Kwanini Waafrika Tunahitaji Misaada tuko nje ya Bara letu?

Ww hapo ulipo umefanya nini mpaka sasa ambacho kimesaidia watu? Sana sana umepata elimu yako ya vyeti na kushia kuajiriwa. Huna chochote cha maana unachozalisha. Cha maana ni kufurahia ubazazi wa viongozi na kusujudu mawazo ya kisadikika. Katoe ajira hata 1,000 kwa wazo lako, kisha uje na verified id kwamba tusitegemee misaada kwani ww umeweza jambo fulani.
Ni swali zuri. Mimi sijatoa ajira hata moja rasmi lakini nina vijana kama tano ninawapa kazi kwa kutegemea uwepo wa tender. Na bado napambana nikuze biashara zangu lakini hali yangu ya kimaisha haininyimi haki ya kuhoji utegemezi wa Afrika.
 
Tunanyoosha vidole kwa viongozi kwanza, wengi wa viongozi wa kiafrika hupatikana kwa mifumi mibovu mfano halisi ni hapa kwetu. Nusu ya viongozi wetu wa kuchaguliwa hupatikani kwa dhuluma na wakishatangazwa washindi huhakikisha wanalinda mazingira yote ya dhuluma ili waendelee kukaa madarakani. Mfano hapa nchini utasikia kiongozi anasema katiba sio muhimu bali wananchi wanataka maji, afya nk. Anaipinga katiba ili atawale kwa mitazamo yake bila kushirikisha wengine, matokeo yake viongozi wazuri wa kuweza kuliongoza taifa hawapatikani kwani viongozi halisi hawawezi kutumia dhuluma kupata uongozi.
Kama jamii inajielewa kwanini inaruhusu mifumo mibovu na viongozi wa ajabu waendelee kuharibu ustawi wao. Tuwe wa kweli jamii zenye uelewa zinasimamia viongozi wao wanapokosea sisi tunaishia kulalamika na kusubiri wazungu watusaidie "utegemezi mwingine ".
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Kwa IQ ndogo ya viongozi kama Magufuli lazima tuwe tegemezi
 
Kama tunasaidiwa toka 60's hadi leo unadhani hii njaa itaisha? Kuna vizazi vinne vimepita toka 60's.. Babu, Baba, mtoto hadi mjukuu bado wote wana njaa? Lini watajilisha?
nafikiri shida ni watoa msaada, misaada yao imeka kimitego ndo hadi tokea 60's hadi leo nishida kuji nasua mkuu.ukitaka tupone nikujitoa kwenye mambo yao tuh.
 
Yes ni madhara ya mfumo uuitwao uraisi, bila kuubadili mfumo huu tutakuwaomba omba na masikini milele,mfumo wa uraisi unafaa ulaya na marekani na sio Africa.
Mfumo mzima, Afrika mambo ni vice versa hata mwenyekiti wa mtaa anataka kuwa juu ya wananchi wake. Mbaya zaidi wananchi hawatambui Kiongozi ni mtu waliochagua asimamie agenda zao na siyo Mungu au special kuliko wao. Hii dhana ya kuwaona viongozi wapo juu yetu inatulemeza tusubiri watuletee maendeleo na kuogopa kuwatoa pale wanapoenda kinyume mkataba yetu/ahadi zao walizotoa wakati wa uchaguzi. Uwa sioni mantiki ya kusubiri mtu akae miaka tano kama anaturudisha nyuma.
 
nafikiri shida ni watoa msaada, misaada yao imeka kimitego ndo hadi tokea 60's hadi leo nishida kuji nasua mkuu.ukitaka tupone nikujitoa kwenye mambo yao tuh.
Ningependa na sisi tunaopokea misaada ya kimitegeo tuanze kujitadhimini lazima tutakuwa na shida kuanzia viongozi wetu hadi wenyewe la sivyo hali zetu hazitabadilika.
 
Tatizo ni wakoloni weusi, Africa bado haijapata mfumo sahihi wa uongozi, huu uitwao Uraisi ndo kuongoza wengi tutegemee umasikini zaidi.Ni hadi tubadili mfumo nchi zisiongozwe na MTU mmoja Bali kundi la watu.Mwafrica hana uwezo wa kumuongoza mwafrica mwenzake ataishia kumletea umasikini mwafrica mwenzake, atamfilisi,atamuuwa,atamteka,na madhila ya kila hali

Kati ya kuongozwa na mwizi na mnyang'anyi mmoja au kuongozwa na wezi na wanyang'anyi mia, ni kipi kibaya zaidi?
 
Viongozi wetu wamekosa ubunifu na kuumiza ubongo kufikiria,muda wote wanataka kutafuniwa tu
 
Karibuni nimekuwa nikijiuliza sana hili swali lakini sipati jibu. Waafrika ni binadamu waliokamilika kama wenzetu wa mabara mengine lakini kwanini tunakuwa tegemezi? Kwanini tuliweza kuishi na kuendela na maisha yetu kabla ya wazungu na waarabu kuja kwenye bara letu na sasa tunashindwa kuishi na kujiendeleza bila wao? Naamini tukiweza kujibu haya maswali kwa dhati tutakuwa huru.
Kwasababu kabla ya uhuru,tulikuwa hatuzidi million 9 nchi nzima....so tulikuwa hatuhitaji misaada kihivyo.

Sasahivi tuko million 50 na magonjwa mengi yanahitaji msaada wa nje,kama HIV hatuna uwezo wa kununua hizo dawa,watoto ambao tunaambiwa tuwazae tu,wanahitaji elimu ambayo serikali haiwezi kulipia.

Kiufupi huduma nyingi za kijamii hatuwezi kuzimudu, tunahitaji hiyo misaada toka nje kutokana na watu wengi tulionao.
 
Ndugu watu wengi watakupa majibu meeeengi lakini mimi nadhani jibu ni jepesi tu - VALUE CREATION basi. Muda hautoshi kudadavua hili kwa sababu ya muda lakini waafrika tumekuwa hatu-create value that is why tuko nyuma. Nitakupa mfano hapo ulipo kuanzia suruali, chupi, soksi, shati, saa, kiatu, computer unayotumia hapo, calculator, printer kuna kilichozalishwa Tanzania au Afrika? jibu ni hapana hivyo vitu ni value iliyozalishwa na watu wa nje.Maana yake ni kwamba hiyo pesa wametajirika nayo watu wa nje ya bara hili kwa hiyo as long as mnawategemea kwenye value creation ina maana pesa yenu haizunguki miongoni mwenu, inazunguka kidogo miongoni mwenu inatoka nje ya nchi na huo ndo mwanzo mkubwa wa umaskini wetu. Mfano mdogo chunguza hapo nyumbani kwako kuanzia gari, TV, taulo, shuka ya kujifunika vyote vimetoka nje ya nchi hii maana yake watu wetu wengi hawana ajira na kwa kuwa watu wetu hawana ajira serikali inaishia kupata mapato kidogo kwa kuwa inakusanya kutoka kwenye vyanzo vichache matokeo yake inabidi serikali zetu ziwapigie magoti wazungu ili tuweze kujazia kidogo tulichokusanya.

Suala muhimu la kujiuliza ina maaana mpaka karne hii tumeshindwa kutengeneza glass ya kunywea maji mpaka tuiagize China? So the bottom line is that as long as we remain dependent to other countries to facilitate exchange of goods and services we will remain poor
 
Tunawahitaji sana sana tena nyakati za Uchaguzi mkuu waiisimamie tume iihi feki uone afrika itakavyobadilika vitambi vyaCCM vitasinyaa ndani ya masaa kadhaa.
 
Kawaida watu wakiongezeka tena kama wengi ni vijana kuliko wazee basi uchumi unatakiwa ukuwe.
 
Sababu tunapenda kuishi kama wao
Na siyo kama sisi. Hii inaweza kuwa sababu kwasasa hatuna miundo yetu ya kiuchumi wala hatuzienzi tamaduni zetu. Tumetekwa kiakili na kitamaduni.
 
Tunawahitaji sana sana tena nyakati za Uchaguzi mkuu waiisimamie tume iihi feki uone afrika itakavyobadilika vitambi vyaCCM vitasinyaa ndani ya masaa kadhaa.
Sawa kabisa mabadiliko muhimu lakini ukiangalia kwa mtazamo wa kiafrika nchi kama Kenya, Ghana, Senegal, Malawi, Zambia, Nigeria zimetoa vyama vyao vilivyokuwa vinatawala lakini bado ni tegemezi. Mimi nina tatizo na Afrika kuwa tegemezi na hiyo njia ya kubadilisha vyama bado haijatatua hili tatizo.
 
Uchumi hauwezi kukua kama hakuna njia za kuzalisha....

Elimu yetu haikuzi watu wakawa wabunifu,Wenye nchi hawapendi watu wabunifu ambao wana'challenge status quo kwa ubunifu wao.

Kama unatengeneza Jamii ambayo haiwezi kufikiria na unashindwa kuiwezesha,huwezi kukuza huo uchumi.
 
Sawa kabisa mabadiliko muhimu lakini ukiangalia kwa mtazamo wa kiafrika nchi kama Kenya, Ghana, Senegal, Malawi, Zambia, Nigeria zimetoa vyama vyao vilivyokuwa vinatawala lakini bado ni tegemezi. Mimi nina tatizo na Afrika kuwa tegemezi na hiyo njia ya kubadilisha vyama bado haijatatua hili tatizo.
Angalao CCM itoke tupumue labda sisi ndio tutakua waanzilishi na tuna historia hiyo.
 
Ndugu watu wengi watakupa majibu meeeengi lakini mimi nadhani jibu ni jepesi tu - VALUE CREATION basi. Muda hautoshi kudadavua hili kwa sababu ya muda lakini waafrika tumekuwa hatu-create value that is why tuko nyuma. Nitakupa mfano hapo ulipo kuanzia suruali, chupi, soksi, shati, saa, kiatu, computer unayotumia hapo, calculator, printer kuna kilichozalishwa Tanzania au Afrika? jibu ni hapana hivyo vitu ni value iliyozalishwa na watu wa nje.Maana yake ni kwamba hiyo pesa wametajirika nayo watu wa nje ya bara hili kwa hiyo as long as mnawategemea kwenye value creation ina maana pesa yenu haizunguki miongoni mwenu, inazunguka kidogo miongoni mwenu inatoka nje ya nchi na huo ndo mwanzo mkubwa wa umaskini wetu. Mfano mdogo chunguza hapo nyumbani kwako kuanzia gari, TV, taulo, shuka ya kujifunika vyote vimetoka nje ya nchi hii maana yake watu wetu wengi hawana ajira na kwa kuwa watu wetu hawana ajira serikali inaishia kupata mapato kidogo kwa kuwa inakusanya kutoka kwenye vyanzo vichache matokeo yake inabidi serikali zetu ziwapigie magoti wazungu ili tuweze kujazia kidogo tulichokusanya.

Suala muhimu la kujiuliza ina maaana mpaka karne hii tumeshindwa kutengeneza glass ya kunywea maji mpaka tuiagize China? So the bottom line is that as long as we remain dependent to other countries to facilitate exchange of goods and services we will remain poor
Nashukuru sana kwa maelezo mazuri. Inaonekana unajua mengi, kwanini hatuamini tunaweza ku create value bila kutegemea teknolojia ya wazungu au msaada wa serikali?
 
Shinda ni hii mkuu HATUNA VIONGOZI WENYE AKILI TIMAMU,angalia swali la korosho, kiongozi gani mweye akili timamu anaweza fanya vile huyu kiongozi wetu amefanya?badala la kutatua tatizo kwa kutumia akili, tunatatua tatizo kupitia mabavu na vicha tupu,hio ndio shinda mkuu
Acheni kusingizia viongozi, individualy we're like/ worse than our viongozi.
 
Back
Top Bottom