Kwanini Wabobezi wa siasa za CCM na wasomi wa falsafa Dkt. Bashiru Ally na Dkt. Wilson Mukama wamesahaulika haraka sana?

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,315
2,000
Wote uliowataja waliidumbukiza ccm matatani

Mukama huyu ndo hakufanya lolote tushukuru mze kinana kuja kuitoa ccm shimoni ilikokua imeelekea

Dr Bashir -kuibadili ccm kua ya kikomunist fully Hilo limemmaliza kabisa ,kutoka kijana pendwa kwenye medani zasiasa na uhojaji Mambo Hadi kuonyesha PhD sio ishu Sana
Kiitikadi chama cha CCM ni cha mlengo gani?
 
kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,635
2,000
Ukitaka kujua rangi halisi ya binadamu mpe utajiri haraka au madaraka (katika sayansi tungeita litmus test). Akibaki na utu ule ule wa awali basi huyo ndiye binadamu wa kupigiwa mfano. Wapo wachache sana duniani wa kupigiwa mfano.
huo ndo ukweli mkuu
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,315
2,000
Hakieleweki ,mixed pengine ,mlengo Kati kushoto kipo Kati kulia kipo (ujamaa kipo na ubeberu kipo)
Watanzania niwabeberu tayari kuwarudisha kusikoeleweka utakwisha
Viambatanishi! Na si mnasema wafuate Katiba?

Screenshot_20211017-092806_Adobe%20Acrobat.jpg
Screenshot_20211017-092345_Adobe%20Acrobat.jpg
 
Chendembe

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
262
500
Hawa wawili Dr Bashiru Ally na Dr Wilson Mukama ndio makatibu wakuu wa CCM waliojaliwa PhD.

Wengine akina Kawawa, Kolimba, Gama, Kinana, Makamba nk...nk ni wasomi wa kawaida siyo wabobezi labda Gama ndio alikuwa na Udaktari wa zamani.

Najiuliza tu kwanini Bashiru na Wilson wamesahaulika kwa haraka sana tofauti na mzee Makamba au Kinana waliowahi kuitwa na kamati ya maadili ya Lumumba?!

Dominica Njema!
Mwalimu wangu alinifundisha kuwa, katika nafasi za uongozi, maranyingi wanataaluma wenye PhD na professor sio waziri katika nafasi za uongozi na haswa pale uongozi huo unalenga kutoa huduma na maamuzi ya kijamii kwakuwa wanafalsa wanazoziamini na hawapendi kuzigeuka. Pia, hawana uchangamano na maisha halisi ya jamii inayowazunguka Hali inayopelekea kukosa kutambua maisha halisi ya kijamiii.
Aliniambia ni wazuri katika nafasi za ushauri katika nyanja zao.
Alituambia, viongozi wazuri ni kutoka masters kushuka chini.
Hakika nami nakubaliana nae
 
Wakabambee58

Senior Member
Aug 14, 2020
114
250
Hawa wawili Dr Bashiru Ally na Dr Wilson Mukama ndio makatibu wakuu wa CCM waliojaliwa PhD.

Wengine akina Kawawa, Kolimba, Gama, Kinana, Makamba nk...nk ni wasomi wa kawaida siyo wabobezi labda Gama ndio alikuwa na Udaktari wa zamani.

Najiuliza tu kwanini Bashiru na Wilson wamesahaulika kwa haraka sana tofauti na mzee Makamba au Kinana waliowahi kuitwa na kamati ya maadili ya Lumumba?!

Dominica Njema!
Wamesahaulika na Nani? Au ninyi ndio mmewasahau, ushauri nenda lumumba uwaulize!!!!!!!
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,061
2,000
Wote uliowataja waliidumbukiza ccm matatani

Mukama huyu ndo hakufanya lolote tushukuru mze kinana kuja kuitoa ccm shimoni ilikokua imeelekea

Dr Bashir -kuibadili ccm kua ya kikomunist fully Hilo limemmaliza kabisa ,kutoka kijana pendwa kwenye medani zasiasa na uhojaji Mambo Hadi kuonyesha PhD sio ishu Sana
Kitendo cha bashuri kutuletea ukomunist kimemfanya tumuone mtu wa ajabu anayeishi fikra za miaka 60 katika ulimwengu wa kisasa PhD ni muda wa kukaa saratani sio uwezo wa akili
 
keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,200
2,000
Siasa za bongo hazihitahi sana PhD bali ujanja ujanja ndivyo sivyo kibao....bla bla maneno meeengi na urongo pia....ukiwa msomi umenyooka hutaweza kwenda nazo....pia uwe umekulia humo kujua fitna zoote hizo
Pia na kujipendekeza kukiwemo
 
chungachungu

Member
Dec 31, 2020
56
125
unatiwa na kijiti kirefu

bashiru kaingia ccm ikiwa inaingiza 2bn kwa mwaka

leo inaingiza 30bn kwa mwaka kama initiative zake

hilo hauwezi kuambiwa, maana mnapenda wanachekesha na kuongea sana jukwaani
Bilioni 30 si za ruzuku? Kwa ushindi upi was halali ambao chama kilishinda? Aliratibu magenge ya kununua wapinzani kwa kivuli Cha kuunga mkono juhudi za magufuri,, pesa ya dhambi
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
8,015
2,000
Hawa wawili Dr Bashiru Ally na Dr Wilson Mukama ndio makatibu wakuu wa CCM waliojaliwa PhD.

Wengine akina Kawawa, Kolimba, Gama, Kinana, Makamba nk...nk ni wasomi wa kawaida siyo wabobezi labda Gama ndio alikuwa na Udaktari wa zamani.

Najiuliza tu kwanini Bashiru na Wilson wamesahaulika kwa haraka sana tofauti na mzee Makamba au Kinana waliowahi kuitwa na kamati ya maadili ya Lumumba?!

Dominica Njema!
Hakuna katibu mjinga amewahi tokea CCM Kama Bashiru!
 
mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,587
2,000
Ndiyo Dr. Bashiru alikuwa PhD holder lakini amefanya ccm kiasi Cha kumfanya watu kumkumbuka? Aliharibu chama Sana Sana kuimba mapambio, kuharibu uchaguzi na mengine mengi! Elimu si tija ya kumfanya mtu kuwa kiongozi mzuri na bora!
Na mbaya zaidi Bashiru, Polepole na Majaliwa wakataka kuchukua nafasi ya urais baada ya msukuma kufariki.
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
2,547
2,000
Channel 10 si ameporwa Rostam Azizi na shetani.

Ameporwa au imerudishwa ilipokuwa imeibwa. Kuna majengo, mali lukuki zilirudishwa baada ya mapendekezo ya kamati ya uhakiki ya Dr Bashiru.

Vingi vilichukuliwa kiufisadi, kutumia rushwa, ubabe, uporaji nk.

Kazi alioifanya hapo ndio ilimfanya ateuliwe kuwa katibu mkuu kutoka UDSM. CCM wamshukuru sana huyu.
 
mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,587
2,000
unatiwa na kijiti kirefu

bashiru kaingia ccm ikiwa inaingiza 2bn kwa mwaka

leo inaingiza 30bn kwa mwaka kama initiative zake

hilo hauwezi kuambiwa, maana mnapenda wanachekesha na kuongea sana jukwaani
Bashiru huyu huyu aliyeenda kumwambia Samia “magufuri amesema ujiuzuru hawezi kuendelea kufanya kazi na wewe” kwenye nafasi ya makamu wa rais ili yeye na genge lake (majaliwa, polepole na bashiru) wachukue nafasi za juu baada ya kusikia msukuma alikufa muda mrefu wakaendelea kutwambia hajafa ili wapindue meza!?!?

hawa hawafai wasahaulike tu na siasa zao za tamaa na ulafi wa madaraka.
 
