph.D kaipata lini na wapi?
Huyu Mukama alikuwa anabebwa na godfather wake marehemu Kinginge Ngombale Mwillu basi! Kichwani kumejaa pombe basi na porojo nyingi.
The most hopeless Secretary General ccm has ever had!
 
Siasa za bongo hazihitahi sana PhD bali ujanja ujanja ndivyo sivyo kibao, bla bla maneno meeengi na urongo pia. Ukiwa msomi umenyooka hutaweza kwenda nazo....pia uwe umekulia humo kujua fitna zoote hizo
Walipewa nafasi wakaigeuza kuwa "a Road to hell"
 
Bashiru lini alikua mbobezi jamani?, Wabobezi wapo bana, akina Tyson,, George mkuchika, mizengo pinda,, hao ndio wabobezi wa siasa za nchi hii
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom