Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Mkuu
Ni kwamba kila kitu kina maandalizi. maandalizi ya akili nayo pia huhitajika ili ujikomboe kama mtu mmoja au kikundi na hatimaye taifa kwa ujumla wake.
Sisi kwa ujumla hatukuandaliwa, au niseme tumeandaliwa kushindwa.
Kwanza ni vitu tunavyojifunza shuleni vinatuandaa kuwa wanyonge mbele ya wengine, namaanisha hii historia. Inatufunza kuona kuwa kuna watu wanatuzidi kwa kila kitu hivyo mpaka maamuzi juu yetu.
Mfano mzuri wa hilo ni hata viongozi mbadala wa waliopo, utaona ukikwaruzana na watoa misaada, wao ndo wa kwanza kusema tutanyimwa misaada na taifa litaangamia. Sijawahi kuona kiongozi asiyesifia misaada na hili limeenda mbele zadi kwamba lazima uwe na chama rafiki huko ili kikusaidie kupata madaraka.
Pili ni tamaa ya viongozi wenyewe, namaanisha kuwa siasa ni kama ajira sawa na ajira nyingine. Mbaya mwanasiasa anataka awe na nguvu kuliko wale waliomuweka madarakani. Kuwa na nguvu lazima uwanyanyase na kuwatisha walio wanyonge ili wakusujudia, hapa huhitaji kwenda GYM, lazima uwe na peas kuwazidi, tena kwa mbali. Hapa ndo mwanasiasa anapotafuta pesa kwa njia yoyote ile ili awe SUPERIOR kuliko wengine. Wale ambao ataona kuwazidi kifedha hataweza, anaungana nao kuwanyayasa walio wanyonge,NDO MISAADA inapoanzia.
Kwa ujumla mwanasiasa hatashughulika na matatizo ya wananchi mpaka atosheke yeye, na nakuhakikishia hatatosheka mpaka na hivyo ataenda mbali zadi kuhakikisha anajenga urafiki nje ya mipaka kwa kutumia rasilimali za nchi kujiimarisha, huu ni MWANZO WA MISAADAya kimataifa.
Tatu ni mataifa yatoayo misaada kunufaika kwa mgongo wa nyuma, waweza kudhani ni wema sana, la hasha, bali nyuma ya pazia akitoa moja moja anapata mbili. Naye kwa upande wa pili atajitahidi kwa hali na mali kukuaminisha kuwa wewe huwezi bila yeye na yupo tayari kukusaidia ili wewe usiishughulishe akili.
Namalizia kwa kukili kuwa kuna mikataba inayoyalazimisha mataifa yale yatusaidie, na ndo hiyo hiyo inawapa fursa ya kuchukua mali gafi kwa bei poa na kutuuzia kwa ghali baada ya kuboresha.