Kamugumya

JF-Expert Member
Aug 18, 2021
910
1,000
Na jambo la kushangaza CCM chini ya uongozi wao hamna la maana walilolifanya. Mukama viatu vya Mzee Makamba vilimpwaya kabisa. Na bila JK kumrudishia Komredi Kinana kuchukua nafasi ya Mukama CCM ilishakuwa hali mbaya. Turudi kwa Bashiru kafanya nini cha maana kwenye chama zaidi ya kusifia? Alikuwa naye mungumtu akifikia hatua ya kutishia kuwafukuza kazi watendaji wa serikali msajili wa vyama na Waziri wa Tamisemi. Lilikuwa janga. Wote wawili hamna anayemsogelea Mzee Makamba wala Komredi Kinana wale walikuwa wameandaliwa kuwa viongozi na hawakuwa na roho mbaya.
 
mpondamali

JF-Expert Member
Sep 5, 2011
462
250
Hawa wawili Dr Bashiru Ally na Dr Wilson Mukama ndio makatibu wakuu wa CCM waliojaliwa PhD.

Wengine akina Kawawa, Kolimba, Gama, Kinana, Makamba nk...nk ni wasomi wa kawaida siyo wabobezi labda Gama ndio alikuwa na Udaktari wa zamani.

Najiuliza tu kwanini Bashiru na Wilson wamesahaulika kwa haraka sana tofauti na mzee Makamba au Kinana waliowahi kuitwa na kamati ya maadili ya Lumumba?!

Dominica Njema!
Dr .Bashiru c mtu wa CCM.....uteuzi ndio ilibidi awe.lkn
 
kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,635
2,000
Bilioni 30 si za ruzuku? Kwa ushindi upi was halali ambao chama kilishinda? Aliratibu magenge ya kununua wapinzani kwa kivuli Cha kuunga mkono juhudi za magufuri,, pesa ya dhambi
Mwambie zilikua zinatoka kwamajambazi Kama sabaya na vyazo vingine harafu wanapika data zaccm
 
kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,635
2,000
Viambatanishi! Na si mnasema wafuate Katiba? View attachment 1977152 View attachment 1977153
Ujamaa ulikataliwa na nyerere mwenyewe toka 1992 ,aliamua kutumia fikra za kambona upumbavu uliofanyika wanashindwa kufuta kimaandishi kwasababu ya ujinga uliokuwepo kwa wananchi kutokuelewa na kuhoji

Leo hii kizazi kinaona mienendo ya Imani yetu kisiasa inavobakwa kwamana yakutoeleweke wananchi wanavohoji yanayotukuta ndohaya ...pia unakuta wasomi nao wanaoteuliwa hushauri wakiwa nje wakiingia ndani wanatumiwa Tena kukidhana na waliyokua wakinena kabla hawajaingia katika mapipa ya serikali
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
2,547
2,000
Na jambo la kushangaza CCM chini ya uongozi wao hamna la maana walilolifanya. Mukama viatu vya Mzee Makamba vilimpwaya kabisa. Na bila JK kumrudishia Komredi Kinana kuchukua nafasi ya Mukama CCM ilishakuwa hali mbaya. Turudi kwa Bashiru kafanya nini cha maana kwenye chama zaidi ya kusifia? Alikuwa naye mungumtu akifikia hatua ya kutishia kuwafukuza kazi watendaji wa serikali msajili wa vyama na Waziri wa Tamisemi. Lilikuwa janga. Wote wawili hamna anayemsogelea Mzee Makamba wala Komredi Kinana wale walikuwa wameandaliwa kuwa viongozi na hawakuwa na roho mbaya.

Chini yao mali nyingi za chama ziliibiwa, kupewa watu binafsi kwa mikataba ya hovyo, ufisadi, ubadhilifu ulitamalaki hadi kushindwa kuwalipa baadhi ya makada wao.

Pesa za kampeni walikuwa wanategemea mikopo, msaada wa watu kama Rostam Aziz.

Sasa hivi wana vyanzo vyao vinayowaingizia pesa za kutosha, ingekuwa vizuri CCM wakaacha kuchukua ruzuku.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom